Tundu Lissu apata passport mpya, amshukuru Rais Samia, kurudi Nchini

Naipenda sana nchi yangu, siasa Safi na utawala bora, hongera Rais wetu SSH na Tundu Lissu hii ndiyo nchi tunayoitaka.
 
Samia ni kiongozi ambaye ana baraka za Mwenyezi Mungu
 
Hawatasauliana wote maana wanahitajiana wote ,msione hivi ,moto ulikua unawaka
Ndg.Tundu Lissu hatomsahau mh.SSH maisha yake yote.....

Bila ya mh.rais SSH asingepata STAHIKI ZAKE ZOTE ZA UBUNGE ....

#Siempre SSH 🙏
 
Tanzania ni yetu sote,tupendane.
Asante&hongera kwake SSH,amefanya vyema.
 

Ulichokisema na alichokisema ni tofauti

Lengo lako nn haswaa!?
 
Ni jambo jema. Awaase na viongozi wenzake na wanachama/wanaharakati wa Chadema, wawe wanaokosoa serikali kwa lugha ya staha. Waache kuropoka na kutukana. Wanaweza kufikisha ujumbe wao kwa watawala bila matusi na kashfa na ujumbe ukafika.
 
Ni jambo jema. Awaase na viongozi wenzake na wanachama/wanaharakati wa Chadema, wawe wanaokosoa serikali kwa lugha ya staha. Waache kuropoka na kutukana. Wanaweza kufikisha ujumbe wao kwa watawala bila matusi na kashfa na ujumbe ukafika.

..ubaya wa matendo ya serikali na ccm ndio unaosababisha ukosoaji kwa kutumia lugha kali.
 
Tanzania yetu sote wale wa visasi ,washamba na malimbukeni wa madaraka kazi yenu Ni rahisi kupokea na kuishi maisha halisia ya Kitanzania.
Hapana.

Siyo swala la "visasi", na wala Tundu Lissu au CHADEMA hawajahimiza au kutohimiza visasi.

Mtu/watu wanaojulikana kufanya makosa ni lazima sheria ifuate mkondo wake. Siyo swala la kunyamazia au kufukia fukia tu kwa hivi vimaneno maneno matamu.
Vinginevyo, kama unataka kusawazisha mambo kiutaratibu, basi unda tume itakayochunguza maovu yaliyofanywa kuumiza waTanzania, na isimamie upatanisho na kusameheana kwa waliokosewa na waliowakosea.

Tutakuwa tunafanya makosa kuanza kumsifu mtu (Rais), kwa maneno matamu na vitendo vya hapa na pale visivyokuwa na msingi wake katika taratibu za kisheria. Hii haitakuwa tofauti sana na huko nyuma tulikotoka. Rais huyo huyo, kesho atageuka na kuminya haki na uhuru wa watu asiokubaliana nao.
Tusiwe watu wa kupumbazwa haraka haraka na hadithi tamu za muda mfupi.
 
Na unahakika Samia hakusema lolote juu ya Lissu baada ya kumtembelea Nairobi, au umechagua upande mmoja tu? Kwa hiyo Samia naye tumpachike sifa ya "#dishlimetilt"?

Nakujua wewe, vyema, lakini potelea mbali kwa muda wangu niliopoteza hapa kuandika haya.
 
Maandiko yanatwambia " Tazama ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja "

Ni Jambo jema,, na Ni wakati wa kusameheana kwa mabaya yote na kuyasahau,, tufungue ukrasa mpya kwetu sisi watanzania,, tuwe kitu kimoja!
Huu mstari unatoka kitabu gani mkuu cha bibilia
 
Sio bure yaelekea up mmoja wa wasiojulikana na bado unayatafuta uyatakayo! Ila kamwe hutafanikiwa utajikuta unamfuata yeye uliyeamini ataendelea kutesa taifa la Mungu.
Siku niliposema kitakachompata lissu, waliokuwepo waliona naota. In 24hrs happened what happened.

Sijui unabishia nini. Aache tamaa za madaraka ndani ya chama, atakuwa salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…