Tundu Lissu hajawahi kunyamaza na hatonyamazishwa kamwe

Tundu Lissu hajawahi kunyamaza na hatonyamazishwa kamwe

A
Kama yeye ni mbabe, saa hizi yuko wapi? Hakuna mtu anayeweza kushindana na dola, hasa katika kipindi hiki. Hata kama una pembe ngumu namna gani ni lazima hizo pembe zitang'olewa na hatimaye utashika adabu tu.
Acha maneno ya kipuuzi, hakuna anyeshindana na dola, Mtu akiapa kulinda Katiba na Sheria ni lazima atimize, hataki akachunge ng,ombe wake ambao atawaswaga atakavyo.
 
"if freedom of speech is taken away then dumb & silent we may be led like sheep to slaughter"
-George Washington
 
Ataufyata tu. Hizo ni kelele za mfa maji.

Atatia akili tu na kuweza kujua nini tofauti ya sense na nonsense, siasa na harakati, kuhutubia na uchochezi.


Usalama wa wananchi hauwezi kuwekwa rehani kwa sababu ya mropokaji, mchu wa madaraka, mchumia tumbo na mtafuta kick.
 
Naomba hii iwe angalizo kwa wote wanaodhani wanaweza kumnyamazisha Tundu Lissu. Ukifuatilia tangu awamu ya 3 huyu mtu alikuwa mwiba halisi kwa uanika ukweli kuhusu wachimbaji waliozikwa kibabe huko kanda ya ziwa ili kupisha mwekezaji, Mh. Lyatonga Mrema na IGP Mahita wanalifahamu hili vizuri sana.

Pamoja na vitisho vyote Lissu hakuwahi kumpigia magoti mtu yeyote na mwisho wa siku ukweli ulikuja kubainika, Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wahanga wale, Amina.

Awamu ya nne ya Mh Profesa Kikwete makali ya Lissu ya kusimamia ukweli wote mnayafahamu, kuna wakati Dk Kikwete alinukuliwa akisema " NI HERI DR SLAA AENDE IKULU KULIKO TUNDU LISSU AINGIE BUNGENI " Dr slaa hakwenda ikulu lakini Tundu Lissu aliingia bungeni kwa kishindo.

Huyu mtu hanyamazishwi na wanadamu, atanyamaza pale tu Mungu atakapomtwaa kwa hiyari yake lakini si kwa hila za wanadamu wenye mwili na nyama.
Asante sana mkuu kwa kutukumbusha tulikotokea hadi siku ya leo na bado tunaendelea kushuhudia uimara na usmart wa lisu na tunamuombea kila la kheri aendelee kusimamia haki za watanzania
 
Mwaka huu atapigia kelele zake ukonga kwa wafungwa wenzie ila wafungwa watafaidika atakuwa anawaandikia rufaa wafungwa wenzake
Umekua hakimu mfawidhi,na hapohapo umekua jaji wa mahakama ya rufaa,na isitoshe hata katiba huijui nini kusoma katiba.Jazba hazitakiw kwenye masuala ya kitaalam mdau.Ona sasa jana kesi imeenda hadi saa 3 usiku nadhan kama wangekua na mawazo yako wangemlaza tu,
 
Hata waalimu wake wanamfahamu kuwa hanyamazi penye ukweli, badala ya kushindana naye wamtumie
 
Mwaka huu atapigia kelele zake ukonga kwa wafungwa wenzie ila wafungwa watafaidika atakuwa anawaandikia rufaa wafungwa wenzake
Hahahaa kama mmeanza kuandaa ndoo za vinyesi, hatakuja kubeba mtazubeba wenyewe...
 
Back
Top Bottom