Uchaguzi 2020 Tundu Lissu akiwa Iringa: Upinzani ni Watu, ukitaka kuua Upinzani ua kwanza Watu

Mbona kwa lowassa ilikuwa n mara mbili ya huyu nyumbu na bado alishindwa in short hamna mtu hapo
 
Jamaa anajichosha kabla hata kampeni hazijaanza na anapoteza kamvuto kadogo ambako anadai anako.

Sasa kampeni zikianza Rasmi utakuta ashachoka na Raia washazoea blah blah zake.
 
Chadema ilishakufa, na hao tunaowaona hapo ni mizimu ya kina Alphonce Mawazo na Mzee Ndessa. Huyo jamaa anayepiga picha hapo ni Ben Saanane
 
Alete sera Sasa apigiwe kura
 
uliambiwa kila kijiji kitapewa 50milioni keshi money Halmashauri inaingiaje hap....subirini LISSU AWAPASUWE KWENYE KAMPENI

Atapasuliwa yeye kwa sababu ya kiburi chake cha kudharau mamlaka halali na mbaya zaidi kumdharau Mungu juu ya hali ya corona Tanzania.
 
Kwani wakati wa Lowassa cdm ilikuwa imekufa? Ni kweli hawatampigia kura, lakini wamekubali kwenda kumsikiliza, hilo pekee linatosha. Na tungekuwa na tume huru basi hapo ukweli wote ungekuwa hadharani.
Kwa kuongezea tu kwenye hoja yako mujarabu, hiyo ELIMU YA URAIA (iliyositishwa kwa takribani miaka mitano sasa na ilikwishaondolewa katika mitaala ya shule miaka kadhaa) anayoitoa ni mchango mkubwa kuelekea ukombozi wa taifa hili kutoka mikononi mwa mkoloni mweusi - kama sio mwaka huu, basi itakuwa 2025 au 2030. Ukombozi haudondoki kama mvua, hupiganiwa tena kwa muda mrefu. Pamoja na kumwaga ELIMU YA URAIA, pia huu ni ujumbe tosha kwa mhusika mkuu kuwa ile projekti ya kuua upinzani ifikapo 2020 imefeli vibaya sana. Arejee kwenye drawing board, achemshe ubongo upya.
 
Hapo ndio anaomba wadhamini? Aandike anayoyaongea maana kampeni zikianza asijerudi haya haya tunataka mapya
 
Kwahiyo kwa akili yako unadhani hao walikusanyika apo watampigia kura? Mbona hata theluthi ya lowasa hajawahi fikia na hatofikia kamwe. Watanzania sio wajinga.
Unadhani lowasa hakupigiwa kura na watanzania?
Mataga mna shida Sana nyie
 
Jamaa anajichosha kabla hata kampeni hazijaanza na anapoteza kamvuto kadogo ambako anadai anako.

Sasa kampeni zikianza Rasmi utakuta ashachoka na Raia washazoea blah blah zake.
Sasa hiyo si ndio neema kwa magufuli kushinda kwa kihindo. Mimi nilifikiri MATAGA mgeiona hii ni habari kuw nzuri ili ajichoshe!!
 
Sasa hiyo si ndio neema kwa magufuli kushinda kwa kihindo. Mimi nilifikiri MATAGA mgeiona hii ni habari kuw nzuri ili ajichoshe!!
Of course ndio maana unaona hakuna anayehangaika naye,

Wacha apige kelee wee.

Muda ukifika atausikia mziki wake.
 
Lissu ni mwanaume wa shoka, kapigwa risasi 16 na bado karudi nchini na anaunguruma kama Simba dume wa nyikani, moto ule ule alipoishia sept 11 2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…