Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Lissu na Membe wao wanapiga kampeini za hasira binafsi dhidi ya Magufuli; hilo linajulikana kabisa; siyo kuwa wanashindana na sera za CCM. Sasa awe makini atakapokuwa anatumia vyombo vya nje kumtukana Magufuli kama alivyokuwa anafanya alipokuwa Ulaya. Watangazaji wa Kenya wanaweza kabisa kumwuliza maswali yanayoelekea huko, na akishindwa kuwa makini atajikuta anatoa matusi tena, jambo litakalokuwa inakiuka kanuni za uchaguzi.
Sioni shida yeyote ile kupiga kampeni dhidi ya mgombea wa chama unachoshindana nacho katika Uchaguzi. In fact, mgombea wanayeshindana naye ndio huyo huyo aliyeko madarakani na ndio huyo anayetafuta kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine.

Unawezaje kushindana na sera za chama cha mgombea unayeshindana naye bila kumgusa mgombea huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho?

Ni nchi gani ya kidemokrasia ambayo mgombea Urais aliyeko madarakani huwa hashambuliwi kwa maneno na vyama pinzani wakati wa kampeni?

Hata katika nchi zilizoendelea na za kidemokrasia kama vile Marekani ambayo pia inakaribia kwenye Uchaguzi, mgombea wa chama kilichopo madarakani [Donald Trump] anashambuliwa vivyo hivyo kwa maneno na wapinzani wake [Democrats]. Hivyo ndivyo siasa ilivyo hasa katika kipindi cha karibu na Uchaguzi.
 
Sioni shida yeyote ile kupiga kampeni dhidi ya mgombea wa chama unachoshindana nacho katika Uchaguzi. In fact, mgombea wanayeshindana naye ndio huyo huyo aliyeko madarakani na ndio huyo anayetafuta kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine.

Unawezaje kushindana na sera za chama cha mgombea unayeshindana naye bila kumgusa mgombea huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho?

Ni nchi gani ya kidemokrasia ambayo mgombea Urais aliyeko madarakani huwa hashambuliwi kwa maneno na vyama pinzani wakati wa kampeni?

Hata katika nchi zilizoendelea na za kidemokrasia kama vile Marekani ambayo pia inakaribia kwenye Uchaguzi, mgombea wa chama kilichopo madarakani [Donald Trump] anashambuliwa vivyo hivyo kwa maneno na wapinzani wake [Democrats]. Hiyo ndio siasa ilivyo hasa katika kipindi cha karibu na Uchaguzi.
Ukisoma kanuni za uchaguzi, kuna sehemu inayozuia wagombea kushambuliana kwa matusi ya binafsi. Kama unakumbuka, ubunge wa Wassira ulienguliwa baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 kwa sababu Wassira alikuwa anaendesha kampeni za kumtukana Waryoba binafsi.
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!

Kama ananyimwa media coverage hapa nyumbani ni kwanini asitumie za nje ya nchi? Mnataka aendelee kubembeleza za hapa nyumbani ili muishie kutesa familia za hao wenye hizo media? Lisu tumia hata BBC, CNN, DW, AFP nk tutakusikiliza, ili mradi tu uongee mambo ya msingi ya nchi yetu.
 
Ukisoma kanuni za uchaguzi, kuna sehemu inayozuia wagombea kushambuliana kwa matusi ya binafsi. Kama unakumbuka, ubunge wa Wassira ulienguliwa baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 kwa sababu Wassira alikuwa anaendesha kampeni za kumtukana Waryoba binafsi.
Unaposema "matusi ya binafsi" inakupasa uiweke hoja hiyo wazi zaidi hasa kuhusiana na hao wagombea wawili uliowataja hapo awali. Be explicit!

Maana neno "matusi" linaweza kutumika vibaya kuendana na uelewa wa watu tofauti tofauti. Kwa mwingine, mgombea anapozikosoa sera za mgombea aliyeko madarakani hudhani kuwa ni matusi.

