Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

"Mtu anachaguliwa kwa mujibu wa katiba alafu anashindwa kuilinda katiba....hatufai kabisa....aende shambani kwake akalime"Nyerere.
Ila sinakumbukumbu kama kweli rais huyu alichaguliwa kwa mujibu wa katiba.Huenda ndio maana anaichezea.
 
Tundu na zito hawatofautiani kitu katika kujitafutia umaarufu binafsi,tofauti yao ni kuwa tundu anabebwa na dini yake mbele ya pro chadema,wanampenda na ujinga wake

nashindwa kuelewa kama umeisoma vizuri hoja ya Lisu kwa aina ya mchango unaotoa katika hoja hii.Sikufikiri kama kuna watanzania wanaoweza kutoa michango ya aina hii kwa hoja nzito kama hii.
Tunao wengi, akina Mulugo na yule mganga mkuu wa mkoa fulani hapa Tanzania ambaye pia hoja yake ililetwa humu humu kwenye JF.
 
Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action. Sio aliyewateua ndio mdini. Hatahivyo kuna waislam wengi wenye sifa zilizotajwa na Mh. Tundu Lissu.
 
Kama madai ya Lissu ni sahihi basi hatuko salama!
Kwanini yasiwe sahihi wakati wajibu hoja hujibu kwa ujumla badala ya hoja kwa hoja.. kwamfano mtu katajwa kwa jina na tuhuma unapojibu lazima umtaje kwa jina na utetezi (hoja) wako sio kusema kwa jumla tu kwamba taratibu hufuatwa.
 
Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action. Sio aliyewateua ndio mdini. Hatahivyo kuna waislam wengi wenye sifa zilizotajwa na Mh. Tundu Lissu.
Hebu fafanua udini umekaa vipi hapo.. yani kuitaka serikali kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ni udini.. kweli unakazi. Mwenyewe unakiri kuwa wapo waislamu wenye sifa, sasa kwanini asiwateue hao anakwenda kuteua wenye walakini?
 
Lissu na ateue wake; Raisi ameteua kwasababu wanasifa zinazotakiwa hata leo hii Lissu akiteuliwa wapo watu watasema Lissu hana sifa; sasa kama huyu mwanaharakati wenu Lissu na atue jopo lake la majaji.

Mkuu hujaji kitu hoja ya lissu ipo wazi vigezo umepewa sasa mbona hujibu hoja.
 
Kwa kifupi kabisa kipengele hii peke yake inatosha kum-impeach Rais Kikwete kwa kuvunja na kuendelea kuvunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania:

"Lissu alifafanua kuwa, katika hoja zake alisema kuna baadhi ya majaji waliteuliwa bila kuwa na sifa maalumu kama zilivyobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 109, kipengele cha 6, 7 na 8.

“Ibara hiyo ya 109 kipengele cha 6-8 kinasema; mtu anaweza kuwa Jaji iwapo tu ana shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa kisheria, awe ameshakuwa hakimu, awe ameshakuwa wakili na kusajiliwa na sifa zote hizo ziambatane na utumishi wa miaka kumi mfululizo.

“Lakini sifa zote hizo lazima mtu anayeteuliwa kuwa Jaji awe nazo kwa miaka kumi mfululizo. Sasa badala ya kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla jumla, ningependa wanaonijibu watamke wazi wazi Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa,” "

Wananchi sisi ni waoga lkn hii ni skendo kubwa ajabu tena ya kimataifa. Kisheria hii ni kosa kubwa kuliko Clinton kudanganya kuhusu Monica Lewinsky .. hii ni unconstitutional, deliberate and direct interference of executive branch in the judiciary branch! Huu ni uvunjaji wa misingi ya demokrasia!
 
"Nchi hii inanuka udini..... yaani mtu leo hii anaongelea udini! Badala ya kuongelea ujenzi wa nchi..." Nyerere
Maoni yangu ni kwamba siasa siku zote natokana na maslahi ya watu wachache sasa katika ulimwengu wa leo dini+ siasa ndo vitaivuruga democrasia badala ya kuijenga!!
 
