Tundu Lissu aongoza kura za mtandaoni dhidi ya Mbowe kwa kura asilimia 84 dhidi ya 16

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,171
Reaction score
4,295


Kwa mujibu wa kura za maoni zilizo fanywa na Jambo online TV matokeo yapo hiv:

Watoa maoni: 12,148

Tundu Lissu kapata kura 10,204 sawa na 84%

Freeman Mbowe kapata kura 1,944 sawa na 16%.

Haya ni maoni ya watanzania walio nje ya mfumo wa Chadema. Wajumbe wa mkutano mkuu wana nafasi ya kuyakubali au kuyakataa.
 
Sijaelewa hapo ulipoandika wananchi wanataka Chadema iongozwe na Mbowe.!
 
Mbowe angeachana na hii kitu kama ana washauri wazuri
 
Punguza pupa kwani unashindana na nani kuwahi kupost taarifa hii mkuu?
 
Kwisha ,nacheka kama mazuri ,simchukii Mbowe ila nacheka kama mazuri
 
Life isn't about working hard, it's about working smart...hata katika biashara unapotafuta masoko ni lazima ufahamu "Targeted Audience" yako ni ipi.
Hata kwenye mpira kinachoangaliwa ni magoli mangapi yameingia wavuni,timu yenye magoli mengi ndio hushinda,hata kama timu pinzani ilikua na ball possession kubwa na wamecheza mpira mzuri lakini wasipofunga ni kazi bure.
Yawezekana Lissu anapendwa na wananchi wa kawaida ila Mbowe akawawin wajumbe wanaopiga kura....
Nimechoka siwafundishi kila kitu✍️
 
M
Mwambieni mbowe aache mambo ya kitemi, chama si mali yake kama anavyo jinasibu chama ni cha wanachama wote from grassroot, kwahiyo kupendwa na sijui na kamati kuu ambao ni wachache lakini wanachama wengine wakawa hawakupendi ambao ni wengi, jibu ni kwamba hupendwi labda atumie utemi wake tu
 
Na akitumia huo utemi wake tutaunga mkono CHAUMA kuliko kuwa na kiongozi ambaye amefikia ukomo wa mawazo na analazimisha kuwepo tu.
 
Maoni ya wana lumumba
 
Omba mods warekebishe kichwa cha habari.
 
Bahati mbaya hao karibu wote sio wajumbe wa mkutano wa uchaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…