Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania

Ningekuwa mshauri wa Tundu Lissu ningemwambia achana na nia ya kugombea uraisi kwa mustakabala wa amani ya taifa lako,hakuna namna yoyote inayoweza kumpa ushindi Bw. Lissu zaidi ya kuleta taharuki katika jamii na usalama mdogo wa maisha yake.
Ukinuliza kwanini nasema hivyo ni kwa sababu kuna hisia kwa baadhi ya watu na yeye binafsi kwamba serikali ilihusika kwa yeye kupigwa risasi,kwa mtazamo huo ni wazi kwamba kama binadamu atakuwa na kinyongo na kulipiza kisasi kama mwanadamu.
Mwisho namshauri Bw.Lissu atulie huko aliko,asitegemee huruma (simpathy) toka kwa jamii ili imchague,yeye amshukuru Mungu kwa kumponya na tukio baya ambalo ni kubwa kuliko huo uraisi anaoutafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mzee mmoja kule lumumba akisikia jina la Lisu Vima yanagonga pichu
 
Acheni kumsumbua huyo Lissu hatafanya kampeni yoyote hapa Nchini,Kwanza ana kesi ambayo inamsubiria,Pili afya yake sio imara kwa Sasa,Tatu usalama wake Ni mdogo ndani na nje ya Chama Chake,Nne sio Presidential material Ni Mtu anayeropoka na kupayuka ovyoo,Pia anaunga mkono Ndoa za Jinsia moja na mengine mengi
 
Kajamaa kajanja sana,kameona kuwa ubunge kamekosa sasa kanaenda kujichomeka nafasi ya Urais ili kije kugawana posho na wabunge wa cdm watakaochaguliwa...aisee kina sugu na prof J kazi wanayo wamehusle kwenye muziki lakini kule siasani wameeenda kukutana na maharamia ya Siasa.
 
Lissu aache tamaa ya madaraka, ataongozaje nchi na huo ulemavu?

Wachaga wanamtumia kama walivyowatumia kina Silinde, Lijualikali, Prof Safari, Lwakatare.
Lissu anafaa sana wakati huu tumechoka.
 
Umenifanya nicheke mkuu, Lisu ndiyo habari yenyewe, mimi na familia yangu pamoja na wilaya yote kama siyo mkoa ama nchi kura ni kwa Lisu, nyie kalaleni juu ya mawe na jiwe
 
Lisu ni unfit..... hawezi.... a gwalide

Mbali na Maudhi ambayo Lissu aliyotufanyia sisi Watanzania (ya kutuombea mabaya kama tususiwe kiuchumi, kisiasa, kijamii kidiplomasia nakadhalika)! bado hiyo haikufanyi kama wewe mwanaJF umudhiaki kiasi hiki kwa hali aliyonayo hata kama hafai hata thumuni kugombea nafasi yoyote ya uwakilishi nchini.

Sijafurahishwa na post yako hii Mkuu.
 
Hoja yako haina mashiko
 
Tundu ni mwanasiasa na ataendeleza siasa za maandiko na mitandaoni akiwa huko ughaibuni.Ukweli ni kwamba hana mpango wa kurudi Tanzania kwenye uchaguzi.
 
Huyu hawezi kurudi nchini hata yeye anafaham hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…