PreGE2025 Tundu Lissu akamatwa na Polisi akielekea Mbinga, Ruvuma

PreGE2025 Tundu Lissu akamatwa na Polisi akielekea Mbinga, Ruvuma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Nimemuona hapa Central Dar now....na baadhi watu wa CDM...wanaingia kutoka ofisi za wakubwa hapa Central ....
 
Anaandika John Heche Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,.

Nimepewa taarifa ya kukamatwa kwa mhe Tundu Lissu Mwenyekiti wetu wa chama Taifa... mda huu huko Mbinga, tunafuatilia na tutatoa taarifa kamili ya tukio mda sio mrefu.

Lolote baya likimtokea Mwenyekiti serikali inawajibika kwa asilimia 100.
Nimemuonaa kwa karibu kabisa mita 1...ametusalimia anatabasamu yuko salama....anavyoonekana....kwa wajihi wa nje...atakuwa amesafiri usiku kucha au helikopta
 
Ccm lmesheheni wajinga, wanahubiri amani na wanachukia haki
 
dah wafuasi wamekaa wanametoa macho tu! kweli hawa wanaweza kuzuia uchaguzi?
 
TWENDE LISU TWENDE. HASHETANI TU HAO WALA RUSHWA WAKUBWA

Hapo nimeangalia nikagundua kua sisi watu sawasawa na wale nyati kule mbugani. Angalia hapo wapo WATu karibu 30k (30,000) polisi sioni wako zaidi ya 50. Sasa unashangaaje kuona simba wawili au hata mmoja anaweza kumteka nyati mmoja na kumla? Polisi hata ukiwaangalia wako na wasiwasi.

Mimi sipo hapo ningenyang’anya bunduki na mambo yangekuwa vingine

Don’t moan take action
 
Lissu amekosa mbinu za kuendesha chama anatukana ili akamatwe aseme alikuwa jela, wamwachie aje apambane jukwaani, asipate visingizio, huyu hawezi zuia uchaguzi hata wa kiranja wa bweni
 
Jeshi la Polisi limepiga mabomu na kumkamata Tundu Lissu muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake huko Mbamba Bay mkoani Ruvuma sasa hivi.


TAARIFA KUTOKA CHADEMA
BreakingNews Mwenyekiti wa Chama wa Taifa Mhe. Tundu A. Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi wilaya Mbinga. Mhe. Lissu amekamatwa wakati alipomaliza mkutano wa hadhara uliofanyika leo tarehe 09 Aprili 2025 Jimbo la Mbinga, mpaka sasa haijulikani amepelekwa kituo gani cha Polisi. Mwenyekiti amekamatwa pamoja na wanachama wengine, kwa sasa Jeshi hilo linaendelewa kutawanya wananchi kwa mabomu uwanjani hapo.

--
View attachment 3298076
VIDEO: Muda mchache kabla ya Lissu kukamatwa​

Muendelezo Wa Taarifa Iliyotolewa Na Godbless Lema Kuhusu Kukamatwa Kwa Tundu Lissu

Baada ya mkutano leo jioni saa 12:00 wilaya ya Mbinga, wakati wa kufunga mkutano OCD alimfuata Mwenyekiti Tundu Lissu Jukwani akamwambia tafadhali ukishuka hapo jukwani Ingia kwenye gari ya Polisi nakutaka Polisi kwa mahojiano.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

View attachment 3298243
Baadhi wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo wadaiwa kujeruhiwa wakati polisi wakitawanya wananchi​

Mh Lissu alimwambia nimefanya nini ? Huku akiendelea kuchangisha fedha ktk hadhara ‘ Tone Tone. baada ya kuona hiyo zogo , Kamanda Sosopi alimfuata OCD nakumwambia kama Lissu analo jambo na nyie pls mnaweza kuja pale tulipofikia mkamchukua kwa utaratibu hapa mtazua tafrani kubwa maana halaiki hapa ni kubwa,

Pia Mimi nilisisitiza Ushauri huo kwa OCD na wasaidizi wake wengine, alionekana kama anaelewa lakini ghafla mabomu ya machozi mengi yalianza kurindima.

Mh Lissu amekamatwa na sasa yuko kituo cha Polisi Mbinga.
Tanzania nchi yangu haina Usalama wa Taifa kama zamani. Kuna miaka tuliheshimika Afrika nzima kuanzia Afrika kusini, Namibia, Msumbiji, Ghana mpaka Biafra. Leo hii mpaka upinzani hausikilizwi na Serikali inatumia mabavu, hivi TISS wanamshauri nini rais ?Basi kama TISS wanaogopa kusema wamwite Kikwete amshauri Rais maana kipindi chake aliitwa ''hamnazo'' hadharani. Maana kumkamata Lissu ndio unazidi kumpa nguvu. Makaburu walin´mfunga Mandela miaka 27. Hivi wanajua kuna mitaa na majengo yana jina la Nelson Mandela Kuanzia Ulaya, Urusi, Marekani mpaka China ?

Magufuli alikuwa aliiharibu hii nchi lakini alikuwa hajui alilokuwa anafanya. Kuongoza ni kwa kutumia referal, leo hii wazanzibari ndiyo wasukuma wa Mama Samia na Kizimkazi ndiyo Chato ya Mama Samia. TISS wanatakiwa kuona mbele , na walitakuwa kuyaona haya kipindi cha Magufuli. Mimi naona TISS waangalie maslahi mapana ya nchi na sio ya chama utawala.
 
Back
Top Bottom