Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

..sasa wewe shutuma za kuwa walinzi waliondolewa area D umezichukuliaje?

..umeridhika na majibu ya serikali kuhusu shutuma hizo?

..umeridhika na jinsi jeshi la Polisi lilivyoshughulikia uchunguzi wa shambulizi lile?

Nimezichukulia kuwa ni shutuma ambazo hazina ushahidi.

Sidhani kama serikali ina cha kujibu kuhusu shutuma ambazo hazina ushahidi.

Pia uchunguzi hauwezi kuendelea kufanyika endapo dereva wa Tundu Lissu hataweza kuhojiwa na polisi na maelezo yae kuchukuliwa.
 
..wanawajua waliotaka kumuua Tundu Lissu.

..wangekuwa hawawajui wangewatafuta, maana kuna uwezekano wakashambulia na mwingine.

..lakini kwasababu wanawajua, na wanajua walitumwa kumuua Tundu Lissu na siyo mtu mwingine, basi ndio maana unaona wametulia tu.

Hapa bado waendelea kutoa shutuma ambazo huna ushahidi nazo.
 
Nimezichukulia kuwa ni shutuma ambazo hazina ushahidi.

Sidhani kama serikali ina cha kujibu kuhusu shutuma ambazo hazina ushahidi.

Pia uchunguzi hauwezi kuendelea kufanyika endapo dereva wa Tundu Lissu hataweza kuhojiwa na polisi na maelezo yae kuchukuliwa.

..hazina ushahidi kivipi wakati mhanga wa tukio hilo ndiyo aliyesema.

..yaani kwa akili yako unaamini mhanga wa tukio kama lile anaweza kudanganya?

..au unaweza kuamini mtu, au chombo kingine, zaidi ya victim mwenyewe?

..kama victim amesema walinzi wa getini, na kwenye nyumba za viongozi walikuwa hawapo, who is to dispute that?

..Na kama suala hilo ni disputable basi ilitakiwa wajitokeze hao walinzi na kueleza walikuwa wapi, au kama walikuwepo waeleze waliona nini.

NB:

..anayeweza kubishia na kukanusha kuhusu walinzi kuwepo au kutokuwepo ni magaidi waliotumwa kumuua.Kwasababu wauwaji, Tundu Lissu, na dereva, ndio waliopita getini kabla ya tukio.
 
Unaweza kuwa na familia inayoongea kiingereza wakati mwenyewe unababaisha ila mnaelewana kimawasiliano tu! Nimeshakutana na familia nyingi za aina ambayo mke anakuwa ni face ya familia kwa sababu mwanamme hajui lugha vizuri. Binafsi watoto wangu wote hawajui kiswahili sawaswa ingawa mke wangu ni mtanzania ambaye siyo kabila langu na wala sijui lugha yao lakini siwezi kutumia leverage ya watoto wangu au mke wangu kujua lugha zao. Mimi nazungumzia lugha ya kiingereza kwa sababu ya nature ya kazi yangu, siyo kwa sababu ya mazingira ya familia yangu.

Kama kazi hata na mimi nimeajiriwa na nawasiliana na watu kwa lugha ya Kiingereza.. Kwa ufupi hata na mimi nakijua vizuri sana. Mpumbavu kama wewe unataka kuwaaminisha watu kuwa Tundu Lissu na Magufuli wapo sawa kwenye lugha ya Kiingereza, siyo kweli.
 
Anatapatapa sasa ameshindwa kuwa win watz! Hatuhitajj mdahalo sisi bali tunataka utuambie umefanya nini na utafanya nini tukikupa kura zetu! Hatuko kwenye mashindano ya mdahalo!
Vijana wa ccm zero brain
 
Hiyo ilani ni kajitabu cha kitapeli tu.

Kama ilani haiwezi hata kuajiri watu, ujue humo ndani kumejaa unyang'anyi mtupu.

