Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Lengo la mdahalo ni nini?
Kama ni utendaji wote tunajua kwa sasa JPM hana mpinzan
Ili juelewa lazima ujue maana ya mdaharo na umuhimu wake. Pia mmekuwa mkisika kwamba magu anapita kwenye nyayo za nyerere. Mwalimu nyerere aliamini sana katika MIDAHARO. Huyu mnayesema anafuata nyayo zake kwanini mnatumia nguvu kupinga mdaharo

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Kajifunze kwanza kiswahili
 
Lengo la mdahalo ni ku assess uwezo wa kujieleza na kuelezea mipango yake. Uwezo wa JPM tumeuona kwa vitendo hakuna haja ya blablaa. Mwambien Lissu afanye mdahalo na Rungwe na Membe ndio wa level yake
Una haki ya kutoa maoni yako pia, lakini Jiwe anaogopa nini kuhusu mdahalo? Kama tatizo ni lugha kaambiwa achague ambayo atakuwa comfortable hata kama ni kisukuma.
 
Lengo la mdahalo ni ku assess uwezo wa kujieleza na kuelezea mipango yake. Uwezo wa JPM tumeuona kwa vitendo hakuna haja ya blablaa. Mwambien Lissu afanye mdahalo na Rungwe na Membe ndio wa level yake
Asingefanya kampeni pia kama tukisimamia hoja yako.
 
Anaposema mdahalo kwa lugha yeyote anakusudia nini maana lugha ambayo watanzania wengi huizungumza ni kiswahili tu au wanataka kutumia lugha za makabila kufanyia mdahalo?

Kama ni kiingereza basi Lissu anatakiwa ajue kuwa si Jiwe tu ambae anaona hajui kiingereza bali watanzania wengi kiingereza kwao ni shida,hata leo akisema atumie hicho kiingereza kwenye kampeni zake basi watanzania wengi hawatomuelewa. Kwahiyo Lissu lazima ajue kuwa kitendo cha yeye tu kuona fahali kuweza kuongea kiingereza ni ishara kuwa eneo alipo watu wengi hawakijui hicho kiingereza na ndio maana yeye akaona ni fahali kujua hicho kiingereza ambacho wengine wengi hawajui.
 
Anaomba mdahalo kwa mtu ambaye kila kukicha anamtukana, kumkejeli na kumdharau anatarajia atakubaliwa???? Waswahili wananena kuwa 'Kimya Kina Mshindo'
 
Midahalo aliyofanya huko BBC, US, Ubelgiji na Kenya haijamtosha kujitangaza na kuwaridhisha wafadhili wake kwamba yuko kwenye kampeni na kinyang'anyiro cha urais Tanzania? Au hilo ni sharti jipya kapewa na akina Amsterdam? Basi halitakamilika. Hapati nafasi hiyo, aombe wafadhili wake wampee sharti jingine.
 
Hoja nyingine nzito hiyo!
Kweli CCM lazima akimbie mdahalo.
tatizo la JIWE wanaccm wanalijua.. hawezi kusimama hata dkk 1 kuongea yanayotuhusu kwa ufasaha akaeleweka. ATAWAAIBISHA ndo mana wanakwepa MDAHALO ila tutammburuza tu kwalazima ae aongee atueleae kwanini amefukuza wafanyakazi anaosema ni vihiyo na mwishoe kawazulumu mafao yao ya kuachishwa kazi. na hela zote KAMEZA.
 
Aende UDSM huko ndio kwenye midahalo na watu wanapimana kwa uwezo wao wa kuzungumza Kienglish. Sisi hapa ni KAZI TU. Angoje atakaporudi Ughaibuni atapata PAID MIDAHALO huko!
 
Wananchi wanataka sera zinazo telelezeka sio mdahalo,
Sera za majukuani ni zaidi ya mdahalo
 
Hawaelewagi wale!
Ndo maana hadi leo hawaelewi risasi 16 zilivotokea kushoto na kukata kona kuupiga mguu wa kulia wa Lisu bila kumgusa dereva wake.
 
Na kwanini huo Madahalo uwe lazima awepo Magufuli tu mbona Mama Anna Mghwila kipindi kile yupo Act wengine tulimuelewa pasina kuwepo Magufuli?
 
Lissu atangaze sera zake ataeleweka hii ya kutaka akubalike kwa mgongo wa Magufuli wengi tumeistukia. Kila mmoja ashinde mechi zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…