and delivered.Message sent!
...Ila Lisu angeanza na MUSIBA. amueleweshe ilikuwaje risasi 16 zilipigwa kutokea kushoto lakini mguu ulioumia ni wakulia na dereva wake asiguswe kabisa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
and delivered.Message sent!
lazima mkimbie muingie mitini mana hamna mtachoweza kuwaambia wananchiHuyo mjamaa amekulia porini afu anajiona lugha ya kingereza ni kijijini kwao
Kufanya mjadala na mropkaji wa matusi nani atakubali?
Aende ubeligiji akafanye mjadala na robert
vipi leo hukulala na mumeo mbona unatapika utopolo tuand delivered.
...Ila Lisu angeanza na MUSIBA. amueleweshe ilikuwaje risasi 16 zilipigwa kutokea kushoto lakini mguu ulioumia ni wakulia na dereva wake asiguswe kabisa?
Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"
=====
LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi...
Hakuna kosa ambalo litamgaharimu magufuli kama kukubali hiyo battle
Atamtuma MUSIBA msihofu.lazima mkimbie muingie mitini mana hamna mtachoweza kuwaambia wananchi
Kwa maoni yako Jiwe anatakiwa afanye mdahalo na nani?Hana hadhi ya kufanya mdahalo na number moja level yake ni wakina katambi, polepole etc
Duh!vipi leo hukulala na mumeo mbona unatapika utopolo tu
Duh!
makamanda mmejaa hoja za Tundu Lisu hadi raha.
Somo likieleweka hakuna maswali. Asante kwa kunielewaKukaa kimya nalo ni jibu.
Nikuelewe kwa upuuzi ulionadika, unacommit mradi wa umeme kwa Usd 6000 si upuuzi. Usd 6000 ni mradi wa JNHPP? Unakariri renewable energy, wakati Hep ni cheap na haina madhara kwa mazingira.Somo likieleweka hakuna maswali. Asante kwa kunielewa
Lissu hajui ‘budgeting limitations factors’ wala actual cost za bima yake kila mtu achangie shilling ngapi. Let alone nikisema jambo kama hilo linataka uanze na hospital service costing kwanza, aina ya magonjwa tuliyonayo, idadi ya watu wanaogua magonjwa mbali mbali kila mwaka, hospita stay, hospital bed capacity etc before you even think of insurance cover ya nchi nzima kila mtu achangie kiasi gani.Hauoni kwamba ndiyo wakati mzuri wa Magufuli kumchakaza kabisa Lissu? Kuna msemo unasema "Mtoto akililia wembe mpe umkate". Magufuli ni wembe na Lissu ni mtoto! Uwacheni wembe ukafanye kazi yake.
Ruhusuni mjadala.
Mwambie lisu hana sera kabaki kudandia dandia tu...hakuna kura za huruma hapa...
Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"
=====
LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.
Mhe. Lissu amesema kuwa ushiriki wa midahalo kwa wagombea urais ni mojawapo ya kipimo muhimu kinachotumika kimataifa kujua uwezo wa wagombea urais na kwa hapa nchini, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu, Agosti 26, mwaka huu, haina shaka yoyote kuwa ushindani katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko kati ya Mgombea wa Chadema na Mgombea wa CCM, ambapo amesisitiza wito huo kwa kuviomba vyombo vya habari vikubwa hususan vituo vya luninga, kuandaa mdahalo huo.
“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake,” amesema Mhe. Lissu.
Aidha, Mhe. Lissu amesema Serikali atakayoiunda chini ya chama Chadema, itaondoa mara moja masharti ya kibaguzi na utaratibu mbovu wa kisheria unaotumika katika mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao umegeuka kuwa adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi na badala yake, kanuni pekee itakayosimamia upatikanaji wa mikopo hiyo ni uhitaji wa mhusika.
Akisisitiza hoja hiyo, Mhe. Lissu amesema kuwa mfumo wa urejeshaji riba ya mikopo hiyo unaotumika sasa nao pia uko kinyume na utaratibu wa kisheria uliokuwa mwongozo kwa wanafunzi na wazazi kuingia makubaliano ya kukopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB), ambapo Serikali imeingiza utaratibu mwingine kuwataka wanufaika kulipa riba ya asilimia 15 badala ya asilimia 3 ya awali, akiahidi kuwa Serikali ya Chadema itaufutilia mbali kwa sababu unawafilisi kiuchumi wanufaikaji wa mikopo hiyo.