Hebu muacheni aje azungumze huenda tutamuelewa. Hizo ilani huwa sizielewi kabisa.
Comrade nimeshakuambia kuwa mdahalo hautakusaidia kitu. Nimekuwekea na baadhi ya mikakati kutoka kwenye ilani makini ya ccm uone kuhusu ajira inasema nini.
Screenshot_20200914-004106_Office.jpg
 
Ni
Huyu mgombea wetu hana adabu kabisa sijui kalelewa na mzazi mmoja? Wanachadema wenzangu nisaidieni kunielewesha juu ya mgombea wetu lissu, kwani mdahalo ndo utampa kura? Akafanye midahalo na Robert Amsterdam,
[/QUOTE)nimecheka sana umeongea kwa hasira kweli, Lissu anahitaji uwemvumilivu kweli n MTU anae kera na kuudhi Tanzania haijawahi kutana na mpinzani wa aina kama ya Lissu,wakati wengine wanamuogopa Magufuri yeye anamuweka ka mtani wake.Nafkiri njia pekee n kumuacha azungumze amalize kampeni kwani kushinda siorahisi
 


Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"

=====

LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

Mhe. Lissu amesema kuwa ushiriki wa midahalo kwa wagombea urais ni mojawapo ya kipimo muhimu kinachotumika kimataifa kujua uwezo wa wagombea urais na kwa hapa nchini, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu, Agosti 26, mwaka huu, haina shaka yoyote kuwa ushindani katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko kati ya Mgombea wa Chadema na Mgombea wa CCM, ambapo amesisitiza wito huo kwa kuviomba vyombo vya habari vikubwa hususan vituo vya luninga, kuandaa mdahalo huo.

“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake,” amesema Mhe. Lissu.

Aidha, Mhe. Lissu amesema Serikali atakayoiunda chini ya chama Chadema, itaondoa mara moja masharti ya kibaguzi na utaratibu mbovu wa kisheria unaotumika katika mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao umegeuka kuwa adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi na badala yake, kanuni pekee itakayosimamia upatikanaji wa mikopo hiyo ni uhitaji wa mhusika.

Akisisitiza hoja hiyo, Mhe. Lissu amesema kuwa mfumo wa urejeshaji riba ya mikopo hiyo unaotumika sasa nao pia uko kinyume na utaratibu wa kisheria uliokuwa mwongozo kwa wanafunzi na wazazi kuingia makubaliano ya kukopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB), ambapo Serikali imeingiza utaratibu mwingine kuwataka wanufaika kulipa riba ya asilimia 15 badala ya asilimia 3 ya awali, akiahidi kuwa Serikali ya Chadema itaufutilia mbali kwa sababu unawafilisi kiuchumi wanufaikaji wa mikopo hiyo.

Akihutubia mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake, uliofanyika leo katika Uwanja wa Mwembetogwa, Mhe. Lissu amesema mfumo unaotumika sasa umewekewa utaratibu ambao unawaumiza na kuwabagua wanafunzi na wazazzi hata wenye uhitaji wa mikopo hiyo ili waweze kujielimisha elimu ya juu kwa kadri ya uwezo wao.

Aidha, Mhe. Lissu akizungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote bila kubagua hali wala hadhi ya mtu, amesema kuwa kila mmoja katika wakati usiotarajiwa anaweza kuhitaji msaada wa kuhifadhiwa iwe kwa matibabu, ulemavu usiotarajiwa, umri wa uzeeni, kupoteza ajira au uhitaji wowote ule, hivyo Serikali atakayoiunda, akichaguliwa Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu utakaohakikisha kila Mtanzania anapata hifadhi kadri ya ya mahitaji, ikiwemo bima ya afya, badala ya sasa wanaohudumiwa walioko kwenye ajira rasmi pekee.

