Mkuu 'Erythrocyte', unauelewa barabara msimamo wangu kuhusu Katiba Mpya na mambo mengine yote, kwa sababu wewe na mimi tumetoka mbali kwa pamoja.
Kwa hiyo, najuwa ninaposema kitu humu, huna mashaka yoyote juu ya msimamo wangu tokea mwanzo hadi sasa. Mimi siyo mtu ninayeyumba tu, bila ya sababu maalum, tena sababu yenyewe ihusike na maslahi ya nchi.
Sasa, kuhusu hili la Katiba Mpya, usidhani kuna chochote kilichobadilika katika msimamo wangu, ila, kutokana na sababu na mtego aliowawekea CHADEMA, kuhusu "maridhiano", Samia kishafanikiwa sana kuiondoa hiyo ajenda ya Katiba Mpya kuwa ni namba moja kaboisa, kwa sababu muda wa kutengeneza Katiba kabla ya uchaguzi mkuu, muda huo haupo, kama hapatakuwepo na kusogeza uchaguzi mbele. This is a fact, mtake au msitake.
Huwezi kwenda haraka haraka sasa hivi na kuchukua Rasmu ya Warioba na kutengeneza Katiba Mpya, na bado pakawepo na muda wa kujiandaa na uchaguzi. Hii kazi ya kuandika katiba haiwezi kufanywa iwe ya dharura.
Kwa hiyo, kwa maana hiyo sasa, CHADEMA inawapasa kutafuta njia za kuhakikisha mambo yote yanayoharibu uchaguzi yanatafutiwa njia za kuhakikisha kuwa uchafuzi huo hautokei wakati wa uchaguzi.
Na kama CCM wanang'ang'ania kuendelea na njia hizo, basi, hapo CHADEMA itawalazimu kutangaza wazi kwamba HAWATASHIRIKI kwenye uchaguzi huo, na muhimu zaidi, kwamba huo UHAGUZI HAUTAFANYIKA.
Huu ndio mstari ambao CHADEMA inahitaji kuujengea hoja wakati huu, pasiwepo tena na sintofahamu toka sehemu nyingine yoyote.