Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nihesabie mie nitakuwa mpiga kampeni wa kujitegemea asiye kwenye timu maalum, na ambaye hahitaji malipo ya aina yeyote. Huo utakuwa mchango wangu kwa Taifa langu na vizazi vijavyo, maana hakika chini ya uongozi wa Lisu, sote tutakuwa na uhakika wa maslahi ya Taifa.
Umeliweka vizuri sana hili. Tundu Lissu hatakuwa mgombea wa CHADEMA pekee, atakuwa ni mgombea wa wote wanaojali maslahi ya taifa letu.
Naungana nawe kutangaza nia ya kumpigia kampeni Tundu Lissu bila ya kuhitaji malipo yoyote, bali malipo ni kuliona taifa letu likiinuka tena na kupata heshima linalo istahiri.
 
Huyu kwa Urais HAPANA. Uwaziri Mkuu sawa kabisa. Watu ambao hawakubali mawazo ya wenzao na kujiona kila wakati wako sawa huwa wanaishia kuwa viongozi wabaya sana kama Magufuli
Nimekubali mawazo ysko but hapo kwa Magu nimekataa Magu hakuwa kiongozi mbaya
 
Labda wewe, lakini nchi hii haina nafasi tena ya kuleta kichaa mwingine kama Magufuli kwenye uongozi wa Taifa letu.

Mungu katusadia kumtoa yule naamini alikusidia kuikoa nchi yetu isiharibike na kuwa kama Somalia
Wewe una yako mengine pembeni.
Unatumia mfano wa Magufuli kutishia watu. Hii ni dharau kubwa kwa hao unao watisha' kwamba hawana uwezo wa kuona tofauti kubwa zilizopo baina ya watu hao wawili.

Magufuli ubaya wake unafahamika; na laiti isingekuwa kwa hayo mabaya, Magufuli angekuwa ni kiongozi mzuri sana wa taifa hili.

Unachoweza kufanya sasa ni bora kumpamba 'Chura Kiziwi" wako, kama unavyoweza kumnakishi nguruwe na kumvisha shela aonekane kuwa Bi Harusi aliye pendeza, lakini hata hilo halitatosha tena safari hii.
Utapoteza muda bure kujaribu kutishia watu kwa kutumia ubaya wa Magufuli; ambaye kwa mazuri yake, hata waliochukizwa na yale mabaya, wanamtambua kwa hayo mazuri.

Hivi hata huwezi kutambua kuwa Tundu Lissu mwenyewe aliyepitia kwenye magumu ya Magufuli hatumii tena mfano huo kutishia watu?
 
Mbowe ana nguvu sana nchi hii, kumbe alimpiga risasi Lissu na akawazuia poliis kufanya uchunguzi!?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Halafu tena kwenye sehemu nyeti ya serikali na cctv-camera, na ulinzi wa kutosha, eti mpaka leo hawajulikani. Lilikua jambo la kihuni sana na serikali??
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema nia yake ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 iko palepale.

Tundu Lissu ameyasema hayo leo, Julai 26, 2024 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam alipowasili akitokea nchini Ubelgiji.

Tundu Lissu amesema wakati anamkabili Hayati Magufuli alikuwa na umri wa miaka 52, mwaka kesho atakuwa na umri wa miaka 57 hivyo hawezi kuwa na nguvu zile zile za miaka 52 na kwa miaka 57. Lissu meongeza kuwa nguvu ya hoja, na msimamo wa kisiasa na uaminifu kwa watanzania bado uko palepale.

Huyu mama, kama tuliweza kumkabili Magufuli hajatoa matokeo ya urais mpaka leo, huyu aliyekuwa anaua watu, kama tuliweza kumkabilia miaka mitano iliyopita, huyu mama hatakuwa na shida kubwa kama Magufuli.

Pamoja na yote, hii mama mama mama hii ni ya watu waliohongwa na hii haina shida.

Nia yangu ya kugombea Urais iko palepale, nitaitikia wito wa watanzania, nitaitikia wito wa chama changu.
Chakademus watampitisha?
 
..Lissu wakati anagombea 2020 alisema hapendi kuwa Raisi mwenye mamlaka ya ki-mungu mtu kama ilivyo sasa hivi. Sasa unaposema anafanana na Magufuli naona kama umelenga kudharau jukwaa letu.
Kusema ni kitu kimoja, na kutenda ni kitu kingine.
 
Nimekubali mawazo ysko but hapo kwa Magu nimekataa Magu hakuwa kiongozi mbaya
Magufuli:-
1. Alizuia shughuli halali za vyama vya siasa hususan mikutano na maandamano
2. Alikuwa ameitisha Mahakama iamue kwa kuipendelea Serikali
3. Aliliteka Bunge likawa kama kitengo cha Ikulu
4. Alinyang'anya fedha za wafanyabiashara na kuwatupa rumande bila makosa
5. Alikuwa MWONGO sana kwa kuwa alijuwa Watanzania ni wajinga. Alidai anajenga miradi kwa fedha za ndani kumbe anakopa kwenye mabenki ya nje
6. Alidhibiti uhuru wa maoni na kuvitisha kuvifungia vyombo huru vya habari ambavyo vingeripoti kinyume na matakwa yake
7. Aliiba uchaguzi wote wa 2020 na kutuachia wabunge aliowateua yeye

Uzuri wa Magufuli unatoka wapi hapo?
 
Wewe una yako mengine pembeni.
Unatumia mfano wa Magufuli kutishia watu. Hii ni dharau kubwa kwa hao unao watisha' kwamba hawana uwezo wa kuona tofauti kubwa zilizopo baina ya watu hao wawili.

Magufuli ubaya wake unafahamika; na laiti isingekuwa kwa hayo mabaya, Magufuli angekuwa ni kiongozi mzuri sana wa taifa hili.

Unachoweza kufanya sasa ni bora kumpamba 'Chura Kiziwi" wako, kama unavyoweza kumnakishi nguruwe na kumvisha shela aonekane kuwa Bi Harusi aliye pendeza, lakini hata hilo halitatosha tena safari hii.
Utapoteza muda bure kujaribu kutishia watu kwa kutumia ubaya wa Magufuli; ambaye kwa mazuri yake, hata waliochukizwa na yale mabaya, wanamtambua kwa hayo mazuri.

Hivi hata huwezi kutambua kuwa Tundu Lissu mwenyewe aliyepitia kwenye magumu ya Magufuli hatumii tena mfano huo kutishia watu?
Basi tuseme Tundu Lissu ni mwema na kiongozi mzuri kama Magufuli. Ukiipenda hii nijulishe
 
5. Alikuwa MWONGO sana kwa kuwa alijuwa Watanzania ni wajinga. Alidai anajenga miradi kwa fedha za ndani kumbe anakopa kwenye mabenki ya nje
Alidanganya kwamba maabara ya taifa iliona virusi vya corona kwny mapapai.
Alidanganya kwamba tumejenga viwanda vipya zaidi ya 4000.
 
Alidanganya kwamba maabara ya taifa iliona virusi vya corona kwny mapapai.
Alidanganya kwamba tumejenga viwanda vipya zaidi ya 4000.
Ongeza million hamsin kila Kijiji na mtaa

Nafikili kwenye kipindi chake waliokuwepo walikuwa wamejazwa mapesa
 
Mbingu na ardhi zote ziko upande wa Tundu Lissu , rais wetu ajaye , rais m'beba maono .
 
Back
Top Bottom