“Iringa ni mahali sahihi kabisa kuzungumzia agenda ya hali ya elimu yetu na hususan elimu ya juu. Kuna tatizo katika mfumo wetu wa utoaji elimu nchini. Mtakumbuka wakati ule nilipokuja wakati wa kutafuta udhamini nilizungumza hili. Tunapaswa kuubadili ili uweze kuwapatia watoto wetu maarifa na uwezo wa kufikiria kutatua matatizo yao na kuajiriwa mahali popote duniani. Kwa sababu hilo nililisema wakati ule na mlinielewa, leo nataka nizungumzie hili la elimu ya juu na hususan elimu ya juu, chuo kikuu. Wale wa makamo yangu wanajua kuwa wakati wetu elimu tuliyosoma ililipwa na umma wa Watanzania. Katika zama za CCM wanaita ya kisasa, ili motto wako asome Chuo Kikuu lazima umlipie au akopeshwe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mikopo hiyo na utaratibu wa utoaji wake na urejeshaji wake, imegeuka kuwa adha kubwa mno kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.

“Kumekuwa na masharti ya kibaguzi katika utoaji wa mikopo ya hiyo. Wanafunzi waliosoma shule za binafsi wamekuwa wakiambiwa hawastahili kupata mikopo. Wanafunzi wengine wengi wameshindwa kuendelea na masomo yao. Serikali ya Chadema, nitakayoiunda mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu unaohakikisha kila mtoto anastahili kupata mkopo bila kujali alisoma wapi. Kanuni pekee itakayotuongoza ni, je anahitaji mkopo? Tutahakikisha pia wanufaikaji wote wanatendewa haki kwa kurejea kwenye sheria ya mwanzo iliyokuwa inaelekeza makato ya riba ya asilimia 3 badala ya sasa ambapo imefanywa kuwa asilimia 15 hali inayowafilisi kiuchumi,” amesema Mhe. Lissu.

Akitumia mkutano huo pia kuomba kura zake na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Mkoa wa Iringa, Mhe. Lissu amezungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote, ambapo amesema kuwa mfumo uliopo sasa pamoja na kuwatenga watu wengine wasiokuwa kwenye ajira rasmi, pia umeshindwa kuwahudumia hata wahusika baada ya kutumiwa vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na tija kwa wachangiaji, ambapo amesema fedha nyingi zimefujwa kiasi cha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha na hatimae kufilisika.

Ameongeza kuwa tatizo la hifadhi ya jamii si uwingi au uchache wake, bali ni matumizi mabaya ya rasilimali zake, hivyo ameahidi kuwa Serikali atakayoiunda baada ya kuchaguliwa mwezi Oktoba, itahakikisha utaratibu mpya wa hifadhi ya jamii unawahusisha watu wote kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha inaendeshwa katika namna inayozingatia matumizi sahihi yenye tija kwa wahusika ambao watakuwa na uhuru wa kuamua.

“Tunazungumzia mfumo wa hifadhi ya jamii utakaoweza kuwahudumia watu wote, wastaafu wetu, wazee, wasiojiweza, bima ya afya. Tutahakikisha kila asiyejiweza anatunzwa na hifadhi ya jamii. Sisi wote hapa tutazeeka, tunaweza kuwa walemavu, tunaweza kupoteza ajira, tutaugua, tutahitaji kuhifadhiwa. Shida hapa kwetu si wingi wa mifuko, bali mifuko hiyo imefujwa. Walipoifilisi wakaleta masuala ya fao la kujitoa na ile kanuni mpya ya kikotoo, maana mifuko hiyo haina fedha tena,” amesema Mhe. Lissu.

Mhe. Lissu amesema kuwa utekelezaji wa mipango hiyo utahitaji vyanzo vya uhakika vya fedha, ambapo ametaja mapato yatakayotokana na uuzaji wa gesi asilia, ambayo uendelezaji wake ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne, ulioibainisha Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo, kabla haujatelekezwa katika awamu ya tano, itakuwa ni mojawapo ya vyanzo vya fedha ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu ya uhakika na Watanzania wote wanapewa haki ya hifadhi ya jamii.

Mhe. Lissu ametumia mikutano yake mitatu katika maeneo ya Migoli (Isimani), Ifunda (Kalenga) na Iringa mjini, kunadi agenda mbalimbali zilizomo katika Ilani ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inayozungumzia masuala yote katika muktadha wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Imetolewa leo, Jumapili, Septemba 13, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Jinsi ambavyo mikutano ya hadhara ina tumiwa vibaya na wagombea na jinsi ya kupata mwanga
 
Lissu kama kweli anataka mdahalo asubiri mgombea wa 2020 apatikane ndipo ajiandae.

