Hapa unamwonea mnyalukolo Thebaptist. Hajadhihaki kifo cha mtu, bali anaonesha ukuu wa Mungu.
Nadhani anadhihirisha lile andiko lisemalo:
'BWANA asipoulinda mji, wakeshao wakesha bure'.
Tunamshukuru sana Mungu, kwa matendo yake makuu juu ya Lisu maana hakika lingefanikiwa jambo lile alilokusudia shetani kupitia kwa hawa mawakala wake waliopo nchini, simanzi za wapenda haki zingekuwa ni kubwa mno, na pengine wengine wangevunjika mioyo ya imani wakiamini sala zao Mungu amezipuuza. Shetani alizuia hata maombi ya pamoja kwaajili ya Lisu, lakini bado watu waliendelea kuomba kila mtu kwa namna yake. Yalikuwa maombi ya moyo na si maombi ya maonesho.
Mungu hutenda kila jambo kwa wakati na kwa hekima yake, ambayo hakuna aijuaye kwa hakika.
Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wetu ulite Mkuu sana, ukuu wako tumeuona juu ya Lisu na wengine wengi, tuwajuao na tusiowajua. Tunaomba uendelee kuwafedhehesha mawakala wa shetani maana baadhi hawajakata tamaa.
Na Lisu atambue kuwa walitaka kumwua kwa sababu ya kuwa mkweli. Basi hata baada ya kunusurika kifo kike, adumu kwenye ukweli, tena kwa ujasiri ulio mkuu.