Pre GE2025 Tundu Lissu: Bilioni 54 za kununua pikipiki "SSH 2025" zimetoka wapi?

Pre GE2025 Tundu Lissu: Bilioni 54 za kununua pikipiki "SSH 2025" zimetoka wapi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Serikali kukaa kimya na kumuacha huyu bwana kudanganya umma ni kama,haileti afya kwa nchi yetu,

Huyu jamaa asili yake ni uongo,na ni mchonganishi mkubwa sana,hafai hata kupewa uenyekiti wa kitongoji. watanzania tuamke tukatae wanasiasa wa jamii ya Lissu wanahatarisha usalama wa nchi yetu.

Nimengalia bei yapikipiki kwenye mtandao wa alibaba ,pikipiki moja mpya inauzwa kuanzia shilingi 700,000 hadi sh 1,000,000 kwa boxer mpya,sasa yeye lissu anasema pikipiki moja ni sh 3,000'000 huu ni uongo,na kwa bei hii nchini China ya 700,000 kuna uwezekano wa kupunguziwa bei kutokana na mzigo kuwa mkubwa hivyo pikipiki moja ikauzwa kwa sh 500,000 mara 18,200 sawa sawa nabilioni 9 tu

Sasa huyu yeye hiyo bei ya 54 B kaitoa wapi,kweli hata mimi nitake mzigo wote huo wa pikipiki 18,200 ninunue nchini wakati ukiagiza china bei ni nafuu mara dufu


Watanzania tuamke na tuwakatae mapema sana hawa watu wanaotuchinganisha kwa masrahi yao wenyewe
Tuseme ni kweli ni 9B,kaitoa wapi huko wakati hatuna maji?
 
sure,
macho yamevimba maana jukwaa lilinivutia zaidi kulitazama kutoka simiyu nilipo dah, halafu mic zilikua zinamsmbua sana kazi sana aise:pedroP:
Utajua yote tu.Hawana bilioni 54 za kuiba wajenge majukwaa ya muda.Bali wana mema na mafundisho ya kuwakomboa wananchi.
 
Usidanganyike...!

Hizo fedha za vyanzo vyao vya mapato zote huishia kwenye mifuko binafsi ya watu..!!

Na ofcoz wana bilioni kama 2 au 3 hivi za ruzuku kila mwezi...

Sasa hizo bilioni 3 hata ukizidisha kwa mwaka mzima hawawezi kufikisha bilion 54..

Na kumbuka CCM ni chama kikubwa. Ndani ya pesa zao hizo za ruzuku na projects za ni lazima zitumike kwenye;

=Gharama za uendeshaji chama zikiwemo operesheni mbalimbali za chama chao,

=Kulipa mishahara ya watumishi wao,

=Maintainince cost nk nk

Swali linabaki palepale huyu katoa wapi pesa zote hizi za mkupuo mmoja wa kulipia pikipiki karibu 20,000 na kuzigawa nchi nzima?????????

Huyu mama ni mwizi na ni fisadi, hakuna kupepesa macho wa kujiumauma!!
wacha nikuongezee kidogo,

yaani unazungumzia vipikipiki elf20 pekee?

sasa hiyo ni nini kwa ccm, kama chadema waliingiza pickup za m4c zaid ya 100 kwa mara moja bila ruzuku na haijulika ziko wap mpaka sasa hata moja:pedroP::pedroP:

sikiliza ilo hivi,
bodaboda, bajaji, mipira na jezi za michezo za ccm, tracks & jackets, t shirts, kofia, fulana, vitenge, kanga, skafu, beji, medali n.k ni sehemu kidogo sana ya ruzuku ya chama cha mapindizi....

lakini bado, kuna kalamu za risasi za kisasa, notebooks, daftari, mav8 kama yote 0km ambayo nayo ni sehemu kidunchu sana ya ruzuku ya chama cha mapinduzi ....:pulpTRAVOLTA:

nimesema sana kwa wenzako, narudia tena kwako, gentleman,
uchaguzi ni process, uchaguzi ni plan na strategies ambayo ni very expensive acha mchezo aise:pulpTRAVOLTA:

ushindi wa kishindo is not a joke, it is real actions, acheni utani bana....