Magufuli ni mtekelezaji wa ilani tangu 2015 hayupo katika hadhi sawa na Lissu kwa sasa.

Mwenye jukumu la kutekeleza malengo ya chama kwa vitendo hawezi kuwekwa jukwaa moja na yule mwenye ndoto za urais.
Kwa kuwa tupo utaona mwakani Kama Trump hatafanya mdahalo na pia tafuta uchaguzi uliopita wa Kenya uone kama Uhuru hakushiriki mdahalo na pia tembelea Israel Kama Letanyau hakushiriki midahalo!!!!! Ccm mnaogoa nini?huu ni uchaguzi wagombea wote Wana hadhi sawa,na kumbuka wote wameomba na kufata vigezo vya tume Kama wagombea wapya
 
Waswahili tunsema kikulacho ki-nguoni mwako. Jamaa hajafungua akili kuangalia kwa kina kujua ni nani aliyetaka kumuua. Yeye anaamini kuwa ni Magufuli tu ndiye aliyetaka kumuua bila kujua kuwa Magufuli kwa position yake kama rais alikuwa na njia nyingi sana za kumhandle. Kibaya ni kwamba, ile kurupuka ya kulaumu serikali ilivuruga sana nguvu za serikali kufuatilia jambo hilo. Tunasahau kuwa miaka ya nyuma kidogo Dr. Mwakyembe naye alikumbana na kadhia ya kufuatiliwa na baadaye kulishwa sumu.
Kwanini hamtaki wachunguzi binafsi Scotland yard walitaka kuchunguza bure bila malipo serikali ilikataa.na serikali imekaa kimya as nothing happened. Usitetee upumbavu hata kama unalipwa ujira.tafuta kazi ya kufanya upate hela halali
 
Mkuu THUBUTU huyo anayejiita MWENDAWAZIMU atokezee kwenye mdahalo. Lissu atamzika mzima mzima itakuwa ni aibu kubwa sana kwa MATAGA ndiyo sababu wamejawa na hofu kubwa kuhusu mdahalo.

haaaa haaa MATAGA mmechafukwa leo. Tatizo nini lugha? au maguvu bila point
 
Hongera sana Lissu hakika hizi ndizo sera ambazo sisi wanyonge wa nchi hii tunazihitaji. Asiyeelewa hapa hawezi elewa kamwe.

CCM mwacheni mgombea wenu ajitokeze kwenye mdahalo akapambane kwa hoja sio kusubiri Lissu ametoka mahali na yeye ndipo anajipeleka kupeleka visera uchwara vyake.

Mimi binafsi hata huwa simuelewi yule mzee anaongeaga nini aisee maana hana speech zenye mvuto wa kumsikiliza kabisa. Lakini kwa Lissu lazima utulize kichwa usikie nondo zinavyoingia mpaka unasema kweli huyu ndiye anastahili kumpa kura yangu.
 
Nina mashaka na uelewa wako aisee. Hivi huwa unajipa muda wa kusoma hata kilichoandikwa? Au wewe unakurupuka tu kucomment?

Mtu wa ajabu sana wewe!!!
 
Hilo karai lisilojielewa; haeleweki hata huwa anazungumza nini, yule hastahili kupangwa na Lissu hata kidogo.
 
Uuuwiiii! Kisu kimegonga kwenye mfupa!

Lissu anajua kukera aisee.
 
Kwa kuwa tupo utaona mwakani Kama Trump hatafanya mdahalo na pia tafuta uchaguzi uliopita wa Kenya uone kama Uhuru hakushiriki mdahalo na pia tembelea Israel Kama Letanyau hakushiriki midahalo!!!!! Ccm mnaogoa nini?huu ni uchaguzi wagombea wote Wana hadhi sawa,na kumbuka wote wameomba na kufata vigezo vya tume Kama wagombea wapya
Ukiwa rais mtendaji yale unayoyafanya ni mdahalo tosha.
 
Back
Top Bottom