Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama unajuwa kila kitu, je umepanda miti mingapi nyumbani kwako?
EEEeeenHEEEeeee!
Tusifanye utani mkuu 'Stuxnet', sitanii katika hili. Nina eka mbili za msitu nilio panda mwenyewe. Huu siyo utani hata kidogo.
Hata kama lengo la kupanda hailikuwa huko kupunguza carbon, lakini katika hili I am walking the talk.
 
kweli lakini angalao wamejali baada ya kugundua hawawezi kufunga viwanda kuepusha hiyo carbon emissions. Kila nchi yenye viwanda imepangiwa kiwango cha carbon cha kupunguza, sasa kama huyo beberu anaweza kutengeneza oxygen kwa kupanda miti Tanzania ambayo itafidia kiwango cha carbon anachopaswa kukikata, ubaya uko wapi
Sasa nasi tusiwe mabwege wa kutupa fursa zetu wenyewe. Tunao mkaa wa mawe hapa; na tayari tumekwisha jadili habari za umeme wa gesi na hydro; lakini wa mkaa ni nafuu zaidi ila ni uchafuzi mkubwa.
Kwani hivyo viwanda nasi hatutavihitaji? Kwanza tumechelewa sana.
Mwishowe, hao hao wakubwa hata bidhaa zetu watakataa kununua kama zimetengenezwa kwa kuzalisha carbon nyingi..., huko ndiko tunako elekea, halafu sisi hatujui dunia inakokwenda!
 
sasa kama huyo beberu anaweza kutengeneza oxygen kwa kupanda miti Tanzania ambayo itafidia kiwango cha carbon anachopaswa kukikata, ubaya uko wapi
Ubaya upo katika ubwege wetu wenyewe, kama tunashindwa hata kazi ndogo tu ya kupanda miti wenyewe na kui'manage' ili tufaidike nayo kama huyo mwenye viwanda anavyo faidika na bidhaa za viwanda vyake kwa kutuuzia kwa bei mbaya. Sisi ardhi yetu tunagawa chee kabisa kwa kazi tunayoweza kuifanya wenyewe na kupata faida kubwa.
 
TUNDU LISSU ndiye mtu pekee mzalendo na ana nia ya dhati ya kutuletea maendeleo wa Tanzania
 
CHADEMA hakuna demokrasia kabisa. Huyo Lissu ana uhakika gani chama chake kitampitisha? Au yeye ndo katiba ya chama?

Kauli ya Tundu Lissu inategemea maamuzi na taratibu za chama, wanachama na watanzania at large

Lakini nyie huko ccm kukoje? Si mmeshachapa fomu moja tu? Ya "nani kama mama?"

Mimi nadhani pengine hujui hata maana ya demokrasia. Hiyo ya CCM bila shaka ni demokrasia tu, au siyo MamaSamia2025? Kama ni hivyo, ya CHADEMA iweje siyo demokrasia?

Kwa maoni yangu demokrasia ya CHADEMA ni afadhali mara 1000 kuliko demkrasia ya CCM.

Maana TL kasema wazi kuwa "endapo chama changu kitanipitisha" nitaitikia wito huo na wa Watanzania".

Hapo bado nia iko ndani ya mtu tu. Vipi hii ya kuchapa fomu moja tu na kutishia wote watakaompinga "nani kama mama?". Hiyo ni demokrasia ya aina gani eti?
 
Ana kura yangu tayari na nitahakikisha nachanga za kutosha kwa ajiri ya kampeni, tumechoka na CCM
 
Back
Top Bottom