, et mtu anakuja from no where, ng"weng"weng"we nataka niwe raisi wa TZ, unachekesha wew:pedroP:
 
Usiwe unakariri yote uliyoambiwa shule ya vidudu kwamba kila nchi ya Ulaya iwe magharibi tu.Tafuta uhalisia.
inabidi ufungue uzi tupate revision kidogo,

kwahiyo yale mabwenyenye ni ya upande gani yanayomrubuni na kumshika akili kamanda wetu ambae alikua mzalendo mzuri tu anaeaminika singida :pedroP:
 
Kuhusu kampeni kuanza mapema ni kawaida ccm kuanza ligi hiyo kabla ya wakati. Kuna wale wapinzani laini bado wamelala usingizi wa pono halafu wanataka walau waambulie jimbo moja. Chadema waendelee na uzi wao waunganishe na kampeni hapohapo.
 
Kuhusu kampeni kuanza mapema ni kawaida ccm kuanza ligi hiyo kabla ya wakati. Kuna wale wapinzani laini bado wamelala usingizi wa pono halafu wanataka walau waambulie jimbo moja. Chadema waendelee na uzi wao waunganishe na kampeni hapohapo.
ccm wakifanya mikutano yao ya hadhara ni kampeni, upinzani wakifanya mikutano yao iliyododa, hiyo sio kampeni ni uhuru na haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara....

daahh,
hii dunia ni mvinringo au duara :pedroP: :pedroP:
 

Pikipiki zimeandikwa SSH2025 na zina picha yake, hatujaanza kampeni, mama ameanza kampeni zaidi ya mwaka na nusu kabla ya uchaguzi. Kama ameanza yeye na sisi tuanze, amefungulia mlango.

Kila kata ya mkoa wa Singida imepewa pikipiki kulingana na idadi ya vijiji vyake, mkoa mzima wa Singida zimeletwa pikipiki 700, na Tanzania nzima kila mkoa kapeleka pikipiki 700, na Tanzania bara iko mikoa 26, hivyo fanya pikipiki 700*26 ni 18,200. Ukienda mjini kuafuta pikipiki moja inauzwa milioni 3 mpyaa. Zidisha pikipiki 18,200*3,000,000 ni shilingi bilioni 54,600,000,000.

Bilioni 54 katika nchi ambayo watoto wanakaa chini hawana madawati, mahospitali hayana madawa, hakuna maji ya kunywa, barabara ni mbovu ila kuna pikipiki za kugawa bure za Rais za Tsh. 54,600,000,000

Nyie mnajua maana sizungumzi vitu ambavyo hamvijui, Magufuli si alifanya kampeni, aligawa pikipiki? Kikwete si alifanya kampeni, aligawa pikipiki? Mkapa aligawa pikipiki?

Huyu anatuletea pikipiki, siyo za CCM, zingekuwa za CCM zingeandikwa Chagua CCM etc etc. Hizi zimeandikwa SSH2025, ni za kwake na siyo za Serikali.

Hizo hela amezitoa wapi huyo anayetaka tumuite mama? kumbuka ameuza bandari zetu kwa warabu, ameuza hifadhi ya misitu yetu hekta 9,900,000 kwa waarabu, kiwanja cha ndege cha KIA kauza kwa waarabu, kule umasaini kafukuza wamasai wamepelekwa Handeni ili auze kwa waarabu.

Hii bilioni 54 ametoa wapi kama siyo hii biashara haramu anayofanya na mali za nchi yetu? CCM tuambie huyu mwenyekiti wenu anayetaka tumuite mama ametoa wapi hizi pikipiki hizi 18,200. Ana hela wapi, ana biashara gani?

Mwalimu Nyerere kabla hajafa aliuza " Hivi Ikulu kuna Biashara gani" Samia Suluhu Hassan, Ikulu kuna biashara gani za kukupatia wewe Tsh 54,600,000,000 za kugawa pikipiki Tanzania nzima?


