Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Hao hawajakaa serikalini inatakiwa aliyeshika madaraka na kuaminisha watu juu ya hili na lile aje kwa miaka mingi ayathibitishe hayo kwenye mdahalo

Niliwahi kuomba picha za viwanda vinavyohubiriwa kujengwa nchi nzima na products zake hakuna lumumba aliyepost hizo picha luthibitisha

T2020JPM, Alumni wa kawe, vingi Lowassa=yehodaya, magonjwa matambuka mkuje. Mnaitwa huku!
 
Mwaka huu kazi ipo mgombea wa Chadema Tundu Lisu Baada ya kuishiwa sera mkutano wa kampeni azindua sera mpya ya kuomba mdahalo wa wagombea Uraisi ambao Television zote lazima zitangaze!!!

Tulisema kampeni ya Ugombea uraisi Sio lelemana sera tayari Lisu zimeshakauka kooni.
 
Mwaka huu kazi ipo mgombea wa Chadema Tundu Lisu Baada ya kuishiwa sera mkutano wa kampeni azindua sera mpya ya kuomba mdahalo wa wagombea Uraisi ambayo Television zote lazima zitangaze!!!

Tulisema kampeni ya Ugombea uraisi Sio lelemana sera tayari Lisu zimeshakauka
Hivi naachaje kumchagua Lissu wakati ana Sera ya kumsomesha hata mwanangu ambaye nimemsomesha private?

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambae anarudisha makato ya mikopo ya bodi ya mikopo kutoka asilimia 15 ya magufuli hadi asilimia 6?

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambaye ametoa Sera ya kunijali mimi mlioandika kodi na mfanyabiashara kwa kuniwekea mswada wa kunilinda mimi mlipa kodi ili TRA wasininyanyase?

Hivi na Haji kumchagua Tundu Lissu ambaye hataniwekea mipaka kwenye masoko ya kuuza mazao yangu niliyoyalima kwa jasho kubwa?

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu mwenye Sera ya kurudisha katiba mpya ya warioba itakayoweka misingi ya utawala bora na kuondoa matumizi mabaya ya madaraka?
 
Rais Magufuli endelea kuchapa kazi na kuwaletea maendeleo watanzania. Kampeni unazofanya ni kama kutimiza matakwa ya katiba ya JMT, unazunguka kufanya presentation ya mazuri ambayo umewafanyia watanzania...
Maendeleo gani unayasongelea?

ATCL?
Ukijiuluza kwa nini ATCL imehamishiwa kwenye Kasma ya Ikulu ambayo CAG haruhusiwi kukagua utagundua kuwa ununuzi wa madege hauna faida. Yamenunuliwa bila kufuata sheria ya PPRA ili kujipatia RUSHWA tu.

Juzi tarehe 11 jioni Bombardier ya Mwanza -DSM ya saa 10 ilikuwa na abiria 33. Just imagine hiyo ni ruti ya Mwanza kwa Bombardier. Kwa hiyo ma Airbus na Dreamliner ni LOSS tupu. Wananchi hawana hela hata za kusafiria hiyo ATCL.

FLYOVER?
Suala ni kipaumbele. Lipi lianze elimu na afya au daraja la juu la DSM? Ni vipi Mwananchi wa Kazuramimba au Nanjilinji anafaidika na hilo daraja la DSM wakati yeye hata barabara ya vumbi ya kusafirisha mazao yake haipo

Barabara?
Jili la barabara za lami hajaanza yeye. Alianza Benjamin Mkapa na Kikwete kaendeleza. Kama kuna mtu wa kumsifia kwa barabara ni Mkapa kwa kuanzisha Road Fund na TANROADS. Afanye kadri ya uwezo wake na wengine wataendeleza kama yeye alivyopokea.

SGR?
Cha ajabu nini hapa. Mjerumani mwaka 1890- 1915 alijenga Reli ya Kati na bado aliondolewa na Muingereza.