Akihutubia mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake, uliofanyika leo katika Uwanja wa Mwembetogwa, Mhe. Lissu amesema mfumo unaotumika sasa umewekewa utaratibu ambao unawaumiza na kuwabagua wanafunzi na wazazzi hata wenye uhitaji wa mikopo hiyo ili waweze kujielimisha elimu ya juu kwa kadri ya uwezo wao.
Aidha, Mhe. Lissu akizungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote bila kubagua hali wala hadhi ya mtu, amesema kuwa kila mmoja katika wakati usiotarajiwa anaweza kuhitaji msaada wa kuhifadhiwa iwe kwa matibabu, ulemavu usiotarajiwa, umri wa uzeeni, kupoteza ajira au uhitaji wowote ule, hivyo Serikali atakayoiunda, akichaguliwa Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu utakaohakikisha kila Mtanzania anapata hifadhi kadri ya ya mahitaji, ikiwemo bima ya afya, badala ya sasa wanaohudumiwa walioko kwenye ajira rasmi pekee.
“Iringa ni mahali sahihi kabisa kuzungumzia agenda ya hali ya elimu yetu na hususan elimu ya juu. Kuna tatizo katika mfumo wetu wa utoaji elimu nchini. Mtakumbuka wakati ule nilipokuja wakati wa kutafuta udhamini nilizungumza hili. Tunapaswa kuubadili ili uweze kuwapatia watoto wetu maarifa na uwezo wa kufikiria kutatua matatizo yao na kuajiriwa mahali popote duniani. Kwa sababu hilo nililisema wakati ule na mlinielewa, leo nataka nizungumzie hili la elimu ya juu na hususan elimu ya juu, chuo kikuu. Wale wa makamo yangu wanajua kuwa wakati wetu elimu tuliyosoma ililipwa na umma wa Watanzania. Katika zama za CCM wanaita ya kisasa, ili motto wako asome Chuo Kikuu lazima umlipie au akopeshwe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mikopo hiyo na utaratibu wa utoaji wake na urejeshaji wake, imegeuka kuwa adha kubwa mno kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.
“Kumekuwa na masharti ya kibaguzi katika utoaji wa mikopo ya hiyo. Wanafunzi waliosoma shule za binafsi wamekuwa wakiambiwa hawastahili kupata mikopo. Wanafunzi wengine wengi wameshindwa kuendelea na masomo yao. Serikali ya Chadema, nitakayoiunda mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu unaohakikisha kila mtoto anastahili kupata mkopo bila kujali alisoma wapi. Kanuni pekee itakayotuongoza ni, je anahitaji mkopo? Tutahakikisha pia wanufaikaji wote wanatendewa haki kwa kurejea kwenye sheria ya mwanzo iliyokuwa inaelekeza makato ya riba ya asilimia 3 badala ya sasa ambapo imefanywa kuwa asilimia 15 hali inayowafilisi kiuchumi,” amesema Mhe. Lissu.
Akitumia mkutano huo pia kuomba kura zake na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Mkoa wa Iringa, Mhe. Lissu amezungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote, ambapo amesema kuwa mfumo uliopo sasa pamoja na kuwatenga watu wengine wasiokuwa kwenye ajira rasmi, pia umeshindwa kuwahudumia hata wahusika baada ya kutumiwa vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na tija kwa wachangiaji, ambapo amesema fedha nyingi zimefujwa kiasi cha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha na hatimae kufilisika.
Ameongeza kuwa tatizo la hifadhi ya jamii si uwingi au uchache wake, bali ni matumizi mabaya ya rasilimali zake, hivyo ameahidi kuwa Serikali atakayoiunda baada ya kuchaguliwa mwezi Oktoba, itahakikisha utaratibu mpya wa hifadhi ya jamii unawahusisha watu wote kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha inaendeshwa katika namna inayozingatia matumizi sahihi yenye tija kwa wahusika ambao watakuwa na uhuru wa kuamua.
