CHADEMA CHUKUENI TAHADHARI ZA KUTOSHA HAPO CHATO……
Na Thadei Ole Mushi.
Gari la Matangazo Chadema Wilayani Chato limechomwa Moto. Nalaani kitendo hiki si cha kiungwana kabisa na kinaweza kuhatarisha Amani.
Kwa Chadema Chato si eneo salama sana kwenu hivyo mnavyokwenda mchukue Tahadhari zote. Nasikia kuna na Bajaji imekula Kiberiti jana huko huko Chato ilikuwa ipo kwenye matangazo na yenyewe.
Kama hatufahamu ni kwamba Ndugu zetu hawa bado wapo kwenye Maombolezo ya Mpendwa wao JPM. Wanajua mnawafanyia Siasa kusema mnaenda kwenye Kaburi la JPM…. Kulikuwa hakuna haja ya kufanya hivyo, mngeenda tu kufanya Mkutano Chato bila Kumtaja JPM.
Siasa za Kanda ya Ziwa hata kwa Chama Changu CCM huwa nasema lazima waheshimu sana jina la JPM kwenye kuomba kura. Chadema wanapaswa kukumbuka ugomvi wao na JPM na wachukue kila Tahadhari wawapo kwenye eneo hilo.
Wakati wana Chato na kanda ya Ziwa wanagaragara kumlilia Mpendwa wao Chadema walikuwa wakisema taifa limepata Ahueni kwa Magufuli kufariki.
Chato chama chao cha Siasa kwa miaka sita iliyopita kilikuwa ni JPM wala sio CCM au Chadema. Magufuli wakati anawapelekea maji, Barabara za Taa, Mbuga ya wanyama, kuwajengea miundombinu ya Afya, Uwanja wa Ndege nk Chadema mlikuwa hamtaki na Mliwatukana sana wana Chato.
Nilitahadharisha kabla na lilionekana mapema
hili. Bora Mbowe angeenda Mwenyewe kuliko Lisu…. Polisi watafuteni waliochoma ila angalieni hali ya Usalama huko yasije kutokea mambo mabaya zaidi. Ma RPC wa mikoa hii hali sio Shwari, Taarifa za Kiitelejensia zinaonyesha wazi kuwa hata wenye nia mbaya na Chadema wanaweza kujificha kwenye ugomvi wa Chadema na JPM. Tafsirini hili tukio na mchukue hatua accordingly.
Lakini pia kwenye Siasa kuna Mambo Mengi, huenda ni njia ya kuondoka Kanda ya Ziwa kwa Chadema waseme wametishiwa maisha. Wanaweza kufanya chochote kutafuta pia Political sympathy. Siasa za Nchi zimehamia kanda ya Ziwa.
Tafuteni watu wanaokubalika Chato mkayasuluhishe kwanza maisha yaendelee.
Ole Mushi
0712702602