Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Really?!!

Hii si fake ID?!!!

Mmh....Hapana aisee wamemdukua....

Haya yalikuwa mawazo yake huyu bwana kabla ya kuuza utu wake!!!!Pole pole hakuna fake ID hapo.! Ukweli mtupu kuwa mnakwepa midahalo kwa kutumia ujanja ujanja tu. Mgombea wa kwanza na wa mwisho wa CCm kushiriki mdahalo wa wagobea URAIS ni marehemu Ben Mkapa; Jakaya ndio kabisa alisepa na inaelekea JIWE atasepa pia kwani hajiamini!!!
 
Oktoba 2010

Ana kwa ana na Mgombea Urais wa CCM Jakaya Kikwete.


Mgombea Jakaya Mrisho Kikwete wa Chama tawala CCM akijibu maswali na akijieleza kwa watanzania na wanahabari kupitia vyombo vya habari mwaka 2010 kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2010.
 
Lengo la mdahalo ni nini?

Kama ni utendaji wote tunajua kwa sasa JPM hana mpinzan
Hana mpinzani? Kwa nini afanye kampeini tena kwa kulialia. Mara hamnipendi, mngenipenda mngenipitisha bila kupingwa. Mara watangulizi wangu wamepewa miaka 10 kwa nini nami nisipewe bajameni? Alale asubiri kuapishwa 28 Oktoba.
 
Mbona wagombea wako wengi tu, kwanini iwe ni John tu.
Kuna Membe, Rungwe n.k anaweza fanya nao mdahalo pia.
Ligi kuu Tanzania bara VPL ina timu 18..lakini siku wakicheza Simba na Yanga kila Mtanzania atajuwa..GIANTS...Magufuri hawezi kushindana hoja na Lissu..fullstop
 
Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"
lissu ajikite katika kueleza atatufanyia nini zaidi ya Magufuli
Anataka kutumia mdahalo kujiongezea nguvu,tupo bize vijijini kusambaza sera
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Huyu jamaa anafikiri kushinda urais ni sawa na kutetea kesi za akina Mbowe pale kisutu!

Mwambie kura hazipo kwenye mdahalo ila zipo huko field..
Mkuu mdahalo ni sehemu ya hiyo field,sasa mnaogopa nini ndugu yenu hawezi kujieleza,wazungu wanasema,kama huwezi kuelezea yale uliyoyafanya you simply hukuyafanya
 
lissu ajikite katika kueleza atatufanyia nini zaidi ya Magufuli
Anataka kutumia mdahalo kujiongezea nguvu,tupo bize vijijini kusambaza sera
Sasa mdahalo si ni sehemu ya kuelezea hiyo mambo atakayo yafanya,tena unawaelezea watu wengi zaidi kwa wakati mmoja kuliko hata wanavyofanya kwenye majukwaa ya campaign?,ndugu zangu ninyi mna kwama wapi?
 
Sasa mdahalo si ni sehemu ya kuelezea hiyo mambo atakayo yafanya,tena unawaelezea watu wengi zaidi kwa wakati mmoja kuliko hata wanavyofanya kwenye majukwaa ya campaign?,ndugu zangu ninyi mna kwama wapi?
sisi tunawafuata watu walipo,mdahalo mnaweza fanya hata na hashim rungwe mtasikilizwa tu,hatutoi kiki
 
Naunga mkono, maana ni vizuri sana kuiga mambo ya US ambako mheshimiwa Lissu alipeleka malalamiko ya risasi zake. Mjadala uzungumzie elimu, uchumi, sayansi na teknolojia, na hapo Lissu jiandae vizuri maana usije ukaulizwa Laws of motion, wewe ukaishia kuzitafuta kwenye katiba ya nchi. Tutakupa kidogo na swali la kutafuta density, na tutakuwa tumeshafahamu nani ana kichwa cha kutuvusha.
 
Eti mdahalo na JPM..Hivi mna akili kweli.nyinyi...tangu lini baba akawa na mdahalo na mtoto...ambaye bado kinda anakua. .mdahalo labda akafanye na wazungu wake kule Ubelgiji.. Magufuli ni level nyingine jomba...eti DR. akadahalo na mtu ambaye hata Masters hana..Khaaaaa. ...swainnnnn nn. ..mtu hajawahi kuwa hata mtandaji wa kata..ubunge tu ulimshinda akatelekeza jimbo lake akakimbilia nje
 
sisi tunawafuata watu walipo,mdahalo mnaweza fanya hata na hashim rungwe mtasikilizwa tu,hatutoi kiki
Kwa sababu matumizi mabaya ya fedha za walipa Kodi wa nchi hii haijawahi kuwa issue kwa ccm,lakin pia kwa kuwa kazi yetu ni kueneza Uongo miongoni mwa watanzania then tukifanya mdahalo tunaweza umbuka
 
Kumbe ulikuwa hujui kwamba ivo ni vitu viwili tofauti......ikitokea vile vyoooooote ulivyofundishwa/karirishwa vikiondolewa kichwani, kitakachobaki ndio AKILI, aliyebuni mambo ya elimu yeye alikuwa ana AKILI sio ELIMU, sijui umenielewa mkuu John7371
Bado hujaelewa kuelimika ni nini basi;ukishaelewa maana yake nadhan kwa pamoja tutaelewana pasipo shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…