Mimi ningependa hao watumishi wa serikali kuanzia naibu waziri wa katiba na sheria pamoja na waziri wake, katibu mkuu kiongozi, jaji kiongozi na jaji mkuu na hata raisi kikwete mwenyewe wajitokeze na utetezi wenye kueleweka.

Kwakuwa Lissu amewataja kwa majina majaji wasio na sifa ya kuwa majaji basi nao wawataje kwa majina na kuthibitisha kwamba wana sifa za kuwastahili kuwa majaji.

My friend Mwita...siasa kuingizwa kwenye utendaji ni kosa kubwa sana sana. JK alichoangalia ni ushkaji, u ccm, uswaiba...bila kijali taaluma. Kuna haja katiba mpya itenganishe hivi vitu.

Hawa jamaa hawatakaa wajitokeze kujibu hoja kwa jinsi unavyotaka. Kinachotakiwa ni mipango ya kichama ktk kushughulikia hili jambo. Tuanze na bungeni...likishindikana tulirudishe kwa wananchi kwa kutumia nguvu nyingi ya pamoja. Haki haiombwi bali inadaiwa.
 
Mkuu hujaji kitu hoja ya lissu ipo wazi vigezo umepewa sasa mbona hujibu hoja.

Lissu katoa vigezo vyake anavyotaka yeye; Raisi anateua majaji kwa mujibu wa katiba inavyomruhusu; sasa yeye Lissu kama haradhiki na uteuzi wa majaji huo ni mpango wake; mpaka sasa hakuna aliyelalamika na maamuzi ya majaji husika na kwa utaratibu wa maamuzi ya mahakama kuu na rufaa ni jopo la majaji ndilo linalotoa maamuzi; Lissu na atueleze ni wapi Raisi amekiuka madaraka yake kuteua hao majaji.
 
Lissu katoa vigezo vyake anavyotaka yeye; Raisi anateua majaji kwa mujibu wa katiba inavyomruhusu; sasa yeye Lissu kama haradhiki na uteuzi wa majaji huo ni mpango wake; mpaka sasa hakuna aliyelalamika na maamuzi ya majaji husika na kwa utaratibu wa maamuzi ya mahakama kuu na rufaa ni jopo la majaji ndilo linalotoa maamuzi; Lissu na atueleze ni wapi Raisi amekiuka madaraka yake kuteua hao majaji.

Mfano kunajaji hana shahada ya sheria sasauivi ndio anasoma open mkuu nani moja ya vigezo,mwingine ni mgonjwa kateuliwa akiwamgonjwa inamaana Jk hakujua anateua mgonjwa?
 
Mfano kunajaji hana shahada ya sheria sasauivi ndio anasoma open mkuu nani moja ya vigezo,mwingine ni mgonjwa kateuliwa akiwamgonjwa inamaana Jk hakujua anateua mgonjwa?

Je kuna kipengele cha katiba kilichikiukwa? Katiba inasemaje kuhusu mamlaka ya Raisi kwenye kuteua majaji?
 
Hebu fafanua udini umekaa vipi hapo.. yani kuitaka serikali kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ni udini.. kweli unakazi. Mwenyewe unakiri kuwa wapo waislamu wenye sifa, sasa kwanini asiwateue hao anakwenda kuteua wenye walakini?
ahsante mchape na bakora kama ataendelea kuandika upuuzi
 
