Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Kujenga JNHPP ni kitu kimoja na kupata MW 2100 ni kitu kingine. Una commit leo USD 6,000 kwa umeme unaotokana na maji wakati una vyanzo vingine vya renewable energy kama gesi, upepo na geothermal. Ni udwanzi!
Kukaa kimya nalo ni jibu.
 

Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"

=====

LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi....
Ni ujinga kumkutanisha kwenye mdahalo MTU aliyechukua HKL na PCM,inafahamika wazi kuwa tobolisu ni muongeaji sana kutokana na kukalili sheria na historia wakati huyu mwingine ni mtu wa kutenda vitu vionekane na anachokituamia tobolisu ni kuaminisha watu kupitia kuongea kwake lakini si mtendaji kama anavyowaamisha watu, mfano mdogo ni ahadi alizotoa ni nyingi na zote zinaitaji pesa, ameahidi kufumua mifumo ifuatayo:TRA ,HABARI MAELEZO, ELIMU, KATIBA MPYA, MIFUKO YA JAMII, AFYA pia ameahidi kulipa fidia kwa waliondolewa kwa vyeti feki.

Waliobomolewa na kuamishwa kwa ajili ya ujenzi na ameahidi kupandisha mshahara kwa wafanyakazi, hapo ni miaka 05 bado miladi ya maendeleo ambayo yote inaitaji pesa na kutokana na kwamba hivyo vitu vyote vinaitaji pesa nyingi zaidi y tillioni 20. huyu MTU ni wa kumuogopa kama ukoma hafai bora Mara 10000 zimwi likujualo kuliko lisilokujua,
 
Anatapatapa sasa ameshindwa kuwa win watz! Hatuhitajj mdahalo sisi bali tunataka utuambie umefanya nini na utafanya nini tukikupa kura zetu! Hatuko kwenye mashindano ya mdahalo!
Jamaa kwani wewe umefanya nini
 
Tundu Lissu hajajitengenezea utaratibu mzuri wa kupewa "offer" ya mdahalo.

Midahalo ni "privilege" yaani upendeleo na si "right" au haki.

Isitoshe, midahalo huwa haiombwi au kushurutishwa na mgombea au wagombea

Hiyo ni kazi ya vyombo vya habari ambayo hufanywa baada ya kuridhishwa na sera walozisikia kutoka kwa kila mgombea wa vyama viwili vikuu.
Pia Mh Lissu anayo haki ya kuomba mdahalo na Jiwe, ila kama Jiwe anaogopa pia ana haki ya kukataa, kama lugha kwake ni tatizo amepewa uhuru wa kuchagua lugha yoyote ambayo yeye(Jiwe) atakuwa comfortable.
 
Hebu kaa utulie tafadhali.
Nitulie kivipi? Anasaini waziri ambae ni mbunge ndio wa kawaida atazuiwa kuipata kama anaihitaji? Uliza ni mkataba gani ambao bunge au mbunge akiutaka Serikali itakataa kuutoa.
 
Iwekwe sheria kwamba wagombea urais lazima washiriki kwenye mdahalo miongoni mwao. Hapa Magu hawezi kutokea kwenye mdahalo unaoombwa
 
Mbona wagombea wako wengi tu, kwanini iwe ni John tu.
Kuna Membe, Rungwe n.k anaweza fanya nao mdahalo pia.
Kweli hukui jibu ya hilo swali lako? [emoji848][emoji848][emoji848]
Kweli ccm wana wanachama wasiojua chochote
 
Lengo la mdahalo ni ku assess uwezo wa kujieleza na kuelezea mipango yake. Uwezo wa JPM tumeuona kwa vitendo hakuna haja ya blablaa. Mwambien Lissu afanye mdahalo na Rungwe na Membe ndio wa level yake
Unajua lengo la mdahalo wewe mataga? Kama hukui rudia kusoma tena
 
Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"

=====

LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi...

Huku ni kudhalilishana tu.
 
Nitulie kivipi? Anasaini waziri ambae ni mbunge ndio wa kawaida atazuiwa kuipata kama anaihitaji? Uliza ni mkataba gani ambao bunge au mbunge akiutaka Serikali itakataa kuutoa.

Narudia tena, hebu kaa kimya boss.
 
Lengo la mdahalo ni ku assess uwezo wa kujieleza na kuelezea mipango yake.
Uwezo wa JPM tumeuona kwa vitendo hakuna haja ya blablaa
Mwambien Lissu afanye mdahalo na Rungwe na Membe ndio wa level yake

Ni nadra sana mtu muovu kukubali kuhojiwa.
 
Hata Hayati Mwalimu Nyerere alikulia kijijini akichunga ng'ombe.

Baadae akatimkia shule na akaanza shule akiwa na miaka 12, na "upstairs" akawa si wa kawaida.

Huyohuyo umwonae mshamba leo hii kakuzidi akili, yeye ni raisi wa nchi.
Anayesema kuwa alisukumiziwa ndani au nani unamzungumzia?
 
Mimi ninaongea na kuandika kiingereza vizuri sana kuliko Lissu na Magufuli; ni matokeao ya nature ya kazi yangu ambapo nimekuwa mwalimu Marekani kwa takriban miaka 25 sasa. Je mimi ndiye ninafaa zaidi kuwa rais wa Tanzania? Nimemsikiliza Lissu anpoongea kiingereza jinsi anavyokosea na anatumia tabia ya kuweka pause kwa muda mrefu ili kurekebisha makosa hayo, na nimesikia Magufuli pia anapoongea kiingereza yeye anaongea kwa haraka katika lafudhi ya kisukuma na hivyo kufanya makosa ya matamashi fulani. Kati yao hakuna bingwa.
So tukusaidie nini ndugu Mwalimu wa Marekani?
 
Mkuu tuliza akili,utapasuka. Unashindana na jitu ambalo kundi kuuubwa la viongozi wako limemshindwa kwa hoja
Yaah!
Mfano hoja ya kuwalipa mabilioni ACACIA kwa kuzuia mchanga wetu bandarini. Hili jitu liliwagaragaza kabisa.
 
Back
Top Bottom