Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Nimeisikiliza audio amejibu vyema sana kuhusu Covid19
 
Ushamba mwingine. Tangu Lisu aje Tanzania, umeshaona TBC waki-cover shughuli zake? Au mnataka media za Kenya nazo ziwe kama TBC ili msherehekee? Yaani binadamu wengine mnasikitisha sana. Hapa Tanzania mnapiga vyomboo vya habari faini kumzumgumzia Lissu.

Sasa vyombo huru Kenya vinamhoji, pia mnavimba. Kweli hasidi ni hasidi. Ucheke, unune haina tofauti kwake. mmefanya siasa wenyewe kwa mika 5 wakati wengine wakikamatwa na kupigwa mabomu kwa kufanya vikao vya ndani. Bado tu hamjiamini na roho zenu zimepinda kama korosho.
 
Kaidanganya mahakama kuwa yupo karantini kumbe anazurura kila mahalo atakap. Siku akikum ana na rungu la mahakama aslete deama.
Kama covid ipo mbona hachukui hatua kujizuia asiambukizwe? To
 
Wapambe siyo wagombea; iwapo wapambe wa CCM ndio walikuwa wanamtukana wao siyo wagombea na wala tume haishughuliki nao. Tatizo ni pale mgombea mwenyewe ndiye anayerusha matusi.
Ndiyo sheria inasema hivyo!!? Sasa zile push up zilikuwa na malengo gani... Si ndiyo matusi ya rejareja hayo.
 
Ndiyo sheria inasema hivyo!!? Sasa zile push up zilikuwa na malengo gani... Si ndiyo matusi ya rejareja hayo.
Push up siyo tusi ingawa inaweza kuwa ni kejeli lakini siyo tusi linaloweza kulalamikiwa mbele ya sheria. Matusi yantolewa kwa maneno ambayo yakihusisha utambulishi wa anayetukanwa na yanaweza kuthibitishwa mbele ya sheria.
 
Push up siyo tusi ingawa inaweza kuwa ni kejeli lakini siyo tusi linaloweza kulalamikiwa mbele ya sheria. Matusi yantolewa kwa maneno ambayo yakihusisha utambulishi wa anayetukanwa na yanaweza kuthibitishwa mbele ya sheria.
Embu mkuu niambie kuna tusi gani katukana kweny hii audio???
 
Mwaka huu mtavimba hata mtapasuka.

Mwambieni Meko aache ukandamizaji kwa vyombo vya habari vya Bongo la sivyo Lissu atatumia hata CNN kufikisha ujumbe kwa watanzania.

Asubuhi tarehe 28.10.2020 kabla ya jogoo wa kwanza Lissu anaukwaa Urais wa Tanzania
 
Kaidanganya mahakama kuwa yupo karantini kumbe anazurura kila mahalo atakap. Siku akikum ana na rungu la mahakama aslete deama.
Kama covid ipo mbona hachukui hatua kujizuia asiambukizwe? To
Nje ya mada
 
Embu mkuu niambie kuna tusi gani katukana kweny hii audio???
Audio sijaisikiliza; nitafanya hivyo baadaye. Hayo uliyokwoti ni mtililiko wa maswali na majibu yaliyotokana na tahadhari niliyotoa jana kabla hajafanya inteview; nilisema ajizuia asitumie lugha yenye kuwa kutafsiriwa kuwa ni mtusi kwa Magufuli kwani itakuwa ni kinyume cha kanuni za uchaguzi. Kama ali-heed na kujizuia kutoa matusi au kuzusha mambo yasiyo kweli kwa nia ya ku-embarass mgombea mwenzake, hiyo ni sawa.
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Sasa ndugu yangu ili umuelewe ulitaka akaongelee wapi? sisi watanzania wagumu sana kuelewa jaman, unaambiwa media zote za kibongo zimegoma kumpatia coverage sasa ww ulitaka akaongelee kwenye media gan? wakati mwingine tuweke unazi pemben jaman maendeleo hayana vyama
 
Akishindwa kwenye uchaguzi...(100% atashindwa mapemaa) namshauri pia maandamano ya kupinga "wizi"wa kula yaanzie Kenya maana wao wana uzoefu wa kuandamana!
Mchekeshaji mmoja wa Kenya aliwahi kusema kuwa wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi kuna kabila moja liling'oa reli ili CNN na Aljazeera wapate "picha" nzuri huku kabila jingine likiokota vyuma vilivyong'olewa na kwenda kuuza kama chuma chakavu na kupiga hela saafi!
Lissu anatumia "akili" za kabila la kwanza!
 
Ukweli ni kwamba wananchi wengi wamemuelewa sana rais jinsi amedeal na issue ya corona, sasa Lissu akipuyanga kwenye hilo atapoteza mvuto.
Apuyange mara ngapi, ameishaharibu upande ule huku hawa wenzake wakimuacha tu!
 
Kuzuia vyombovya habari vya Tanzania kumhoji Lissu hakutawasaidu chochote sanasana Ni kumpiga teke chura ,kumuongezea mwendo ,awamu hii hebu punguzeni ushamba ,miaka mitano bado washamba tu na malimbukeni.
 

Lisu hajielewi na anafikiri hao ndio voters. Wewe ulikuwa una campaign watu wanyimwe misaada leo umewapenda uwatumikie?

Hiyo reference ya Mwl Nyerere alishasema hapo nyuma mwalimu aliishi kiujanja ujanja which means was not credible. Leo tena kawa reference.
Yet huwezi chukua dora kwa kuvitukana vyombo vinavyotakiwa vikulinde.

Hao Wazungu anaofikiria yeye na Membe eti watatusaidia kukuletea maendeleoni kutokujielewa kabisa.
Hao Kenyas anafikiria wanampenda sana nooo ni interest zao tuu.

Good luck waiting to see what next after seeing Magu's land mark winning.
 

Sisi Wakenya hatuna interest yoyote kwa Lissu, na asilimia kubwa ya Wakenya hata hawana habari ya nani huyo anaitwa Lissu, ni ile kwamba
- Sisi ndio taifa pekee kando na Tanzania ambapo tunatumia Kiswahili kama lugha ya taifa
- Maana kwamba atakayoyasema huku kwetu yataeleweka na Watanzania wenzake
- Mumemfungia media zote huko hana airtime wala uwezo wa kuhojiwa popote
- Media za Kenya huwa na uhuru wa kuhoji na kuuliza maswali ya kila aina, hivyo kwa saa nzima lazima alifunguka yote
- Media za Kenya hususan hiyo Citizen airwaves zake hufika hata Tanzania, hivyo anatumia hii fursa kujaribu kuwafikia mashabiki wake
- Kwetu hapa ni vigumu kuingilia media, leo hii hata Magufuli akimpigia rais Uhuru simu akimuomba azuie, wala hamna kitakachofanyika maana rais Uhuru hana uwezo huo, tunatumia katiba mpya na bora kuzidi zote ukanda huu, rais hawezi kuthubutu kufungia media yoyote ile kisa kiongozi kahojiwa hapo.
- Hapa labda niwashauri CCM mtumie mbinu nyingine, kama vile kupambana naye hoja kwa hoja, maana kufungia media zenu huko hakutasaidia kwa vile atatumia za Kenya, na hatuna namna ya kuwasaidia, atasikika Tanzania yote, labda sijui mzuie frequency zisifike huko.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sasa mnashiriki uchaguzi kwa nini kama mnajua mtaibiwa kura.
Kushiriki ni haki hata watoto tunazaa japo tunajua hawataishi milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…