“Tunazungumzia mfumo wa hifadhi ya jamii utakaoweza kuwahudumia watu wote, wastaafu wetu, wazee, wasiojiweza, bima ya afya. Tutahakikisha kila asiyejiweza anatunzwa na hifadhi ya jamii. Sisi wote hapa tutazeeka, tunaweza kuwa walemavu, tunaweza kupoteza ajira, tutaugua, tutahitaji kuhifadhiwa. Shida hapa kwetu si wingi wa mifuko, bali mifuko hiyo imefujwa. Walipoifilisi wakaleta masuala ya fao la kujitoa na ile kanuni mpya ya kikotoo, maana mifuko hiyo haina fedha tena,” amesema Mhe. Lissu.
Mhe. Lissu amesema kuwa utekelezaji wa mipango hiyo utahitaji vyanzo vya uhakika vya fedha, ambapo ametaja mapato yatakayotokana na uuzaji wa gesi asilia, ambayo uendelezaji wake ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne, ulioibainisha Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo, kabla haujatelekezwa katika awamu ya tano, itakuwa ni mojawapo ya vyanzo vya fedha ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu ya uhakika na Watanzania wote wanapewa haki ya hifadhi ya jamii.
Mhe. Lissu ametumia mikutano yake mitatu katika maeneo ya Migoli (Isimani), Ifunda (Kalenga) na Iringa mjini, kunadi agenda mbalimbali zilizomo katika Ilani ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inayozungumzia masuala yote katika muktadha wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.
Imetolewa leo, Jumapili, Septemba 13, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Kuhusu budget limitation factors ni suala la priorities tu. Tumeanza na lipi na lipi linafuata!!Lissu hajui ‘budgeting limitations factors’ wala actual cost za bima yake kila mtu achangie shilling ngapi sidhani kama let alone nikisema jambo kila hilo linataka uanze na hospital service costing, aina ya magonjwa tuliyonayo, idadi ya hospital bed, etc before you even think of insurance cover ya nchi nzima kila mtu achangie kiasi gani.
Mtu anatopoka tu halafu anataka mdhahalo na raisi. Kukusaidia tu Lissu hana shida ya mdahalo kwa sababu ana hoja za msingi the bottom line kila mtu akiacha ushabiki wa siasa anachoongea Lissu ni upuuzi kuwahadaa wananchi wenye elimu ndogo.
Based on those facts kumpa mtu kama huyo mdhahalo sio kwamba unaenda jibizana nae kwa hoja zenye merit maana hana, bali kufanya ivyo ni ku entertain his mental issues; Tundu inabidi mumpe ukweli wake Magufuli ni raisi wa Tanzania na kwa katiba yetu he is very powerful aache kujiona yeye na Magufuli ni watu sawa.
Budgeting limiting factors inahusiana na vyanzo vya mapato, hili uweze kutumia lazima ujue source of your income. Uwezi toa lita kumi ya maziwa kwa ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa lita tano. Ukilazimisha utakumua damu na kuuwa ng’ombe mwenyewe.Kuhusu budget limitation factors ni suala la priorities tu. Tumeanza na lipi na lipi linafuata!!
Kwa mfano kwa nini utumie Bilions of TSHS kujenga kiwanja cha Chato kimachopokea ndege ya Museveni au Kenyatta once per year? Hizo fedha zingeelekezwa kwenye Afya.
Kwa nini nitumie Billions of TSHS kununua Dreamliners planes halafu ukazikodishe nje ya nchi? Bora ungeelekeza fedha hizo kwenye Afya au Elimu.
Asante, Jipya naona ni hicho mnachokihubiri wakati hamkiishi, please jibadilishe kwanza wewe Mengine yatafuata.wewe bora ungelala,huna jipya
Wewe umeona hilo tu. Ishu ya 15% kwa wadaiwa wa mikopo na hifadhi za jamii hujaona? Ishu ya mtakabari wa elimu nchini hujaona?Huyo mjamaa amekulia porini afu anajiona lugha ya kingereza ni kijijini kwao
Kufanya mjadala na mropkaji wa matusi nani atakubali?
Aende ubeligiji akafanye mjadala na robert
Dah....tatizo watz hatuhitaji Rais mwenye pereteperete nyingi.... tunahitaji Rais atakaye watetea wanyonge....atakayesimamia rasilimali zetu...atakayesimamia kama Rais...not a remote controlled one[/QUOTE]Hivi wanyonge ni watu gani? Ni vipi jiwe amewatetea hao wanyonge? Naomba majibu tafadhariTundu Lissu ameona nini kwa mpinzani wake mbona anakuwa hana huruma