Shida sio nani katekwa bali nani mtakaji. Na kwa nini ateke. Na kwa nini aue watu wa tabaka fulani mfano mmoja tu nadhani unakumbuka idadi na aina ya watu waliouliwa Mkuranga, Rufiji na Kibiti. Ikiwa ni pamoja na askari na Viongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji. Fikiria hapo kwanza. Kisha nitakupa mifano mingine zaidi.
Sent using
Jamii Forums mobile app
..kuna kikundi cha kigaidi ndicho kilichokuwa kinaua viongozi wa serekali na ccm maeneo ya mkuranga-kibiti-rufiji.
..kikundi hicho inasemekana kina mahusiano na kikundi kingine kilichoko kaskazini ya Msumbiji ktk jimbo ambako imegundulika hazina kubwa ya gesi.
..kuna kikundi kingine kilichokuwa kikishughulikia viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.
..Vyombo vya dola vingekuwa huru na wawazi vingeshughulika na vikundi hivyo viwili na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria/mahakama.
..So far, inaelekea walioshughulikiwa ni kile kikundi cha magaidi wa mkuranga-kibiti-rufiji. Lakini serekali haijaeleza wahusika walikuwa ni kina nani, na kwanini walikuwa wakiua viongozi wa serekali na CCM.
..Wakati huohuo serekali imeonyesha kutokujali kabisa kuhusu kupotezwa na kuuwawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani.
NB.
..katika kushughulika na magaidi wa mkuranga-kibiti-rufiji kuna wananchi zaidi ya 300 inatuhumiwa walichukuliwa na vyombo vya dola ktk maeneo mbalimbali.
..kuna madai ya wengine kutukuonekana kabisa, na waliobahatika kurudi majumbani kwao wamerudi wakiwa na majeraha au vilema.
..kuna tukio la mbunge mmoja wa kusini kumpeleka mhanga wa operation iliyofanyika kusini kwa waziri mkuu, na inasemekana waziri mkuu alisikitishwa na hali ya mwananchi huyo.
Cc
Mmawia ,
tindo