Nyerere alijenga TAZARA na akaachia madaraka. Acheni ushamba wa kuabudu matendo ya DIKTETA

STIGLER GORGE?
Huwezi ukaanzisha miradi ya nchi kwa mapenzi yako mwenyewe bila kuzingatia the economic viability zake ili tu kujitafutia cheap popularity. Unaweza ukamaliza kunenga Stigler Gorge electric dam lakini siyo lazima upate hizo 2100 MW
 
Tundu Lissu hajajitengenezea utaratibu mzuri wa kupewa "offer" ya mdahalo.

Midahalo ni "privilege" yaani upendeleo na si "right" au haki...
Do you think vyombo vya habari havitaki kufanya midahalo?
The problem is je pana watu watakubali ambao ni viongozi wa juu?!

Nadhani wengi wanaogopa kuumbuka kwasababu ndipo mahali pekee utaulizwa na kujibu huku mamilioni ya wananchi wakikutazama na kupima uelewa wako, yaani utajibu wewe kama wewe, shida ni kwamba viongozi wengi wa kiafrika wanaogopa kuumbuka sababu hakutakuwa na nafasi ya kuongopa.

if I'm not wrong Tido alitaka fanya wakati yupo TBC ila sijui ilikuwaje ikazimwa kimyakimya ile ishu, ila actually mdahalo ni jambo zuri na pia siku hiyo mara nyingi Nchi husika husimama kusikiliza wagombea wa ngazi za juu sababu ni kipimo cha hali ya juu.
 
Do you think vyombo vya habari havitaki kufanya midahalo? The problem is je pana watu watakubali ambao ni viongozi wa juu?!.
Nadhani wengi wanaogopa kuumbuka kwasababu ndipo mahali pekee utaulizwa na kujibu huku mamilioni ya wananchi wakikutazama na kupima uelewa wako, yaani utajibu wewe kama wewe, shida ni kwamba viongozi wengi wa kiafrika wanaogopa kuumbuka sababu hakutakuwa na nafasi ya kuongopa...
Hapa ndipo Magfuli anapoogopea. Zingatia uwezo wake kujieleza na kujenga hoja ni mdogo. Pale hakuna wa kumkalipia. Unajibu maswali ya mtabgazaji unajibu maswali ya Lissu kichwa tulivu.
 
Maendeleo gani unayasongelea?

ATCL?
Ukijiuluza kwa nini ATCL imehamishiwa kwenye Kasma ya Ikulu ambayo CAG haruhusiwi kukagua utagundua kuwa ununuzi wa madege hauna faida. Yamenunuliwa bila kufuata sheria ya PPRA ili kujipatia RUSHWA tu...
Acha kuongea porojo za kishamba,Atcl kuwekwa chini ya wakala wa ndege za serikali ndio kuwa haikaguliwi mahesabu na CAG? Au kuna mtu anakudanganya!

Unaponda flyovers na interchanges hujui hasara ya foleni kwa uchumi wa nchi. Foleni ilikuwa inasababisha watu kuchelewa kufanya shughuli zao na kupunguza mapato kwa taifa na wananchi. Kodi na mapato ambayo yanapatikana kwa watu kufanya shughuli zao kwa haraka na wakati zinawanufaisha hata hao wananchi wa Nanjilinji.

Ni ajabu kumsifia mjerumani eti alijenga reli,alafu unaponda Sgr. Kwani hujui mjerumani alijenga reli ili kubeba raw material kupeleka kwao na kuinyonya nchi yetu. Sisi tulifaidika nayo kwa kipi mjerunani akiwa mkoloni.

Sgr italiingizia mapato taifa na pia itawanufaisha wananchi kwa namna nyingi ambazo zipo wazi.

Ni aibu kubwa kubeza mradi kama JNHPP wakati unajua unafaida kubwa na utaleta manufaa makubwa ya kiuchumi. Hizo Mw 2100 kwa nini zisipatikane wakati turbines zina uwezo wa kuzalisha hicho kiwango? Acha kukariri siasa za kishamba.
 
