Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ametangaza jambo hilo alipoulizwa na Mwandishi wa habari iwapo bado anayo dhamira ya kufanya hivyo.

Lissu anesema kwamba Japo 2025 atakuwa na Umri wa miaka 57 lakini bado anaamini atakuwa na uwezo huo.

View attachment 3052937
Huyu kwa Urais HAPANA. Uwaziri Mkuu sawa kabisa. Watu ambao hawakubali mawazo ya wenzao na kujiona kila wakati wako sawa huwa wanaishia kuwa viongozi wabaya sana kama Magufuli
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundi Lissu amesema nia yake ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 iko palepale.T undu Lissu ameyasema hayo leo, Julai 26, 2024 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam alipowasili akitokea nchini Ubelgiji.
Kama Lissu atagombea basi kura yangu anayo, kama hatogombea sitapiga kura.
 
Lisu kaingizwa chaka, kaambiwa na mwenyekiti wake kuwa amuachie yeye aendelee kuwa mwenyekiti wa chama, halafu yeye (mwenyekiti atamuachia na kumuunga mkono Lisu kugombea uraisi.

Mwenyekiti katumia akili kuliko Lisu kwani anajua kuwa kushinda uenyekiti huku Lisu akiwa sio mgombea ni rahisi, kuliko kushinda uraisi huku CCM (yenye dola na tume) ikiwa na mgombea.

Mwenyekiti anajua Lisu hawezi kushinda uraisi, ila yeye anaweza kushinda uenyekiti na kuendelea kula mema ya chama kwa miaka mingine mi5 zaidi.
 
Back
Top Bottom