Pre GE2025 Tundu Lissu: Chama hakitaokolewa na mtu ambaye ameshakiongoza kwa miaka 21. Namuokoa Mbowe asiwe 'Mugabe'

Pre GE2025 Tundu Lissu: Chama hakitaokolewa na mtu ambaye ameshakiongoza kwa miaka 21. Namuokoa Mbowe asiwe 'Mugabe'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu ameendelea kumkalia kooni Freeman Mbowe, safari hii ameiambia BBC anataka kumuokoa Mbowe asitoke kwenye chama kwa aibu kama Mugabe.
---
Chama hakiwezi kuokolewa na mtu aliyekiongoza kwa miaka 21"

Mgombea nafasi ya Uenyekiti Chadema Tundu Lissu amesema hatua yake ya kutaka uongozi wa chama hicho unalenga kulinda heshima ya kisiasa ya Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe.

Amesema hayo katika mahojiano maalum na Mwandishi wa BBC, Sammy Awami

Soma ~ Lissu: Mbowe alivyotoka gerezani alibadilika, akasema hawezi kutuambia kila kitu alichozungumza na Rais
Akakiokoe NCCR, asituchoshe.
 
Kunga'tuka ndio mdudu gani? Si amekubali mwende kwenye sanduku la kura, wasiwasi wako ni nini?
Kama kwenye uenyekiti tu hataki kung'atuka , akiwa raisi si ndio atafia madarakani
 
Bado siamini kama CHADEMA itatoka salama kwenye hii civil war. Haijalishi mshindi ni nani.
Pona ya CHADEMA iko kwa Mbowe. Kwamba aache Demokrasia ichukuwe mkondo na iwapo atashindwa akubali matokeo. Lisu naye akishondwa akubali matokeo lakini uchaguzi uwe wa huru na Haki ili watoe somo kwa CCM. Vinginevyo wasahau kuungwa mkono na wananchi.
 
Napenda apewe ili atofautishe theory and practical on knowing things!!

Mambo mengi anayoyaongea sivyo yalivyo apewe akajionee
Wewe unamwonaje Tundu Lissu..?

Ni sawa na Lipumba? John Cheyo?

Kwanini unafikiri CCM hawapendi kuona huyu mwamba anakuwa kiongozi wa CHADEMA, chama ambacho ni hasimu na mkosoaji mkubwa wa CCM na serikali yake..?

Jibu rahisi tu ni kuwa, Tundu Lissu akiwa Mwenyekiti CHADEMA, Samia Suluhu Hassan, CCM yake na serikali ya CCM kwa ujumla wanakuwa wamepigwa bao kubwa la ushindi kwa sababu watakuwa wameshindwa kuweka KIBARAKA WAO...!

Hiyo ☝🏻☝🏻☝🏻ndiyo central point ya mtanange huu unaoendelea kati ya pande hizi mbili...
 
Mbowe sijui anatumia nini Kufikiria kwa sababu kuhuduma for 20 yrs bado unataka nafasi hio inaonesha ni kiasi gani uko na Ulafi wa madarala, Kwanini usipishe Sura na mawazo mapya ?
 
Sasa huyu siri za chama si zitakua sio siri tena ila huyu jamaa anajua sana kubishana mahakaman ni sehem sahihi sana kwake
Siri Gani za chama mkuu? Hayo mambo ya masiri ndo yameifikisha nchi hapa ilipo chini ya maccm
 
Lissu ameendelea kumkalia kooni Freeman Mbowe, safari hii ameiambia BBC anataka kumuokoa Mbowe asitoke kwenye chama kwa aibu kama Mugabe.
---
Chama hakiwezi kuokolewa na mtu aliyekiongoza kwa miaka 21"

Mgombea nafasi ya Uenyekiti Chadema Tundu Lissu amesema hatua yake ya kutaka uongozi wa chama hicho unalenga kulinda heshima ya kisiasa ya Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe.

Amesema hayo katika mahojiano maalum na Mwandishi wa BBC, Sammy Awami

Soma ~ Lissu: Mbowe alivyotoka gerezani alibadilika, akasema hawezi kutuambia kila kitu alichozungumza na Rais
Point
 
Back
Top Bottom