Even if, that's still not enough compared to the age of this beautiful nation.....
Taifa hili lina umri wa miaka zaidi na karibu ya 70, leo ndiyo manasumbuka kujenga zahanati???
Stop joking, please...
Kwa umri huu tulionao kama nchi tulipaswa kuwa tumepiga hatua kubwa sana za maendeleo ya kiuchumi na kijamii sawa na na nchi za Malaysia, Singapore, Thailand (kwa bara la Asia); ama Kenya, Nigeria, South Africa ama Ghana kwa Africa...
Huu ndiyo ugomvi tulionao sisi wengine na serikali zote za CCM tangu Uhuru wa nchi hii...
For sure kabisa, tatizo la CCM kuongoza nchi kwa kukumbatia mifumo dhaifu ya utawala ambayo ni "100% centralized" kiasi ambacho maamuzi ya ki - SERA na MIPANGO yamerundikiwa mtu mmoja tu mwenye cheo cha "RAIS MTENDAJI"...
Hili ndilo tatizo na ndiyo mzizi wa fitina unaotakiwa kuchimbwa na kung'olewa kabisa ili nchi ianze kuona mwanga wa jua la asubuhi...!!
Vinginevyo zitakuja chaguzi na chaguzi tukidanganyana usiku na mchana huku maadui UJINGA, MARADHI na UMASKINI wakiendelea kutukalia usiku na mchana bila majibu...!
They are not doing good enough. They have to go. We need new people with fresh ideas, fresh plans to run this country...
TUNDU LISSU naona wazi kaliona tatizo hili. Maono (vision) take ni suluhu ya matatizo yetu kama nchi....
Anasema, jibu lake ni kuufanyia "overhauling" mfumo wetu wa UTAWALA na KISHERIA kwa kuja na makubaliano mapya ya namna tunavyopaswa kujitawala kama nchi yaani - KATIBA
Hii itakwenda sambamba na mahitaji ya wakati huu kwa kuya - address kwa ufasaha matatizo yetu (Maradhi, ujinga na umasikini) na namna ya kuyatatua....
Anataka kuung'oa mfumo wa UTAWALA wa "RAIS MFALME" au "KICHIFU" na kushusha mamlaka kwa wananchi chini kabisa (devolution & decentralization) ili watu wawe na uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao mwenyewe ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika localities zao kwa maana halisi ya "SERIKALI ZA MITAA" bila kuingiliwa na serikali kuu....
Kama kila mtu ana maarifa (akili nzuri) na busara, atamchagua mtu mwenye mawazo haya...!