Anatapatapa sasa ameshindwa kuwa win watz! Hatuhitajj mdahalo sisi bali tunataka utuambie umefanya nini na utafanya nini tukikupa kura zetu! Hatuko kwenye mashindano ya mdahalo!
Lisu baada ya kujaukiwa sera anataka kugeuza Ugombea uraisi kuwa secondary school English debate competition!!!! Kskumbuka debate za Iliboru alikosoma secondary
 
Ni mtu mjinga tu ndiye anaweza kukataa fursa ya kujieleza kupitia mdahalo.
wapiga kura wetu Wengi wakuu wanaotupa ushindi wa kishindo CCM hawana TV Wala Radio hatuuhitaji huo.mdahalo
 


Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"

=====

LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

Mhe. Lissu amesema kuwa ushiriki wa midahalo kwa wagombea urais ni mojawapo ya kipimo muhimu kinachotumika kimataifa kujua uwezo wa wagombea urais na kwa hapa nchini, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu, Agosti 26, mwaka huu, haina shaka yoyote kuwa ushindani katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko kati ya Mgombea wa Chadema na Mgombea wa CCM, ambapo amesisitiza wito huo kwa kuviomba vyombo vya habari vikubwa hususan vituo vya luninga, kuandaa mdahalo huo.

“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake,” amesema Mhe. Lissu.

Aidha, Mhe. Lissu amesema Serikali atakayoiunda chini ya chama Chadema, itaondoa mara moja masharti ya kibaguzi na utaratibu mbovu wa kisheria unaotumika katika mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao umegeuka kuwa adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi na badala yake, kanuni pekee itakayosimamia upatikanaji wa mikopo hiyo ni uhitaji wa mhusika.

Akisisitiza hoja hiyo, Mhe. Lissu amesema kuwa mfumo wa urejeshaji riba ya mikopo hiyo unaotumika sasa nao pia uko kinyume na utaratibu wa kisheria uliokuwa mwongozo kwa wanafunzi na wazazi kuingia makubaliano ya kukopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB), ambapo Serikali imeingiza utaratibu mwingine kuwataka wanufaika kulipa riba ya asilimia 15 badala ya asilimia 3 ya awali, akiahidi kuwa Serikali ya Chadema itaufutilia mbali kwa sababu unawafilisi kiuchumi wanufaikaji wa mikopo hiyo.

Akihutubia mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake, uliofanyika leo katika Uwanja wa Mwembetogwa, Mhe. Lissu amesema mfumo unaotumika sasa umewekewa utaratibu ambao unawaumiza na kuwabagua wanafunzi na wazazzi hata wenye uhitaji wa mikopo hiyo ili waweze kujielimisha elimu ya juu kwa kadri ya uwezo wao.

Aidha, Mhe. Lissu akizungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote bila kubagua hali wala hadhi ya mtu, amesema kuwa kila mmoja katika wakati usiotarajiwa anaweza kuhitaji msaada wa kuhifadhiwa iwe kwa matibabu, ulemavu usiotarajiwa, umri wa uzeeni, kupoteza ajira au uhitaji wowote ule, hivyo Serikali atakayoiunda, akichaguliwa Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu utakaohakikisha kila Mtanzania anapata hifadhi kadri ya ya mahitaji, ikiwemo bima ya afya, badala ya sasa wanaohudumiwa walioko kwenye ajira rasmi pekee.

“Iringa ni mahali sahihi kabisa kuzungumzia agenda ya hali ya elimu yetu na hususan elimu ya juu. Kuna tatizo katika mfumo wetu wa utoaji elimu nchini. Mtakumbuka wakati ule nilipokuja wakati wa kutafuta udhamini nilizungumza hili. Tunapaswa kuubadili ili uweze kuwapatia watoto wetu maarifa na uwezo wa kufikiria kutatua matatizo yao na kuajiriwa mahali popote duniani. Kwa sababu hilo nililisema wakati ule na mlinielewa, leo nataka nizungumzie hili la elimu ya juu na hususan elimu ya juu, chuo kikuu. Wale wa makamo yangu wanajua kuwa wakati wetu elimu tuliyosoma ililipwa na umma wa Watanzania. Katika zama za CCM wanaita ya kisasa, ili motto wako asome Chuo Kikuu lazima umlipie au akopeshwe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mikopo hiyo na utaratibu wa utoaji wake na urejeshaji wake, imegeuka kuwa adha kubwa mno kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.