Mimi ningependa hao watumishi wa serikali kuanzia naibu waziri wa katiba na sheria pamoja na waziri wake, katibu mkuu kiongozi, jaji kiongozi na jaji mkuu na hata raisi kikwete mwenyewe wajitokeze na utetezi wenye kueleweka. Kwakuwa Lissu amewataja kwa majina majaji wasio na sifa ya kuwa majaji basi nao wawataje kwa majina na kuthibitisha kwamba wana sifa za kuwastahili kuwa majaji.
Bado sasa hivi wako busy wanatafuta vyeti vya kughushi katika vyuo vya nje au vya ndani, wanabadilisha miaka ya kumaliza vyuo, wanatafuta kesi kadhaa za kughushi ili ionekane wameshauri na kuamua kesi nyingi tu kwa miaka 10 na wana degree zao...BAADA YA HAPO WATAJITOKEZA KUJIBU HOJA YA TUNDU LISSU, sasa hivi si unawaona hata watuhumiwa wako kimya sana? Ni nani yuko tayari kutuhumiwa hadharani halafu akawa hana hatia na akakaa kimya bila kuleta ushahidi? Mimi wakijitokeza baadae nitajua tu wameshafanikiwa kughushi nyaraka na vyeti! Nitawashauri wafuatilie uhalali wa vielelezo hivyo hadi mwisho kwa uangalifu!
 
Lissu amkomalia JK

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ameendelea kumwandama Rais Jakaya Kikwete, akisema baadhi ya majaji aliowateua hawana sifa, na kwamba viongozi wa serikali waliojitokeza kumpinga wameshindwa kujibu hoja.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana katika ofisi ndogo ya Bunge, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), alisema kuwa alishatoa maelezo hayo hata katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi.

“Nilieleza jinsi rais alivyofanya uteuzi wa baadhi ya majaji pasipo kupata ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Wamekuwa wakijibu kiujumla, mimi niliwataja kwa majina yao na hata hili nilieleza katika Kamati ya Ngwilizi ambayo taarifa yake haikuwekwa hadharani pasipo sababu za kueleweka,” alisema.

Alisema wanaotaka kujibu hoja zake wanapaswa kuweka hadharani orodha ya majina ya majaji waliopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama kuanzia mwaka 2005 wakati Rais Kikwete alipoingia madarakani.

Lissu aliwataja baadhi ya watu waliowahi kujitokeza kumjibu kuwa ni Naibu wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, ambaye alisema kuwa serikali ina taarifa hizo na itazifanyia kazi.

Alisema kuwa msimamo huo ulikubaliwa na waziri wake, Mathias Chikawe na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambao kwa nyakati tofauti walisema kuwa, endapo serikali itachukua hatua ambazo alipendekeza watakuwa wanaingilia uhuru wa mahakama.

Wengine waliojitokeza kujibu hoja yake ni Jaji Mkuu, Othman Chande na Jaji Kiongozi, Faki Jundu ambao walisema kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni si za kweli.

Pia Rais Kikwete naye alikaririwa hivi karibuni akiwa jijini Arusha ambapo bila kumtaja Lissu kwa jina, alisema kuwa majaji wanateuliwa kwa kufuata utaratibu na wana sifa zinazostahili.

Ni kutokana na kauli hizo, Lissu alifafanua kuwa, katika hoja zake alisema kuna baadhi ya majaji waliteuliwa bila kuwa na sifa maalumu kama zilivyobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 109, kipengele cha 6, 7 na 8.

“Ibara hiyo ya 109 kipengele cha 6-8 kinasema; mtu anaweza kuwa Jaji iwapo tu ana shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa kisheria, awe ameshakuwa hakimu, awe ameshakuwa wakili na kusajiliwa na sifa zote hizo ziambatane na utumishi wa miaka kumi mfululizo.

“Lakini sifa zote hizo lazima mtu anayeteuliwa kuwa Jaji awe nazo kwa miaka kumi mfululizo. Sasa badala ya kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla jumla, ningependa wanaonijibu watamke wazi wazi Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa,” alisema.

Alishangaa viongozi wanaojitokeza kumjibu akisema hata Katiba ya Zanzibar 94 (3) inasema; ili mtu achaguliwe kuwa jaji, ni lazima awe na shahada ya Chuo Kikuu.

