Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Unatetea mediocrity. Watanzania ni wezi, wavivu na watu wa kuendekeza starehe. Nyerere alianzisha mashirika 400 lakini yote yalikuwa dhoofu hali by 1995.'Seriously'? Utakuwa unazo sababu nyingine kuhusu hili, au huna uelewa mzuri kuhusu masuala haya. Kwa mfano, Natural Gas itakuwaje 'Clean Energy' kuishinda 'Hydro Power'? Hata tofauti ya gharama ya uzalishaji kwa 'unit', pia hujui?
Ninapo andika siwezi kutafuna kila kitu ili msomaji ameze tu bila kutumia akili ya kujua maana ya alicho soma.. Kwa bahati mbaya sana unaonyesha wazi hapa hukuelewa nilicho andika hapo juu, au kwa maksudi tu hukutaka kuelewa kwa sababu zako mwenyewe. Kwa mfano kwa nini mzigo wa lawama juu ya huo unaouita wewe "wizi, uzembe/wavivu" uelekeze lawama kwa wananchi, na isiwe kwa viongozi wanaoongoza nchi? Kwa mara ya kwanza naona maneno yanayotumiwa na kundi maalum lililopo hapa JF, lugha wanayotumia hao hao wasiotaka tufanye mambo yetu muhimu sisi wenyewe. Sasa nielewe kuwa nawe ni mmoja wa hawa chawa wa 'Chura Kiziwi'?
. Niambie/toa mfano ni nchi gani hapa duniani isiyokuwa na mambo hayo yote, tena na ziada!
Marekani hayo hayapo? China hayapo? Korea Kusini hayapo? Singapole/ Malaysia/Vietnam hayapo? Nchi gani duniani hapa pasipokuwa na wezi, majambazi n.k., n.k.. Uarabuni kwa wajomba zetu haya hayapo?
Nilikwisha jibishana na watu kadhaa humu JF kuhusu hili, baada ya wao kuzusha hayo hayo uliyo wazushia waTanzania. Tena ni lugha hiyo hiyo uliyo tumia na wao ni machawa kabisa wa huyo 'Chura Kiziwi'. Sasa unanitia wasiwasi nawe kukuweka kwenye kundi hilo hilo. Mmefundishwa kuwadharau na kuwadhalilisha waTanzania?
Itasikitisha kwelikweli, kama nawe ni sehemu ya watu mlio kuja hapa JF kwa kazi maalum ya kuhubiri uduni wa uwezo walio nao waTanzania na kutoweza kujimudu kufanya mambo yao wenyewe, ili kuhalalisha kugawa raslimali zetu kwa hao mnao wagawia. Sikuwahi hata siku moja kukufikiria katika mlengo huo unao uonyesha hapa leo.
Na uchumi wetu ulianza kuboreka baada ya sera za ubinafsishaji za Mkapa
Mnakosea mnapoleta ubaguzi kwenye biashara. Kwa hiyo ungeona Wazungu wemeshinda zabuni ungesikia raha?
Pesa ziko Uarabuni ndiyo maana hata Waingereza wenyewe wame surrender clubs zao za EPL kwa waarabu. Angalia Newcastle, Mancity, Arsenal etc.
Hata bandari ya Portsmouth pale Uingereza inaendeshwa na DP WORLD, wewe ni nani udharau Waarabu