“Kumekuwa na masharti ya kibaguzi katika utoaji wa mikopo ya hiyo. Wanafunzi waliosoma shule za binafsi wamekuwa wakiambiwa hawastahili kupata mikopo. Wanafunzi wengine wengi wameshindwa kuendelea na masomo yao. Serikali ya Chadema, nitakayoiunda mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu unaohakikisha kila mtoto anastahili kupata mkopo bila kujali alisoma wapi. Kanuni pekee itakayotuongoza ni, je anahitaji mkopo? Tutahakikisha pia wanufaikaji wote wanatendewa haki kwa kurejea kwenye sheria ya mwanzo iliyokuwa inaelekeza makato ya riba ya asilimia 3 badala ya sasa ambapo imefanywa kuwa asilimia 15 hali inayowafilisi kiuchumi,” amesema Mhe. Lissu.

Akitumia mkutano huo pia kuomba kura zake na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Mkoa wa Iringa, Mhe. Lissu amezungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote, ambapo amesema kuwa mfumo uliopo sasa pamoja na kuwatenga watu wengine wasiokuwa kwenye ajira rasmi, pia umeshindwa kuwahudumia hata wahusika baada ya kutumiwa vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na tija kwa wachangiaji, ambapo amesema fedha nyingi zimefujwa kiasi cha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha na hatimae kufilisika.

Ameongeza kuwa tatizo la hifadhi ya jamii si uwingi au uchache wake, bali ni matumizi mabaya ya rasilimali zake, hivyo ameahidi kuwa Serikali atakayoiunda baada ya kuchaguliwa mwezi Oktoba, itahakikisha utaratibu mpya wa hifadhi ya jamii unawahusisha watu wote kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha inaendeshwa katika namna inayozingatia matumizi sahihi yenye tija kwa wahusika ambao watakuwa na uhuru wa kuamua.

“Tunazungumzia mfumo wa hifadhi ya jamii utakaoweza kuwahudumia watu wote, wastaafu wetu, wazee, wasiojiweza, bima ya afya. Tutahakikisha kila asiyejiweza anatunzwa na hifadhi ya jamii. Sisi wote hapa tutazeeka, tunaweza kuwa walemavu, tunaweza kupoteza ajira, tutaugua, tutahitaji kuhifadhiwa. Shida hapa kwetu si wingi wa mifuko, bali mifuko hiyo imefujwa. Walipoifilisi wakaleta masuala ya fao la kujitoa na ile kanuni mpya ya kikotoo, maana mifuko hiyo haina fedha tena,” amesema Mhe. Lissu.

Mhe. Lissu amesema kuwa utekelezaji wa mipango hiyo utahitaji vyanzo vya uhakika vya fedha, ambapo ametaja mapato yatakayotokana na uuzaji wa gesi asilia, ambayo uendelezaji wake ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne, ulioibainisha Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo, kabla haujatelekezwa katika awamu ya tano, itakuwa ni mojawapo ya vyanzo vya fedha ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu ya uhakika na Watanzania wote wanapewa haki ya hifadhi ya jamii.

Mhe. Lissu ametumia mikutano yake mitatu katika maeneo ya Migoli (Isimani), Ifunda (Kalenga) na Iringa mjini, kunadi agenda mbalimbali zilizomo katika Ilani ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inayozungumzia masuala yote katika muktadha wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Imetolewa leo, Jumapili, Septemba 13, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Makeni this is the way kila mkutano uwe na summary namna hii safi sana
 
Lisu baada ya kujaukiwa sera anataka kugeuza Ugombea uraisi kuwa secondary school English debate competition!!!! Kskumbuka debate za Iliboru alikosoma secondary
Magufuli akiingia kwenye mdahalo atapata kifafa maana anajuwa ataulizwa aliko Ben Saanane Magufuli mwendesha serikali ya wauuaji
 
Yani Magufuli apoteze muda wake kwenda kujibu upupu wa Lissu anaowajaza viazi wenzake kwenye mikutano yake.

Surely Magu has better things to do.
 
Back
Top Bottom