Tundu Lissu anaongea maneno mengi sana hadi anaishia kujikanganya mwenyewe

Tundu Lissu anaongea maneno mengi sana hadi anaishia kujikanganya mwenyewe

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Mapema leo akiwa Mdabulo, mgombea urais wa CHADEMA kalalamika kuhusu barabara ya kutokea Mafinga mjini.

Kadai eti barabara ni mbaya sana.

Hivi huyu si ndo huwa anamnanga Magufuli kuhusu barabara? Yaani huyu jamaa bana.

Kutwa kucha kumponda Magufuli kuwa eti ni Rais wa mabarabara halafu leo unalalamika kuwa barabara uliyopitia ni mbaya sana. Bure kabisa.

The guy is losing it.

Anzia kwenye dakika ya 1:30 kumsikia anavyojikanganya.
 
What is your point then?

Maana na wewe unalalamika kama yeye.

Pamoja na kuwa magufuli amewekeza kweye barabara haiondoi ukweli kua barabara nyingi za nchi hii bao ni mbovu.

Kulalamikia barabara mbovu imekoa kosa? Kama ni mbovu aseme ni nzuri?

Watu wengine sijui akili hua mnapeleka wapi.
 
Huyo jamaa amekosa sera za kuruka nazo, kwahiyo amebaki na suala la kupinga kila kitu na kumshambulia Mh. John J Magufuli.
 
Huwa mnatumia akili gani kumuelewa Lisu! Lisu hakuwahi kupinga ujenzi wa barabara, mara zote anasema ujenzi uzingatie maisha ya watu kwa upande wa mahitaji mengine. Yani tusielekeze pesa kwenye miundombinu ya barabara tukasahau kuwezesha kilimo, elimu, afya, kuinua kipato cha mwananchi.
 
Tunakushkuru kwa kumfatilia Rais wetu ajaye. Naona unamuadmire sana Tundu Lissu.

#NiYeye2020 #NiTunduLissu
 
Huwa mnatumia akili gani kumuelewa Lisu! Lisu hakuwahi kupinga ujenzi wa barabara, mara zote anasema ujenzi uzingatie maisha ya watu kwa upande wa mahitaji mengine. Yani tusielekeze pesa kwenye miundombinu ya barabara tukasahau kuwezesha kilimo, elimu, afya, kuinua kipato cha mwananchi.

Wanajitoa ufahamu tu Mkuu. Wanamuelewa sana tu. Na watampigia kura vizuri tu.
 
Ndio ujue kuwa hawa jamaa Magufuli kawapiga nje ndani hawana agenda Tena manake rushwa, shirika la ndege, uwajibikaji wa watumishi, ufisadi Magufuli kapambna nazo sasa wanakosa pa kushika wamebaki na hoja za hovyo za kiingereza utafikiri wao wapo competent Sana kwanza sijui Kama Kuna uhusiano wowote wa maendeleo ya wananchi na kiingereza hata China na corea zote mbili zina maendeleo makubwa ktk nyanja zote na hawazungumzi hicho kiingereza hapa ndio utajua kuwa waafrica wenzetu wameshakua totally brainwashed
 
Tatizo ukabila umekutawala na kupelekea ukatae kumuelewa Tundu Lissu!!!

Kwenye maendeleo ya vitu Lissu hajawai pinga ila hoja yake ni kuwa hayatakiwi kufanywa at the expense ya uhuru wa watu au haki za watu

Lissu anapinga pia maendeleo ya vitu yasiyokuwa na mipango thabiti au uwekezaji thabiti wenye matokeo chanya. Mfano mtu unaanzaje kujenga daraja la salander kwa mabilioni ya pesa huku ukishindwa kujenga kilomita 45 za Mufindi huko ambazo wanazalisha mbao na chai ya kutosha????

Tatizo umenyimwa akili na umegoma kumuelewa Lissu kwa hiyo Hilo ni Tatizo lako binafsi
 
Nikiri tu kuwa nyie ni Watanzania halisi, Question to Question, answer to answer Nyani Ngabu Mfukua Makaburi ndo zetu
1600096023766.png
 
Lissu hatoshi kabisa kwenye urais. Hao wananchi wanaomkubali ni kwa sababu hawawezi kuchekecha hoja vizuri, wengu wana kitu unaweza ita " bure syndrome" wanadhani Lissu akishinda basi mahitaji yao yote yatapatikana bure bila kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom