Pre GE2025 Tundu Lissu amteua Lema kuwa wakala wake uchaguzi CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu amteua Lema kuwa wakala wake uchaguzi CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Safi, hii imekaa kimkakati zaidi.
Lissu anacheza na akili za wajinga.
FAM na TAL wanajua wanachokifanya.
Hii itaepusha malalamiko, endapo FAM akishinda.
Na kuepusha mpasuko
 
Kwa jicho pevuu huu uchaguzi una ngumi hapo baadae kama sahivi tu kwenye kuhakiki majina watu wanazozana hivi asbuhi wapiga kura walitangazwa kuwa906 kufikia sahivi idadi imepiga u turn ni1007 Mpaka matokeo kutangazwa jumla ya kura ni2000
Yes asubuhi walikua 900 total was 1200
 
Mgombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa na makamu mwenyekiti anayemaliza muda wake, Tundu Lissu, amemteua Godbless Lema kuwa wakala wake katika uchaguzi unaofanyika leo.
View attachment 3209003
Kuteuliwa kwa Lema, ambaye si mjumbe wa mkutano mkuu kwa sasa, kumetangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, leo Jumanne, Januari 21, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

"Nimepokea barua toka kwa Tundu Lissu akimchagua Godbless Lema kuwa wakala wake kwenye uchaguzi Mkuu, Miongozo ya katiba inamruhusu" - John Mnyika

View attachment 3209007
Akitoa tangazo hilo muda mchache kabla ya uchaguzi huo kuanza, Mnyika amesema suala hilo halivunji kanuni za uchaguzi.

Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?
Safi sana. Lissu, heche, Lema

Hii ni Holy Trinity
 
Katika hali isiyo kua ya kawaida,
Kibaraka amemteua Lema kua shuhuda mkuu wa kushindwa kwa Tundu Lisu kwenye uchaguzi wa chadema ngazi ya Taifa baadae leo, katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es salaam.

Wajumbe wa kambi ya Lisu sasa wako huru kurejea kambi ya Mbowe ambayo wengi wao walikua wanatamani kua huko, lakini Lema alikua akiwazuia na kuwabana kupata nafasi hata ya kusalimiana na wajumbe wengine tu.

Ushindi wa Mbowe ni wa wazi zaidi na rahisi sana baada ya Lema kuwadhibiti wajumbe zaidi ya mia2 kwa siku2 kwa ubabe tu, lakini sasa wako huru kuungana na wajumbe wengine na kumchagua Freeman Aikaeli Mbowe kua mwenyekiti wa chadema taifa.

Wamebana wameaachia, tatu bila tatu bila 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom