Tundu Lissu ana cha kujifunza hapa, Siasa siyo Uadui

Ndugu zangu watanzania,

Tundu Lissu anayo mengi sana ya kujifunza kutoka Katika picha hii inayomuonesha Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Hii picha ilichukuliwa na kupigwa hapo jana walipokutana viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa katika mashauriano ya Masuala mbalimbali chini ya kituo cha Demokrasia Tanzania. Picha hii na namna viongozi wetu hawa wa vyama vyetu wanavyotabasamu na kufurahi inaonyesha siasa siyo uadui.

Lakini pia inaonyesha namna viongozi hawa walivyoelewa vyema na kuzifanyia kazi 4R Za Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ambaye aliziasisi na kuzileta katika lengo la kulileta pamoja Taifa na kujenga umoja wa kitaifa, ndio sababu ya kuona leo watu wakiwa huru kuzungumza yaliyo katika vifua vyao kwa uhuru bila hofu.

Pia soma:
Lakini ndio sababu ya kuona viongozi wa vyama vya siasa wakikutana kwa pamoja kama hivi na kufanya mashauriano kwa njia ya amani kabisa, pamoja na vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na ile ya ndani bila shida wala vikwazo vya aina yoyote ile baada ya kuwa taratibu zote zimefuatwa na kuzingatiwa.

Sasa angekuwa ndio Lissu yupo kwenye nafasi ya Mbowe yaani ya uwenyekiti ungeona namna anavyotoa matamko makali makali na ya hovyo hovyo yenye kujenga chuki,uhasama,uadui na kuchochea ubaguzi kwa misingi tofauti tofauti kwa maslahi yake binafsi.maana yeye ni mtu ambaye anapenda mavurugu vurugu na uhasama wa kisiasa.

Ndio maana hutoa lugha zisizo nzuri akiwa mwenye majukwaa ya siasa.ndio sababu hupenda kuita haya ni Ma CCM na yale ni Ma PoliCCM. Yeye huona ambao hawapo kwenye chama chake au hawakubaliani naye kuwa wote hawana akili na hawajitambui na ni mambumbu tu.

anasahau kuwa katika siasa hakunaga adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu na siasa siyo vita wala uadui.anasahau pia kuwa ili upate ushindi katika ngazi ya aina yoyote ile basi ni lazima ufanye kazi ya kuyashawishi makundi mbalimbali kukuunga mkono na kuwa upande wako badala ya kuyachukia na kuyatukana kwa matusi na lugha za udhalilishaji.

Ndio sababu Lissu anachukiwa na watu wengi sana na watumishi na wafanyakazi wengi sana katika vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na maneno yake ya kuwadhalilisha na kuwashushia heshima. ndio maana hakuna anayeweza kumuunga mkono hata kwa kificho tu, maana kila mtu anaona ni mtu mropokaji, mkurupukaji, Mwenye kujaa mihemuko, jazba, hasira na hivyo kushindwa kutumia Busara na hekima katika kuzungumza na kushawishi watu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mwaka unakaribia Keisha,Leo ndio nimeiona umenena points!Hayo ndio mageuzi ya fkra.
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu
CCM inapita na kushinda Uchaguzi kwa nguvu ya hoja na ushawishi wa kisera .tofauti na vyama kama CHADEMA havina uwezo hata wa kuandaa ilani yake.
 
Ndugu zangu watanzania,

Tundu Lissu anayo mengi sana ya kujifunza kutoka Katika picha hii inayomuonesha Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Hii picha ilichukuliwa na kupigwa hapo jana walipokutana viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa katika mashauriano ya Masuala mbalimbali chini ya kituo cha Demokrasia Tanzania. Picha hii na namna viongozi wetu hawa wa vyama vyetu wanavyotabasamu na kufurahi inaonyesha siasa siyo uadui.

Lakini pia inaonyesha namna viongozi hawa walivyoelewa vyema na kuzifanyia kazi 4R Za Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ambaye aliziasisi na kuzileta katika lengo la kulileta pamoja Taifa na kujenga umoja wa kitaifa, ndio sababu ya kuona leo watu wakiwa huru kuzungumza yaliyo katika vifua vyao kwa uhuru bila hofu.

Pia soma:
Lakini ndio sababu ya kuona viongozi wa vyama vya siasa wakikutana kwa pamoja kama hivi na kufanya mashauriano kwa njia ya amani kabisa, pamoja na vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na ile ya ndani bila shida wala vikwazo vya aina yoyote ile baada ya kuwa taratibu zote zimefuatwa na kuzingatiwa.

Sasa angekuwa ndio Lissu yupo kwenye nafasi ya Mbowe yaani ya uwenyekiti ungeona namna anavyotoa matamko makali makali na ya hovyo hovyo yenye kujenga chuki,uhasama,uadui na kuchochea ubaguzi kwa misingi tofauti tofauti kwa maslahi yake binafsi.maana yeye ni mtu ambaye anapenda mavurugu vurugu na uhasama wa kisiasa.

Ndio maana hutoa lugha zisizo nzuri akiwa mwenye majukwaa ya siasa.ndio sababu hupenda kuita haya ni Ma CCM na yale ni Ma PoliCCM. Yeye huona ambao hawapo kwenye chama chake au hawakubaliani naye kuwa wote hawana akili na hawajitambui na ni mambumbu tu.

anasahau kuwa katika siasa hakunaga adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu na siasa siyo vita wala uadui.anasahau pia kuwa ili upate ushindi katika ngazi ya aina yoyote ile basi ni lazima ufanye kazi ya kuyashawishi makundi mbalimbali kukuunga mkono na kuwa upande wako badala ya kuyachukia na kuyatukana kwa matusi na lugha za udhalilishaji.

Ndio sababu Lissu anachukiwa na watu wengi sana na watumishi na wafanyakazi wengi sana katika vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na maneno yake ya kuwadhalilisha na kuwashushia heshima. ndio maana hakuna anayeweza kumuunga mkono hata kwa kificho tu, maana kila mtu anaona ni mtu mropokaji, mkurupukaji, Mwenye kujaa mihemuko, jazba, hasira na hivyo kushindwa kutumia Busara na hekima katika kuzungumza na kushawishi watu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Angekua siyo adui mngelimchapa Risasi 38? Na 19 kumuingia
 
Kwa papai kama wewe ndiye unajidanganya hivyo, hatuhitaji tume toka nje tunataka Tume huru, Katiba mpya na uwanja sawa wa kufanya siasa.
Kama ilani tu ya uchaguzi mnashindwa kutengeneza ni vipi mnaweza kuwashawishi watu wenye akili Timamu wawape kura za ndio?
 
Hiyo ya kwenu ambayo kila mwaka mnakiri kuwa haitekelezeki ina faida gani zaidi ya kuwa ni utapeli na hadaa tu kwa wapiga kura?
 
Back
Top Bottom