“Huyu jaji ambaye anasoma sasa alipataje kuwa jaji kabla ya kuwa na shahada ambayo ndiyo sifa ya msingi?” alihoji.

Lissu aliwataja majaji wengine ambao wameteuliwa bila kuwa na sifa kuwa ni Fatuma Masengi, ambaye kwa mujibu wa Lissu alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Singida na baadaye akawa Hakimu Mkazi kisha akaanza kujisomea Chuo Kikuu Huria na kuhitimu mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa jaji mwaka 2006.

Alihoji kuwa kama katiba inaelekeza mtu awe jaji ni mpaka awe amekuwa hakimu kwa miaka 10, huyu alipataje kuwa jaji?

Majaji wengine waliotajwa ni Latifa Mansoor, ambaye pamoja na kuwa na shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa 1993, lakini alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala.

Kwamba baadaye alipoibuka mwaka 2008 aliteuliwa kuwa jaji wakati hajawahi kuwa wakili, na kwa kuwa alifukuzwa katika utumishi wa umma.

Lissu pia alimlalamikia Rais Kikwete kwa kutumia vibaya madaraka yake kwani anateua majaji wa mikataba, ambao wameshastaafu na kulipwa mafao yao.

Aliongeza kuwa, majaji wengine waliteuliwa na Rais wakiwa wagonjwa ili waweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.

Kufuatia utata huo, Lissu emeendelea kushikilia msimamo wake kuwa anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili Bunge liweze kuchunguza utendaji wa rais kuhusu uteuzi wa majaji.

Lissu alisema Bunge litaangalia kama rais ameteua majaji kwa mujibu wa katiba au ameikiuka, na kwamba yeye ana uhakika kuwa rais amekiuka katiba.

Chanzo: Tanzania Daima | Nov 29, 2012



Nadhani ni muhimu yatolewe maelezo ya kina kutoka serikalini kwa hawa waliotajwa na Lissu!!!!!!!!!!!
 
Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action. Sio aliyewateua ndio mdini. Hatahivyo kuna waislam wengi wenye sifa zilizotajwa na Mh. Tundu Lissu.
Mkuu pole sana naona kweli umefilisika kimawazo na kiakili. Umebakia kukimbilia kwenye udini na ukabila. Jitahidi kuukumbatia mpaka siku utakapopata akili ya kuelewa na kuchambua mambo
 
Pole sana mheshimiwa ningekuwa ni ww na nina mawazo km yako nadhani ningesimama kusema ndugu wanajf naombeni radhi kwa mawazo yangu maana hayana maana ktk ujenzi wa taifa bali katika maana ya kulibomoa taifa. Nadhani unatakiwa kujiunga na wanywa kahawa magengeni na kutoa hoja kama hizo ndugu yangu maana ukumbuke unaowatolea hoja zako hapa co km ww ulivyo na hduma hii ni kwa manufaa ya wengi hivyo basi lenga katika kutoa hoja za ujenzi wa taifa na c kulibomoa na nikikuuliza unaushahidi na usemayo najua huna hata tone kiasi cha chanjo kwa mtoto. Pole sana.
 
Wapendwa Tanzania inaangamia polepole. JK alishashindwa kuongoza kabisa. Sheria ni mhimili mkubwa sana katika kulitegemeza taifa. Sheria imetoweka. Mahakama imebaki kitendawili na viongozi wa nchi wako kwenye usanii tu wakidhani ni utani. JK nchi bila sheria haitawaliki. Wajukuu zako mwenyewe watajakukata mapanga ukiwa kitandani kwenye nyumba wako. Na ndipo utagundua ni kwa jinsi gani ulivyowaharibia nchi yao ambayo kihistoria ilishawahi kuwa kisiwa cha amani. Tuache kejeli. Hili ni anguko kubwa ktk utawala wa awamu ya nne. Mungu ambariki Lisu kwa kutufahamisha wadanganyika.
 
Back
Top Bottom