Kuna shida kubwa nimeiona ya matumizi ya neno "matusi" kwamba limerahisishwa sana kimatumizi. Imefikia hatua hata mtu anapomkosoa fulani kwa hoja yenye mashiko kabisa, baadhi ya watu huishia husema anatoa matusi pengine kwa sababu tu ya kukerwa na hoja hiyo.

Ni vyema ukaiweka hoja yako wazi na kwa ufafanuzi wa kina kuhusu "matusi" na kuhusiana na hao wagombea wawili uliowataja hapo awali.
 
Lissu na Membe wao wanapiga kampeini za hasira binafsi dhidi ya Magufuli; hilo linajulikana kabisa; siyo kuwa wanashindana na sera za CCM. Sasa awe makini atakapokuwa anatumia vyombo vya nje kumtukana Magufuli kama alivyokuwa anafanya alipokuwa Ulaya. Watangazaji wa Kenya wanaweza kabisa kumwuliza maswali yanayoelekea huko, na akishindwa kuwa makini atajikuta anatoa matusi tena, jambo litakalokuwa inakiuka kanuni za uchaguzi.

Kichekesho ni pale mwenye tafsiri ya matusi ni Magufuli na CCM yake.
 
Ukisoma kanuni za uchaguzi, kuna sehemu inayozuia wagombea kushambuliana kwa matusi ya binafsi. Kama unakumbuka, ubunge wa Wassira ulienguliwa baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 kwa sababu Wassira alikuwa anaendesha kampeni za kumtukana Waryoba binafsi.

Ni nani ana tafsiri ya hayo matusi? Maana utakuta wale wafaidika wa madaraka ya rais, ndio watoa tafsiri ya matusi, na kamwe hawawezi kumfanya lolote rais akitukana. Kichekesho hiki kiko Tanzania tu.
 
Mimi nimetahadharisha tu; kanuni zipo na zinasimamiwa na tume pamoja na mahakama. Kama hawezi kukubaliiana na tafsiri inayotolewa na tume, basi asingechukua form kutoka tume hiyo hiyo asiyoamini.
 
Lissu na Membe wao wanapiga kampeini za hasira binafsi dhidi ya Magufuli; hilo linajulikana kabisa; siyo kuwa wanashindana na sera za CCM. Sasa awe makini atakapokuwa anatumia vyombo vya nje kumtukana Magufuli kama alivyokuwa anafanya alipokuwa Ulaya. Watangazaji wa Kenya wanaweza kabisa kumwuliza maswali yanayoelekea huko, na akishindwa kuwa makini atajikuta anatoa matusi tena, jambo litakalokuwa inakiuka kanuni za uchaguzi.
Bila shaka hujui kitu kiitwacho tusi.
 
Huyu anataka kuongoza hii nchi.. huku akikimbilia kutuonyesha hataki kutumia.. vyombo vya habari vya nchini.. huyu angeuza nchi yetu kama angebahatika kuchaguliwa kuwa Rais..

Anaonyesha yupo radhi.. media za nchi za nje ziendelee.. kuliko za nchini.. mpenda mabeberu.. hajali uchumi wa nchi yetu.. wala kusaidia kutengeneza ajira.. kwa sababu kawaona bora Kenyans waendelee.. poleni washabiki wake wafwu..

Magufuli [emoji817] Mzalendo
Kama kuchukua form tu vyombo vyote vya habari viliacha kurusha na vingine vilivyoanza kurusha vikasitishwa ...ndo wampe masaa ya kuhojiwa?
Thubutuuuuuu!!!
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Sasa afanyaje kama Kenya ndo wamemwalika kumbuka hakuna vyombo vya Tz wanauthubutu wa kufanya hivyo kwa sasa
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Sasa Kama Ni marufuku kupata airtime ktk media za hapa afanyeje? Afe kibudu? Bora afe kwa kutapatapa! When one door is closed The other is open!
 
Back
Top Bottom