Tundu Lissu hajawahi kunyamaza na hatonyamazishwa kamwe

Tundu Lissu hajawahi kunyamaza na hatonyamazishwa kamwe

Mwaka huu atapigia kelele zake ukonga kwa wafungwa wenzie ila wafungwa watafaidika atakuwa anawaandikia rufaa wafungwa wenzake
Hilo nalo litakuwa janga la kitaifa maana
mahabusu karibia wote watashinda kesi zao.
Na hapo atakuwa amewatumikia wananchi wanyonge,
waliopo ndani kwa sababu ya unyonge wao.
 
Hili la kamata kamata ninawasihi wasaidizi ktk dola yetu kutambua Siasa ina sura nyingi, huyu na wengine wanatafutiza au kujikuta majanga na kuishia mikononi mwa wana Dola ni SIASA. Kuna wasaa Siasa itatutaka hawa wasikilizwe tena tukiwalinda, Rais ana mengi ya kuyaweka sawa na trend hii ni kumuandalia wakati mgumu wakati wa Siasa za wazi. Hekima itangulie ili kumlinda Rais na aweze kukamilisha azma zake na kupata utetezi wenye ushawishi mbele umma. Lissu ama anatengezwa na kamata kamata hii ama anajitengeneza kwa kuwa target wa Kamatakamata kuwa Mpinzani halisi wa Rais wetu. CCM especially Comrade Polepole tumia ujana wako kuliangalia hili na ushauri wazee.
 
Tatizo kubwa la huyu bwana ni kutokujua nini anachokifanya na ni kwa maslahi ya nani. Wenzie wenye akili nzuri hizi harakati wanafanyia nje ya mikoa yao. Ndiyo maana utakuta mikoa ya wafamaji wenzie at least hali si mbaya sana. MKOA anakotoka huyu bwana ni hali ngumu sana kimaendeleo. Ni moja kati ya mikoa maskini kabisa hapa Tanzania. Vita ikipiganiwa katika nchi yako, hata kama utashinda lakini utakuwa umepata hasara kubwa. Ni vema akabadili staili, badala ya kuhamasisha maandamano aanze kuhamasisha maendeleo katika mkoa wake ili awe sawa na wenzie. Kwa hilo hata mimi ningeona kama yuko vizuri.
Kwani yeye ni mbunge wa mkoa? Nilifikir ungesema jimboni kwake badala ya mkoa... Maendeleo ya mkoa c aulizwe mkuu wa mkoa? Ni mtazamo wangu lakin
 
Naomba hii iwe angalizo kwa wote wanaodhani wanaweza kumnyamazisha Tundu Lissu. Ukifuatilia tangu awamu ya 3 huyu mtu alikuwa mwiba halisi kwa kuanika ukweli kuhusu wachimbaji waliozikwa kibabe tena wakiwa hai kwenye mashimo ya madini huko kanda ya ziwa ili kupisha mwekezaji, Mh. Lyatonga Mrema na IGP Mahita wanalifahamu hili vizuri sana.

Pamoja na vitisho vyote Lissu hakuwahi kumpigia magoti mtu yeyote na mwisho wa siku ukweli ulikuja kubainika, Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wahanga wale, Amina.

Awamu ya nne ya Mh Profesa Kikwete makali ya Lissu ya kusimamia ukweli wote mnayafahamu, kuna wakati Dk Kikwete alinukuliwa akisema " NI HERI DR SLAA AENDE IKULU KULIKO TUNDU LISSU AINGIE BUNGENI " