Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Demokrasia gani ya kutukana watu...??
Weka hapa matusi aliyotukana. Kwa hapa Tanzania mtu akiambiwa ukweli kile alichokifanya mnaita matusi. Mfano akisema rasimali asilia za Tanganyika haziwezi kuuzwa na Wazanzibar. Kwa Tanzania mnaweza kuita matusi.
Ona Kenya Raila anavyompa vipande Luto. Mpaka anamwambia mjinga,lakini ndio hivyo siasa,wanasonga
 
Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!

Rais anayesaini mikataba ya hovyo kuliko hata wa Chifu Mangungo; anayegawa bandari zetu zote na nia za usafirishaji kisirisiri kwa wageni; anayelazimisha Bunge kubariki uharamia huo, na anayenyang'anya watu wetu ardhi zao na kuwapa wageni, anastahili kukosolewa kwa staha gani?

Tundu Lissu
Julai 18, 2023

View attachment 2692285
Barua ya wito wa Polisi

====

Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
Huyu kingai mwenye elimu ya mpwayungu alishindwa kujibu maswali ya kibatala,mpka kubanwa na haja kubwa...kwa lissu atajipupulia puuu
 
Huu mwenge unatakiwa itupwe mbali ndio inafanya Watanzania watawaliwe na mazuzu..usikute ndio kimbola tunapigwa watanzani tunakosa umoja wa kusimamia mambo yetu.
ati mwenge ni...kha mwenge ni kimbola uishi sana mkuu kwa comment hii 🤣😂
 
Huu mwenge unatakiwa itupwe mbali ndio inafanya Watanzania watawaliwe na mazuzu..usikute ndio kimbola tunapigwa watanzani tunakosa umoja wa kusimamia mambo yetu.
Huo ndio mtaji WA CCM siku utakapotupwa baharini ndio siku watanzania watakuwa na ujasiri kama wakenya. But ule. Moshi ukiendelea kuzungushwa kila MWAKA tutabaki mandondocha kila siku. Ndio tambiko LA chichim na shetani dhidi ya watz
 
Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!

Rais anayesaini mikataba ya hovyo kuliko hata wa Chifu Mangungo; anayegawa bandari zetu zote na nia za usafirishaji kisirisiri kwa wageni; anayelazimisha Bunge kubariki uharamia huo, na anayenyang'anya watu wetu ardhi zao na kuwapa wageni, anastahili kukosolewa kwa staha gani?

Tundu Lissu
Julai 18, 2023

View attachment 2692285
Barua ya wito wa Polisi

====

Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
Safi sana, haya majitu kupatia uhuru uliopitiliza haina maana kwa maana wanshindwa kabisa kujizuia aisee
 
"Utu na heshima ya Rais Samia" itatokana na matendo ya uongozi wake. Kama matendo yake hayaendani na matakwa ya wananchi anaowaongoza, asitegemee kupewa hiyo heshima inayohimizwa..

Maajabu ya nchi yetu ndiyo haya. Mtu anatumia cheo chake kufanya ujambazi kwa watu wake, badala ya kumshutumu na kumtaka aachie ngazi, kuna watu bado wanataka jambazi huyo apewe heshima?

Samia wakati huu angetakiwa kuwa jela badala ya kudai apewe heshima.

Heshima haidaiwi, inatolewa tu kwa mtu yeyote kutokana na matendo yake katika jamii anayoishi
Yaani wasio na HATIA washtakiwe ilhali majambazi yanapewa ulinzi.

Duniani Kuna mambo!!!
 
Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya jinai imemtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Mughwai Lissu kufika kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai makao makuu Dar es Salaam kwa kosa la kutoa maneno yasiyo na staha kumjibu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa kupitia barua ya Ofisi hiyo kwa Lissu ikibainisha kuwa Ofisi inafanya uchunguzi kuhusiana na maneno ambayo Lissu aliyatumia ambayo hayana staha kumjibu Mh. Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia tarehe 15/07/2023.

“Ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam siku ya alhamisi tarehe 20 Julai, 2023 saa 3:00 kamili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.” imesema barua hiyo.
View attachment 2692545
Hii ndo shida ya kuongozwa na raisi mwenye akili ya kisoda ,nguvu nyingi zinatumika kuficha mapungufu yake
 
CDM jitafakarini kama ni sahihi kuridhiana na majizi ya CCCm!!!
 
"Utu na heshima ya Rais Samia" itatokana na matendo ya uongozi wake. Kama matendo yake hayaendani na matakwa ya wananchi anaowaongoza, asitegemee kupewa hiyo heshima inayohimizwa..

Maajabu ya nchi yetu ndiyo haya. Mtu anatumia cheo chake kufanya ujambazi kwa watu wake, badala ya kumshutumu na kumtaka aachie ngazi, kuna watu bado wanataka jambazi huyo apewe heshima?

Samia wakati huu angetakiwa kuwa jela badala ya kudai apewe heshima.

Heshima haidaiwi, inatolewa tu kwa mtu yeyote kutokana na matendo yake katika jamii anayoishi
Wanalazimisha tumeheshimu kiongozi mwenye akili ya kisoda na pia nguvu nyingi inatumika ili kuficha hayo madhaifu yake ,badala raisi ajisimamie ,machawa ndo wantumika kumkingia kifua,
 
TUACHE KUCHANGANYA KWA MIHEMKO YA KISIASA NA PROPAGANDA ZA KIJINGA KWENYE TAALUMA YA SHERIA. MFANO HALISI NI HUU HAPA
SABABU ZA KUKAMATWA WAKILI PETER MADELEKA

Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo. Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu ( Anti Money laundering Act).

Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na serikali ( Plea Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.

Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa mkurugenzi wa mashtaka.

Baadae alifungua kesi katika mahakama kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri Hilo.

Ndipo alifungua shauri hilo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano ( plea bargaining )zilifanyika sawa.

Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo mahakama ilisikiliza Hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.

Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

UPOTOSHAJI:

Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.

Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa.
Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.

Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.
Ndio kipindi hiki hiyo kesi imekumbukwa!?
 
Kama kiongozi ukiongea vitu vya kijinga na watu wakakuambia huo ulioongea ni upuuzi. Kuna shida gani? Kiongozi anapokusea na anakaza shingo, unataka wanaoongozwa wafanyaje?
Nguvu inayotumika kuficha mapungufu ya huyu mama ni kubwa mno ,machawa KAMA akina nape ndo watetezi wake
 
Ila mimi naamini kuna watu wanamhujumu mama katika sakata hili. Wamelianzisha ili ionekane mama ameshindwa kuongoza

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
Raisi kapanda ndege na konvoy ya watu 100 kwa kodi zetu kwa matakww yake bila kushirikisha hats wataalam wake ndo akija na huu uchafu ndo unasema kuna mtu anamhujumu rais jamani .kwa kifupi saa100 akili yake inatosha kisoda tu
 
Daah, hatar sana. Unajua si jambo la kawaida kuamua haraka hivi. Hata majirani wanatushangaa.

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom