Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Taarifa yake iliyonukuliwa na Vyombo vya Habari hii hapa
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, Tundu Lissu ameitaka Serikali ya Kenya kuingilia kati katika madai ya kutekwa kwa mwanaharakati Maria Sarungi.
Taarifa za kutekwa kwa Maria zimesambaa leo Jumapili Januari 12, 2025 baada ya mtandao wa kimataifa wa haki za binadamu-- Amnesty International kuripoti taarifa hiyo.
Soma Pia: Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi
“Maria alikuwa amekimbilia uhamishoni nchini Kenya tangu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo amekuwa akiendesha televisheni ya mtandaoni ya Mwanzo TV, inayotoa maudhui ya kuunga mkono demokrasia.
“Ingawa tunatumai na kusali kwa ajili ya maisha na usalama wa Maria, ni lazima tutoe wito kwa Serikali ya Kenya na watu wote wenye nia njema kutoka duniani kote kuingilia kati, kuhakikisha usalama wa Maria,”ameandika Lissu.
Mwananchi
