Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CHADEMA hakuna demokrasia kabisa. Huyo Lissu ana uhakika gani chama chake kitampitisha? Au yeye ndo katiba ya chama?
Hapo utakua haujaelewa Kiswahili,NIA yake iko palepale,ataitikia wito wa WARANZANIA na CHAMA CHAKE.
Rudia kumikiliza tena
 
Amesema "ana nia" yakugombea Urais kupitia Chadema 2025, akiwa na maana endapo kama atapitishwa na vikao vya chama chake.

Hiyo ni tofauti na kusema atagombea Urais kupitia Chadema, hata kama bado vikao vya chama chake kumpitisha mgombea havijakaa.
Waandishe wetu miak hii huwa wa ovyo au wanakuw na upande ndio huleta utata,
 
Nimeishia hapa : "...huyu aliekua anaua Watu...." Nika-stop alafu nikajiuliza

Sasa anaeua Watoto wadogo sasa hivi ni nani? Au Watoto wadogo sio Watu?
 
Mwamba Lissu, interview moja tu, tena ndogo Tayari kajibu na kuzika arguments zaidi ta 100 za MaCCM.

Hapo wakajipange tu tena.
 
Ni Watz hawahawa waliogoma kumchangia hela ya kununulia gari lake?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema nia yake ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 iko palepale.

Tundu Lissu ameyasema hayo leo, Julai 26, 2024 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam alipowasili akitokea nchini Ubelgiji.

Tundu Lissu amesema wakati anamkabili Hayati Magufuli alikuwa na umri wa miaka 52, mwaka kesho atakuwa na umri wa miaka 57 hivyo hawezi kuwa na nguvu zile zile za miaka 52 na kwa miaka 57. Lissu meongeza kuwa nguvu ya hoja, na msimamo wa kisiasa na uaminifu kwa watanzania bado uko palepale.

Huyu mama, kama tuliweza kumkabili Magufuli hajatoa matokeo ya urais mpaka leo, huyu aliyekuwa anaua watu, kama tuliweza kumkabilia miaka mitano iliyopita, huyu mama hatakuwa na shida kubwa kama Magufuli.

Pamoja na yote, hii mama mama mama hii ni ya watu waliohongwa na hii haina shida.

Nia yangu ya kugombea Urais iko palepale, nitaitikia wito wa watanzania, nitaitikia wito wa chama changu.
Ccm itapigwa shoo mpaka ijute , sio maneno yangu bali ni kwa mjibu wa DC WA KIMATAIFA
 
Magufuli:-
1. Alizuia shughuli halali za vyama vya siasa hususan mikutano na maandamano
2. Alikuwa ameitisha Mahakama iamue kwa kuipendelea Serikali
3. Aliliteka Bunge likawa kama kitengo cha Ikulu
4. Alinyang'anya fedha za wafanyabiashara na kuwatupa rumande bila makosa
5. Alikuwa MWONGO sana kwa kuwa alijuwa Watanzania ni wajinga. Alidai anajenga miradi kwa fedha za ndani kumbe anakopa kwenye mabenki ya nje
6. Alidhibiti uhuru wa maoni na kuvitisha kuvifungia vyombo huru vya habari ambavyo vingeripoti kinyume na matakwa yake
7. Aliiba uchaguzi wote wa 2020 na kutuachia wabunge aliowateua yeye

Uzuri wa Magufuli unatoka wapi hapo?
Wewe umeamua kumchukia kwasababu za kwako binafsi but Magu ni moja kati ya best president
1.Alitengeneza nidhamu ya kazi
2.kapunguza matumizi mabaya ya fedha za umma
3.Usimamizi mzuri wa natural resources pamoja na miradi mbalimbali ya nchi
4.mfumo wa haki bila kujali status ya mtu kipindi chake tuliona anyone wengi wakipata haki dhidi ya wenye nacho
5.kupunguza foleni zisizo na ulazima mf flyover ya ubungo imepunguza sana foleni na miundominu mingi imejengwa chini yake katiba nchi nzima
6.kapunguza ukanjanja mwingi wa ajira mfano kaondoa wenye vyeti feki, kulipwa mishahara wafanyakazi waliofariki ( Wafanya kazi hewa)
7.kukabiliana na mambo yanagusa nchi mfano COVIC 19, kupanda kwa bei ya sukari aliweza kutatua hizi issues
8.kucontrol upandaji wa bei za vitu
9.Yeye ndio alileta mfumo wa kulipa mishahara mapema.
 
Hakuna cha ajabu. Huo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambao hata watangulizi wake walifanya. Hata aliyepo anafanya japo Magufuli aliwadanganya kuwa yeye akitoka madarakani hakina mtu mwingine atajenga mabarabara na madaraja.

Mungu akaona isiwe tabu. Kamsepesha 2021 na Tanzania inakwenda kwa kasi sana. Acha kuabudu marehemu
 
Ndio maana nimekwambia wewe unachuki nae binafsi huna sababu ya maana
 
..mimi sielewi Mama unautakia nini Uraisi wa Tanganyika.

..Ningekuwa karibu naye ningemshauri aunde Tume Huru, aandike Katiba Mpya, halafu astaafu.
Kwa kufanya hayo, angekuwa Mama mwana mageuzi halisi wa Nchi hii na ange kumbukwa na wa Tanganyika wengi kwa miongo mingi.
 
Lisu kaingizwa chaka, kaambiwa na mwenyekiti wake kuwa amuachie yeye aendelee kuwa mwenyekiti wa chama, halafu yeye (mwenyekiti atamuachia na kumuunga mkono Lisu kugombea uraisi.

Mwenyekiti katumia akili kuliko Lisu kwani anajua kuwa kushinda uenyekiti huku Lisu akiwa sio mgombea ni rahisi, kuliko kushinda uraisi huku CCM (yenye dola na tume) ikiwa na mgombea.

Mwenyekiti anajua Lisu hawezi kushinda uraisi, ila yeye anaweza kushinda uenyekiti na kuendelea kula mema ya chama kwa miaka mingine mi5 zaidi.
Mkuu, una ujuzi mzuri wa kutengeneza move; Hongera
 
Huyo Samia kapitushwa na nani na uchaguzi ni 2025? Sisi tunajua hii ni awamu ya 5 anamalizia. Tofauti na ninyi mnaotuaminisha kuwa ni awamu ya 6. Basi uchaguzi ufanyike mwezi wa 3,2026. Miaka mitano itakuwa imetimia awamu ya 6 kama sikosei!
 
Back
Top Bottom