Pia soma: Kuelekea 2025 - Lissu: Wasijifiche nyuma ya msikiti, waje hadharani tuyaseme matendo yao maovu
Tutusa kama wewe huwezi kumuelewa Lissu kwa sababu nawe ni mnufaika wa hizo pikipiki za bure.
Umezoea vya bure hivyo huwezi kumwelewa.
 
Huwa mnalipwa bei gani kuhangaika kuzibeza na kuzikanusha hoja halali za wapinzani?

Kuna mTz yeyote asiyeelewa madudu ya Serikali anayoyaanika Lisu?

Shem on you!
acha upotoshaji basi gentleman,

kuana hoja wapi pale na wewe,
kama sio malalamiko yanayochochewa na mihemko isiyo na maana na ndio maana upuuzwaji wake ni wa kiwango cha juu sana....

kana namna ya kutoa na kuwasilisha hoja bana,
sio kubwekabweka tu, kupayukapayuka na kuropoka ropoka bila mpangilio. atakuskiza nani sasa kama sio kukupuuza tu :pulpTRAVOLTA: :pulpTRAVOLTA:
 
Hizi pikipiki itakuwa ni za waarabu wa dp world na wale wa loliondo waliowatoa wamasai kule na kwenda kuwajengea vijumba msomera. Hii hichi tusipokuwa wakali na rasimali za nchi hii kila taifa uarabuni, uchina, korea, ulaya na amerika wataona ni shamba la bibi watajipatia maeneo yao ya kujitochotea utajiri wa kujenga mataifa yao huku wananchi wakiangalia tu. Ni ukoloni mpya wa aina yake
 
ccm wakifanya mikutano yao ya hadhara ni kampeni, upinzani wakifanya mikutano yao iliyododa, hiyo sio kampeni ni uhuru na haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara....

daahh,
hii dunia ni mvinringo au duara :pedroP: :pedroP:
wapi mikutano ya wapinzani imedoda? Ya ccm ndio hudoda, huhudhuriwa na wanachama wake tu tena kwa kuhamsishana watoke kwa wingi
 
wapi mikutano ya wapinzani imedoda? Ya ccm ndio hudoda, huhudhuriwa na wanachama wake tu tena kwa kuhamsishana watoke kwa wingi
ziliaanza jorgingi zikadoda saivi, mikutano inachekesha na kutia huruma..

yaan, eti mkutano unaendelea hapa, tena ni mtua anaetamani kua rais, lakin wengine wanaendelea kucheza mpira wao tu kama vile hakuna kitu kinaendelea pembezoni mwao:pedroP:

kiongozi amekua sio kivutio tena, dah,

wananchi bana wanajua sana mambo haya, sijui wanaogopa mikutano yake kwasababu anaweza kuomba wamchangie tena :pedroP: :pedroP:
 
acha upotoshaji basi gentleman,

kuana hoja wapi pale na wewe,
kama sio malalamiko yanayochochewa na mihemko isiyo na maana na ndio maana upuuzwaji wake ni wa kiwango cha juu sana....

kana namna ya kutoa na kuwasilisha hoja bana,
sio kubwekabweka tu, kupayukapayuka na kuropoka ropoka bila mpangilio. atakuskiza nani sasa kama sio kukupuuza tu :pulpTRAVOLTA: :pulpTRAVOLTA:
Wewe unaishi jamii gani?

Tz nzima inauguza vidonda vya sukari na ufisadi mwingine wa wazi serikali imefanya, mwenzetu upo mkubwabwaja tu.

Kwa akili za hivi, ndiyo maana mwarabu kukamata watumwa hakuhangaika.
 
Wewe unaishi jamii gani?

Tz nzima inauguza vidonda vya sukari na ufisadi mwingine wa wazi serikali imefanya, mwenzetu upo mkubwabwaja tu.

Kwa akili za hivi, ndiyo maana mwarabu kukamata watumwa hakuhangaika.
naona yaleyale tu ya kupuuzwa nawe uko sambamba nayo :BRUHMM:
 
Back
Top Bottom