Makamu Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema nchini Tanzania, Tundu Lissu leo Oktoba 8 amekutana na wakili wake, ambaye anaitwa Robert Amsterdam.
Hivi karibuni Tundu Lissu alisema amemuelekeza mwanasheria wake Bob Amsterdam kuanza taratibu za kuishtaki kampuni ya Millicom ambayo ilikuwa kampuni mama ya simu za mkononi ya Tigo kwa pamoja na serikali ya Tanzania kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la kutoa uhai wake.
Lissu aliyasema hayo baada ya mahakama moja nchini Uingereza kuelezwa kuwa kampuni ya mawasiliano ya Tigo (ambayo ilikuwa ikimilikiwa kwa wakati huo na Millicom) ilitoa taarifa za mawasiliano na nyendo za mwanasiasa huyo kwa saa 24 siku chache kabla ya tukio la kushambuliwa kwake.
Septemba 7, 2017 Lissu alishambuliwa kwa risasi zipatazo 16 aliporeja kutoka kwenye kikao cha Bunge, akiwa katika uwanja wa makazi yake na viongozi wengine eneo la Area D, jijini Dodoma, na baadaye kufanyiwa upasuaji mara 25 nchini Kenya na Ubelgiji.
Wakati huo Tundu Lissu alikuwa mbunge wa Singida Mashariki mkoni Singida, katikati mwa Tanzania kupitia Chadema.