Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kwanza naomba kuanza kwa kukupongeza kwa mikakati yenu ikiwemo kuzungumza na Viongozi wa Dini ili kuunga mkono kazi nyeti mnayoifanya ya kuleta mabadiliko ya kweli kwenye Taifa letu. Watu hawa ni wa muhimu sana na kongole nyingi kwenu kwa mikakati hii.
Pili kuna kundi moja nchi hii naomba msilisahau kwenye hizo harakati zenu. Kundi hili huwa linatumiwa vibaya sana na CCM alafu linaachwaga kama Watoto yatima baada ya kutimiza azma za CCM. Kundi hili ni watumishi wa umma na wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Hili ndo kundi la mwisho ambalo likipata akili na kufunuliwa basi udhalimu wa CCM ndo utafikia tamati.
Naomba andaa hotuba kuwaelezea vizuri na kuwaelimisha vizuri juu ya nafasi yao kwenye mustakabali wa hii nchi.
Waeleze kwa namna gani wao wana nafasi ya juu kuliko hawa wanasiasa wa CCM wanaowatumia tu kama madaraja ya kujinufaisha binafsi.
Waeleze kuwa CCM wanawatumia tu kama madaraja huku wakiwaacha kwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji yao na familia zao.
Waeleze namna CCM wanavyowatumia tu huku wakiwaacha na bima za afya zisizoweza kuwahudumia kwenye magonjwa makubwa.
Waeleze namna CCM wanavyowatumia huku wakiwaacha na pensheni za aibu zisizowawezesha kuendesha maisha vizuri baada ya kustaafu. Hii ni kwa wote! Polisi, Wanajeshi, Usalama wa Taifa na wengineo wote.
Waelezee wanavyotumiwa na kikundi cha wachache ndani ya CCM kupitisha mapensheni makubwa kwa wanasiasa na wenza wao huku wao wakiachwa na maisha duni baada ya kumaliza utumishi.
Waeleze kuwa hakuna chochote kibaya kitawapata endapo wakiamua kusimamia haki na kuitosa CCM.
Waambie CCM sio Mungu na bila CCM wataishi maisha mazuri wao na vizazi vyao sio kama wanavyoishi sasaivi huku CCM wakijinufaisha binafsi.
Mwisho waambie namna utakavyoheshimu wataalam na utaalam wao na kuondoa mfumo uliopo wa Wanasiasa kuwa ndo final say hadi kwenye masuala ya msingi ya kitaalam.