Tundu Lissu aitaka Serikali ya Kenya Kuingilia kati kutekwa kwa Maria Sarungi

Tundu Lissu aitaka Serikali ya Kenya Kuingilia kati kutekwa kwa Maria Sarungi

Zamani kwenye kifurushi cha TV nilichokuwa nanunua kuna channel ilikuwa inaitwa ‘bad movies’ (literally).

Humo kulikuwa kuna cinema ukiangalia script unaweza sema imeandikwa na mtoto wa miaka kumi. Yaani kulikuwa na cinema unakuta story mbaya kweli kweli na poorly shot film, just bad movies.

Ndio hii cinema ya Maria (what a coincide) mtu anamrekodi Maria going about her business; mara vuu anatekwa tena mbele ya watu. Two hours later she if found unharmed in her house.

Si achukue passport ya upande wa mama ake, aende popote kuishi duniani anapotaka kama kachoka kuishi Kenya kuliko kutengeneza cinema mbovu ivyo.
 
Sasa Lisu anaposema anaitaka Serikali ya Kenya iingilie, anamaanisha nini kaongea na nani huko Serikali ya Kenya?
serikali ya kenya iingilie kati ili waliomteka maria sarungi wajulikane ni kina nani, hatua za kisheria zichukue mkondo wake
 
Taarifa yake iliyonukuliwa na Vyombo vya Habari hii hapa

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, Tundu Lissu ameitaka Serikali ya Kenya kuingilia kati katika madai ya kutekwa kwa mwanaharakati Maria Sarungi.

Taarifa za kutekwa kwa Maria zimesambaa leo Jumapili Januari 12, 2025 baada ya mtandao wa kimataifa wa haki za binadamu-- Amnesty International kuripoti taarifa hiyo.

Soma Pia: Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi

“Maria alikuwa amekimbilia uhamishoni nchini Kenya tangu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo amekuwa akiendesha televisheni ya mtandaoni ya Mwanzo TV, inayotoa maudhui ya kuunga mkono demokrasia.

“Ingawa tunatumai na kusali kwa ajili ya maisha na usalama wa Maria, ni lazima tutoe wito kwa Serikali ya Kenya na watu wote wenye nia njema kutoka duniani kote kuingilia kati, kuhakikisha usalama wa Maria,”ameandika Lissu.

View attachment 3200002View attachment 3200003

Bila shaka ma CCM na Ile timu pendwa ya mwamba walifurahi mno huyo mdada yalivyomkuta.

fazili au nasema uongo?
 
Bila shaka ma CCM na Ile timu pendwa ya mwamba walifurahi mno huyo mdada yalivyomkuta.

fazili au nasema uongo?
Wapenda haki tunalaani vikali yote yaliyomkuta huyo dada na haya yote yanaonesha jinsi serikali hii ya CCM ilivyo na uharamia kwa wananchi wake.
 
Wapenda haki tunalaani vikali yote yaliyomkuta huyo dada na haya yote yanaonesha jinsi serikali hii ya CCM ilivyo na uharamia kwa wananchi wake.
Wamesahau kwamba Kenya kuna Base ya Jeshi la Marekani kuzuia ugaidi, Wameumbuka sana!
 
Nasikia ilikuwa ni kiki tu kama ile ya Abdul Nondo😁

Lengo ni nini ku-stage tukio hilo?

Ili kuandaa justifications za kuombea 'asylum' nchi za ng'ambo?

Ili kuchafua tawala za Kenya na Tz?

Bado haingii akilini.

Inawezekana ametekwa kweli.

-Kaveli-
 
Haya Matamko huwa wanayatoa baada ya kuwasiliana na hizi serikali au wanaongea tu?

Lisu kawasilina na nani katika Serikali ya Kenya na kumtaka aingilie kati utekwaji wa Maria Sarungi?

Unaitakaje serikali ingilie kati kana kwamba unawafahamu watekaji?
Shule ulienda kusomea ujinga? Jukumu la kila serikali ni kulinda usalama wa raia wake kwahiyo iwe serikali imehusika au haijahusika ni sahihi lisu kutoa tamko hilo kama umeumia nenda kizi mkazi kanywe madafu
 
JPM alisingiziwa mabaya mengi sana
jPM ndiye muasisi wa huu unduli wa kuteka na kupoteza watu. Huyu kigagula wa Zenji anatembelea mulemule kwa kuwa amegundua hawa kondoo hata ukikamata mmoja mmoja na kuchinja, hakuna wanachoweza fanya.
 
jPM ndiye muasisi wa huu unduli wa kuteka na kupoteza watu. Huyu kigagula wa Zenji anatembelea mulemule kwa kuwa amegundua hawa kondoo hata ukikamata mmoja mmoja na kuchinja, hakuna wanachoweza fanya.
Mbona ata huko Kenya inasemekana kuna matukio ya utekaji?
 
Njaa zote izo mkishiba wala hatusikii makelele haya
Maria angeamua kua upande wa kishiba wala asingepata shida kupata cheo chochote serikalini; baba yake alikua moja ya senior ministers kwa muda mrefu tu, kahudumu enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa; kaamua mwenyewe kufanya anacho kiamino from her heart na sio tumbo lake. Nadhani ni makosa makubwa sana au uvivu wa kuijua historia yake ndio inaweza sababisha ntu kuandika kama hivo
 
Back
Top Bottom