Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Hii hoja ni nzito nawashauri wana bodi tuache ushabiki,tuweke kando tofauti zetu za dini,kabila na siasa. Wahusika wajibu hoja kwa kina kama mtoa tuhuma alivyotoa maelezo yenye takwimu alozifanyia uchunguzi. Yaweza kuwa takwimu za Lissu ni za uongo! Kama watabaki kimya sisi tutauamini uongo huo na hapo ndipo usemi kuwa rais wetu ni dhaifu utajidhihirisha kuwa ni kweli.
 
ni kweli mkuu, hapo ni urafiki na kujuana na si udini!
 
Chezea tundu lissu wewe? Tungekuwa na wabunge kama tundu 100,tanzania ingesonga mbele kimaendeleo kwa spidi 1000. E mwenyezi mungu endelea kumjalia kiumbe wako lissu! God bless Tanzania!
 
Si ajabu hao ni ndugu zake au waliwahi kuwa washikaji zamani Raisi wetu ni zaidi ya umjuavyo yeye kufuata katiba kuendesha nchi kwake ni tusi ,ashukuru watanzania wapole kama kondoo nchi zingine angekiona
Nakubaliana na wewe kabisa. Katika marais wanaokiuka katiba, kikwete ameweka rekodi ambayo haitakuja ivunjwe kamwe.
 

Lissu na ateue wake; Raisi ameteua kwasababu wanasifa zinazotakiwa hata leo hii Lissu akiteuliwa wapo watu watasema Lissu hana sifa; sasa kama huyu mwanaharakati wenu Lissu na atue jopo lake la majaji.
 

Nimepitia vipengele vyenye red katika katiba nimeona viko sahihi kabisa. LAKINI KIPENGELE CHA 9 KATIKA IBARA HIYO YA 109 INASEMA HIVI"(9) Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenye
sifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa
muda usiopungua miaka mitano, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi
na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa
Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili
kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutangua lile sharti
la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano, na
baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama, Rais
aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu."

KWA MANTIKI HIYO BASI, RAIS YUKO SAHIHI KABISA KUWATEUA ALIOONA WANAFAA.
 

Mimi nashauri LISSU ateuliwe kuwa Jaji hizi kelele za wivu ziishe.
 
watanzania tumezoea kusikia, leo Rais ameteua majaji lkn hatufatilii, ndio maana Wanatuonea. lkn nashukuru Mungu Lisu katufumbua macho sasa.
Lissu keep it up!! Tuko pamoja lzm kieleweke tu. peoplessssssssssssss!!!!!!!
 
Udini tuweke pembeni. Zinazotakiwa ni CV as per job qualifications. As well with shoddy CVs haki haiwezi kupatikana. Kwenye utaalamu wa uhandisi siku hizi ule utashi na ufahamu wa kazi haupo for some engineers hence forth barabara majengo, miradi ya maji inajengwa chini ya viwango! Wabunge maiinjinia fuatilieni na hili tafadhali!
 

Daaa! Aisee tanzania bana kila kukicha ni udaifu tuu unajitokeza! Si wajiuzulu sasa!

Sent from my BlackBerry 9360 using Jamie's
 
Ebu yaangalie haya, nayo ni kutafuta umaarufu wa kisiasa? Lissu kasema haya

1. Jaji Fatuma Masengi, alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Singida na baadaye akawa Hakimu Mkazi kisha akaanza kujisomea Chuo Kikuu Huria na kuhitimu mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa jaji mwaka 2006.

Alihoji kuwa kama katiba inaelekeza mtu awe jaji ni mpaka awe amekuwa hakimu kwa miaka 10, huyu alipataje kuwa jaji?

2. Jaji Latifa Mansoor, ambaye pamoja na kuwa na shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa 1993, lakini alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala.

Kwamba baadaye alipoibuka mwaka 2008 aliteuliwa kuwa jaji wakati hajawahi kuwa wakili, na kwa kuwa alifukuzwa katika utumishi wa umma.

3.J
aji mwngine aliteuliwa na Rais akiwa wagonjwa ili aweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja.

Bwana Salva Rweyemamu mwonyeshe Mheshimiwa Rais andiko hili la Lissu kama lina kasoro yoyote
 
Watasema mnatafuta 'cheap popularity' . Hawana majibu zaidi ya dhihaka
 
Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa," alisema Lissu.

Alishangaa viongozi wanaojitokeza kumjibu akisema hata Katiba ya Zanzibar 94 (3) inasema; ili mtu achaguliwe kuwa jaji, ni lazima awe na shahada ya Chuo Kikuu.

"Huyu jaji ambaye anasoma sasa alipataje kuwa jaji kabla ya kuwa na shahada ambayo ndiyo sifa ya msingi?" alihoji.

 
Na kwa jinsi JK alivyomuoga,ameagiza MAWAZIRI,MANAIBU WAZIRI,MAJAJI,WAKUU WA MIKOA,NA WAKUU WA WILAYA kuanza kulindwa mara moja na jESHI LA POLISI, kwani kuna majaji wamelalamika kuwa hawalindwi na wanahofia usalama wao,na pengine ndo hao waliotajwa na LISSU,tanzania kazi tunayo kila kitu FAKE.
 
Si ajabu hao ni ndugu zake au waliwahi kuwa washikaji zamani Raisi wetu ni zaidi ya umjuavyo yeye kufuata katiba kuendesha nchi kwake ni tusi ,ashukuru watanzania wapole kama kondoo nchi zingine angekiona

Hapo pekundu ongeza na Au UDINI? Tazama majina ya walio wengi waliotajwa bila sifa!!
 
Mimi nashauri LISSU ateuliwe kuwa Jaji hizi kelele za wivu ziishe.

Ndio tatizo la wa TZ walio wengi kila mpinga uovu na uvunjifu wa haki na sheria anaonekana ana wivu. Hii nchi ni yetu sote na mishahara na posho wanazolipwa hawa majaji hewa pa1 na rais aliyewateua zinatoka kwetu kila tunaponunua kiberiti, chumvi n.k, lazima tufuatilie usahihi wa matumizi yake, au wewe unaona sawa kwa kuwa kila baada ya miaka mitano una uhakika wa kupata fulana, skafu, kapelo na kanga mpya?
 

Mimi sikuwai kuisoma katiba hata siku moja lakini kwa jinsi nilivyosoma hoja yako nadhani ukuelewa maana ya LAKINI iliyokusudiwa kwenye kifungu tajwa. Kwa uelewa wangu na naomba tusibishane bali tuendelee kuelimishana na kuelekezana, ile lakini imepunguza sifa ya muda wa miaka kumi lakini sharti la kuwa na digrii na uwakili ni lazima yawepo, sasa jaji anayelalamikiwa ata diprii bado hajaipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…