..TL alitetea wavuvi wa Rufiji delta.
..akatetea wachimbaji wa bulyankulu waliouawa kinyama kwa kufukiwa ktk migodi yao.
..hakuishia hapo ametetea wananchi wa mikoa ya Mara na Geita wafaidike na madini yanayopatikana ktk maeneo yao.
..wakati huyu akijitoa na hata kuhatarisha usalama wake wabunge wa maeneo hayo walikaa kimya huku serikali ikiingia mikataba ya kifisadi.
..leo hii kuna watu wakubwa wanakuja kulia mbele za wananchi ati nchi inaibiwa. Walikuwa wapi wakati TL akihangaika Rufiji, Bulyankulu, na kwingineko?
..TL anafanya harakati popote pale ambapo kuna ukiukwaji wa sheria na haki za binaadamu. Haijalishi ni jimboni kwake, au ktk mkoa wake.
..kama unaona hayo ni mapungufu, tueleze wananchi wa KANDA YA ZIWA wamefaidika vipi kwa wabunge wao kutokufanya harakati za kupinga uporwaji wa rasilimali zao.
..je, mwananchi wa Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Tabora, ana hali nzuri ya maisha kuliko mwananchi wa jimboni kwa TL?
..kwa mtizamo wangu nchi hii inahitaji wanaharakati na wapambanaji wengi kama TL.