Tundu Lissu aitaka Serikali ya Kenya Kuingilia kati kutekwa kwa Maria Sarungi

Tundu Lissu aitaka Serikali ya Kenya Kuingilia kati kutekwa kwa Maria Sarungi

Haya Matamko huwa wanayatoa baada ya kuwasiliana na hizi serikali au wanaongea tu?

Lisu kawasilina na nani katika Serikali ya Kenya na kumtaka aingilie kati utekwaji wa Maria Sarungi?

Unaitakaje serikali ingilie kati kana kwamba unawafahamu watekaji?
 
Serikali ya Kenya imekataa kutumika kuua watu
hata hivyo inaonekana ni serikali dhaifu! Inakuwaje watekaji wa nchi zingine wanaingia katika ardhi yake bila kujulikana kisha wanafanya utekaji?
 
Waaambieni vijana waende shamba wakalime

Harakati sio jambo jepesi

Unafanya harakati hela ya nauli unagongea kwa mbowe?

Wapumbavu nyie

Wapeni vijana njia watafute maisha yao
hukohuko shambani harakati zinafanywa hata kama huna hela
 
Maria kakosoa utawala wa magu na akawa salama!
Kamkosoa Samia Kawa salama!

Kajaribu kukosoa uenyekiti wa Mangi wamepita nae!
Uenyekiti wa CHADEMA una Nini? Kwanini kila anayejaribu kuchallenge anashughulikiwa namna hii?
Kwanini kila anayegombea uenyekiti wa Mbowe lazima aumizwe?
mbowe ana maguvu kama ya dola? Anaweza kufanya uharamia mpaka kwenye nchi ya kigeni?
 
Najua ilikuwa kiki Bro! Hata aliyekuwa Makamu wetu aliwahi kusema kwamba askari wa Tanzania aliyefundishwa vizuri atumie risasi 16 halafu ubaki hai! Hakuna kitu kama hicho nami nakubali hilo!
maoni ya kishenzi, ujiumize kiasi cha kufa kisa kutaka kiki? Huu ni uchuro
 
Kenya hakuna usalama tena.
Yule jamaa wa Uganda kanyakuliwa kama kifaranga.
kenya imeonekana kuingiliwa na maharamia kirahisi na kufanya yao, ulinzi na usalama ni sifuri, hata magaidi huingia kirahisi
 
Haya Matamko huwa wanayatoa baada ya kuwasiliana na hizi serikali au wanaongea tu?

Lisu kawasilina na nani katika Serikali ya Kenya na kumtaka aingilie kati utekwaji wa Maria Sarungi?

Unaitakaje serikali ingilie kati kana kwamba unawafahamu watekaji?
sasa kama hawafahamu inakuwaje uzembe wa kiusalama utokee katika ardhi yao maharamia kuingia kinyemela na kufanya yao?
 
umeambiwa aliutumia sana mtindo wa tekateka, tulia na kibwagizo chako ulichokifanya korasi
Ila c ameshakufa kitambo, ila moto uko pale pale 😂 au anafanya utekaji kwa njia ya online akiwa kaburini?
 
Taarifa yake iliyonukuliwa na Vyombo vya Habari hii hapa

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, Tundu Lissu ameitaka Serikali ya Kenya kuingilia kati katika madai ya kutekwa kwa mwanaharakati Maria Sarungi.

Taarifa za kutekwa kwa Maria zimesambaa leo Jumapili Januari 12, 2025 baada ya mtandao wa kimataifa wa haki za binadamu-- Amnesty International kuripoti taarifa hiyo.

Soma Pia: Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi

“Maria alikuwa amekimbilia uhamishoni nchini Kenya tangu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo amekuwa akiendesha televisheni ya mtandaoni ya Mwanzo TV, inayotoa maudhui ya kuunga mkono demokrasia.

“Ingawa tunatumai na kusali kwa ajili ya maisha na usalama wa Maria, ni lazima tutoe wito kwa Serikali ya Kenya na watu wote wenye nia njema kutoka duniani kote kuingilia kati, kuhakikisha usalama wa Maria,”ameandika Lissu.

View attachment 3200002View attachment 3200003
Lisu sasa nenda kenya uwashinikize maana wewe unasema ni siasa za mshike mshike,,,,,, fanya tuone sasa....
 
sasa kama hawafahamu inakuwaje uzembe wa kiusalama utokee katika ardhi yao maharamia kuingia kinyemela na kufanya yao?
Sasa Lisu anaposema anaitaka Serikali ya Kenya iingilie, anamaanisha nini kaongea na nani huko Serikali ya Kenya?
 
Back
Top Bottom