Tundu Lissu amepewa passport mpya na Serikali ya Tanzania baada ya ile ya awali kupotea kwa kuibwa kule Ujerumani.
Lissu amekabidhiwa passport yake leo na balozi wetu.
Lissu amesema Rais Samia anafanya kazi kubwa na nzuri sana hivyo Watanzania wote tumuunge mkono ili tujenge Tanzania mpya yenye Upendo na Umoja.
Tundu Lissu amemshukuru sana Rais Samia.
===
"Niko tayari kurudi nyumbani muda wowote baada ya masuala ya kiusalama kukamilika, siishi Ubelgiji kwa hiari yangu naishi kwasababu kuna watu katika nchi yetu ambao walijaribu kuniua, walinipiga risasi nyingi sana na watu hao mpaka sasa Serikali yetu inawaita watu wasiojulikana hakuna uchunguzi uliofanywa hakuna alie kamatwa, hakuna alieshitakiwa, hakuna anayejulikana, kwahiyo katika mazingira hayo inabidi tuangalie masuala ya kiusalama ili niweze kurudi nikiwa salama"- Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu.
Source: Star tv
Maendeleo hayana vyama!