Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Sijakuelewa! Uchaguzi upi? Kwani mwaka huu Tanzania kulifanyika uchaguzi!

Sent from my itel A11 using JamiiForums mobile app
 
Atarudi 2025 akiwaaminisha tena kuna usalama

Akishindwa atarudi ulaya
Jamaa wakati anakuja aliwaambia haogopi lolote lakini baada ya kupata ''political sucker punch'', kwa sasa anadai hakuna usalama nchini!
 
Kabla ya vyama vingi tulikuwa na chama kimoja kwa miaka 30, Tulipata maendeleo gani?

Uliuwa na umri gani wakati Mwalimu anang'atuka mwaka 1985, unaijua hali tuliyojuwa nayo kama nchi wakati huo?

Mabeberu wakitaka kuing'oa hiyo CCM yako haiwezi kulast hata wiki moja, wao ndo waliipa TANU serikali na wao wakitaka wanaweza kuijengea mazingira CCM ikang'oka!

Ndiyo maana Jiwe anatuvimbia sisi wananchi lakini Mzungu akikohoa tu chapcha tu anarufi msitarini. Wewe unafikiri bila mzungu kuingilia kati huyo Lissu angeachiwa aondoke?
 
Hivi kweli unaweza kutumia mda wako kuandika ujinga kama huu, wakati dunia nzima inajua jiwe alichokifanya
 
Mmeshinda uchaguzi, kaeni kimya
Kumchagulia mtu mzima nini cha kufanya ni sehemu ya udikteta!

Wewe kama unataka kukaa kimya basi kaa kimya. Waache wengine wafanye wanavyotaka kama hawavunji sheria za Jamiiforums!
 
Mkaambiwa andamaneni kumuondoa huyo wa chato mkajificha uvunguni mwa vitanda

Kuandamana ni njia moja, zipo nyingi sana, ni suala la kuamua itumike ipi na mazingira gani.
 
Haya mambo kama yana ukweli yasiishie kwenye mitandao, mpaka sasa ni kupost Twitter na JF inatakiwa hatua stahiki zichukuliwe tuambiwe ilitokea nini hiyo tar 27/28 mpaka watu wakapigwa risasi.

Ipo tume ya haki za binadamu,mahakama zipo n.k

Hakuna mahakama Tanzania za kuzuia mipango ya dictator.
 
Kuna mwanajamiiforums pale juu amesema, alipokuwa anakuja alituambia haogopi chochote lakini baada ya kupata kipigo cha mbwa koko kwenye sanaduku la kura, amebadilika na kudai maisha yake hayako salama inabidi aondoke haraka!
 
Mmebakiza kilio hicho? Kama ni dikteta mlipata wapi huu uhuru wa kufanya kampeni kisha wananchi wakawakataa?

Kura za kwenye mabeg ndio wananchi au unadhani hatukuona kilichotokea? Kwani kupiga kampeni kunaondoa ukweli vwa udictator?
 
Hawa jamaa niwa kuwapa huruma!

Wamesahau walikuwa wanapiga kelele na kuimba NI YEYE!

Kipi cha ajabu, hata Yesu aliitwa mkombozi lakini aliuwawa na wayahudi. Halafu watu wanashangilia kuwa kwa kifo chake ndio walikombolewa. Toka nje ya box dogo.
 
Kura za kwenye mabeg ndio wananchi au unadhani hatukuona kilichotokea? Kwani kupiga kampeni kunaondoa ukweli vwa udictator?
Mnatengeneza video za uongo ili kudanganya watu kulikuwa na wizi wa kura!
 
Nilisha wahi kuandika mahali ikifika mwezi wa kumi ndio mwisho wa chadema na imetokea.
Jamaa alipotoka Belgium alikuja na mbwembwe nyingi sana nataka maandamano ya kunipokea, nataka nikija Dar isimame na nyingine nyingi.
Ila jana alipokuwa anaondoka hakuwa na tofauti na paka alienyeshewa.
1. Ameagwa na watu wasio zidi kumi
2. Amesindikizwa na Mabeberu.
3. Hata kuwaaga waliompokea kashindwa

Sasa sijuii akirudi tena atakuwa mgeni wa nani. Kwanza amekumbuka kulipa pango la nyumba aliyokuwa anakaa??
 
Itoshe kusema uchaguzi umepita tufanye ishu zingine

NB: Hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu ktk siasa.
 
Kuna mwanajamiiforums pale juu amesema, alipokuwa anakuja alituambia haogopi chochote lakini baada ya kupata kipigo cha mbwa koko kwenye sanaduku la kura, amebadilika na kudai maisha yake hayako salama inabidi aondoke haraka!

Hujisikia Magu anajisifia yeye ni jiwe na wala hajaribiwi, lakini kila anapoenda walinzi kibao. Kama yeye ni mwamba aje kariakoo bila walinzi kufanya shopping.

Akina Museveni, Kabila baba wote hao hawakuwa waoga, mbona walikimbia nchi zao na kurejea tena kuzikomboa? Au hujui maana ya kutokuwa muoga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…