PreGE2025 Tundu Lissu alalamika kunyimwa haki ya kuabudu gerezani

PreGE2025 Tundu Lissu alalamika kunyimwa haki ya kuabudu gerezani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu amelalamika kunyimwa haki ya kuabudu kwa takribani siku 68 tangu alipokamatwa na kupelekwa gerezani.

Lissu ametoa taarifa hiyo siku ya Jumatatu Juni 16, 2025 alipopewa nafasi ya kuzungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Franco Kiswaga wakati kesi yake ya uhaini ikiendelea.

Lissu amesema, “mawakili wangu hawa wamekuja kunitembelea gerezani na muda wote ambao wamekuja katika siku hizi 68 hawajaruhusiwa kuniona na kuwasiliana na mimi, hawajaruhusiwa kuonana na kuzungumza na mimi kwa faragha. Kitu ambacho kimetokea Mheshimiwa ukiingia kwenye Gereza Kuu la Ukonga ukiingia reception kulia kwako hivi kuna kachumba, hako kachumba kamegawanywa mara mbili kamegawanywa na ukuta wa kioo.”

"Nina haki ya kuabudu Mheshimiwa kila Jumapili Wakristo wanafanywa ibada katika Gerezala Ukonga na mimi ni Mkristo, na kwenye sikukuu za Kikristo wanafanyiwa ibada gerezani"

"Mimi nilipelekwa Gereza la Ukonga siku ya Ijumaa Kuu, na nilipopokelewa 'immediately' nikamuomba Mkuu wa Magereza nikafanye ibada akakataa na Jumapili ya Pasaka nikamuomba Mkuu wa Gereza nikasali akakataa, Jumatatu ya Pasaka akakataa, na nimekuwa nikiomba anakataa kila jumapili ikiwamo ya jana".

Hata hivyo upande wa Jamhuri umeeleza kuwa haujapewa nafasi ya kusikilizwa kutokana na madai hayo lakini Hakimu Kiswaga amesema kuwa madai hayo yamebainishwa na mshtakiwa kama taarifa hivyo itafanyiwa kazi kiutawala.


lissu.png


Chanzo: JAMBO TV
 
Mbona huku uraiani hatujawahi kumuona katika kanisa lolote?

Anyway, deconstruction imefanikiwa, jeuri inaisha, in two months atakuwa kama uji wa mchele

WEwe ni mwendawazimu hayawani. Hakuna haja hata ya kukuliza maswali yanayohitaji akili kuyajibu.
 
Mbona huku uraiani hatujawahi kumuona katika kanisa lolote?

Anyway, deconstruction imefanikiwa, jeuri inaisha, in two months atakuwa kama uji wa mchele
MPUMBAFU WW NA ZERO BRAIN
 
Ukiwa uraiani hauabudu ukiwekwa nyuma ya bar's ndo unakumbuka ibada, wakazie hapohapo hamna kufanya ibada yoyote.
 
Mbona huku uraiani hatujawahi kumuona katika kanisa lolote?

Anyway, deconstruction imefanikiwa, jeuri inaisha, in two months atakuwa kama uji wa mchele
Wewe dada mbona unanongwa hivyo ? Kwa hiyo ulikuwa unalala nae chumba kimoja maana mpaka uraiani juu ya kutokwenda kwenye ibada ya jumapili ulikuwa unamuona, basi utakuwa una raha sana kwa kumsaidia Mama wa Belgium japo kwa sasa umeikosa kwa yeye kuwa Lupango.

ONGERA Mwayego
 
Back
Top Bottom