TUJIKUMBUSHE FAILI LA MAOVU YA SERIKALI YA CHAMA DOLA KONGWE CCM LILIPOKUWA JEMBAMBA 2021 KABLA YA OCTOBER 2024 KUTUNA KURASA
Faili la Tanzania linakwenda kuwa nene ( up dated ) kufeli kwa
4Rs za Rais katika Bunge la Ulaya kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu, demokrasia na utawala bora .
TOKA Maktaba:
15 December 2021
View: https://m.youtube.com/watch?v=fVC5CQUk4PoDavid James McAllister MEP ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Ulaya ametoa hotuba nzito na kuwalaumu wataalum wa Umoja wa Ulaya waliotoa ripoti mbele ya kamati hiyo ya Bunge yenye ushawishi mkubwa pamoja na kuaminika kusimamia values / desturi na makubaliano ya kuheshimu haki za binadamu na utawala bora .
Mwenyekiti David James McAllister MEP akakumbushia barua yake aliyoandika kuwaonya wataalamu wa Umoja wa Ulaya EEAS mwaka jana mwezi November 2020 kuhusu "kuubeba" utawala dhalimu usiofuata haki za msingi za kibinadamu yaani Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu ndani ya Demokrasia.
Ripoti hiyo ya wataalamu wa EEAS ilisema kuna maendeleo 'makubwa' nchini Tanzania mbali ya changamoto ndogo ndogo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya akakumbushia hicho kinachoitwa 'changamoto ndogo ndogo' kwa hakika ni kikubwa na hakipaswi kutupiliwa mbali ikiwa watu wanakamatwa ovyo, kutupwa mahabusu, kufunguliwa mashtaka, kutishiwa haki ya kuishi n.k mambo ambayo ndiyo msingi mkubwa wanaousimamia Umoja wa Ulaya wakati wa kutoa msaada kwa nchi yoyote ulimwenguni
EEAS - European External Action Service - European Union External Action
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya amesema mfano wataalamu hao je wameweza kukutana ndani ya Tanzania na mwenyekiti wa CHADEMA au makamu mwenyekiti wa CHADEMA? Ambao ni viongozi wa chama kikuu cha upinzani, mmoja akiwa rumande kwa kesi ya kutunga huku mwingine akiwa uhamishoni Belgium halafu wataalamu hao wanasema ni changamoto ndogo ndogo?
Pia kuna raia wanaoshiriki siasa Tanzania wenye mtizamo mbadala walio wanachama, wapenzi na wafadhili wazalendo wa KiTanzania wanabaguliwa kushiriki ktk vyombo vya maamuzi ngazi zote, wanaoozea ktk jela mbalimbali Tanzania au biashara zao kuhujumiwa je hayo ni mambo madogo ? Amehoji David James McAllister mwenyekiti huyo makini wa kamati ya Bunge la ulaya.
Hivyo amewataka wataalamu hao waliotumwa na bunge la Umoja wa Ulaya kuwabebeleza watawala wa Tanzania kuacha ukandamizaji, kujitathmini kama wanataka kulimwa barua nyingine kali ya karipio kuhusu ripoti yao iliyozua maswali mengi ndani ya Bunge la Ulaya na miongoni mwa wabunge wa Bunge hilo la Ulaya mwaka 2020 na vivyo hivyo pia mwaka huu mwezi November 2021 inayojadiliwa na Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la ulaya amewataka wataalamu hao kuja na majibu mujarabu ya kuibana serikali ya Tanzania kwa kuwa inatumia misaada ya Umoja wa Ulaya itokanayo na kodi za raia wa nchi wanachama zinazoamini katika utawala bora, haki za binadamu kulindwa na demokrasia hivyo haiwezekani nchi viongozi wa nchi walio wakandamizaji kama wa Tanzania kufaidi jasho na nguvu wa walipa kodi wa Ulaya wanaoamini katika uhuru, haki na Maendeleo ya kweli ya watu ktk demokrasia inayozingatia utu.
amesema yeye na wajumbe wabunge wa kamati ya mambo ya nje wanajiandaa kupendekeza hatua "kali" dhidi ya utawala unaoendekeza udhalimu waziwazi na kwa kificho.
David James McAllister mwenyekiti wa Kamati Ya Bunge la Ulaya ya Mambo ya Nje anasema mbali na ripoti hiyo ya wataalamu wake pia wanapata habari kupitia balozi za Marekani, Canada , Uingereza na balozi wa nchi wanachama wanaohudhuria kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya tuhuma nzito za kupikwa dhidi ya Mbowe na wenzie 3, na kesi hiyo ni kichekesho dhidi ya Umoja wa Ulaya na raia wa wa Umoja wa Ulaya ambao wote wanaamini ktk haki mbele ya sheria, demokrasia na kutokuwepo ugandamizaji wa haki za kibinadamu za aina yoyote.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge anataka kuona wataalamu hao wanakuja na mkakati gani wa kuibana serikali ya Tanzania inapotaka misaada na mikopo, kwani sasa siyo muda tena wa maongezi / dialogue yasiyo na kikomo kuhusu hali hii mbaya ya kisiasa nchini Tanzania, bali ni wakati wa Umoja wa Ulaya kufanya matendo kwani muda wa maneno umekwisha, ili ujumbe uwaingie watawala dhalimu....
Serikali, kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye imetoa tamko juu ya matamko yanayotolewa na asasi mbalimbali kuhusu kukamatwa kwa Dr. Slaa, Wakili Mwabukusi, na Mdude. Katika maelezo hayo imeeleza kuwa hakuna Mtanzania aliyekamatwa au atakuja kukamatwa...
RIPOTI YA HALI YA KISIASA NA KIUCHUMI YA TANZANIA
Muenendo wa kuibuka kwa taarifa zisizo sahihi juu ya hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini Tanzania :
02 December 2021
Brussels, Makao Makuu ya
Bunge la Ulaya / EP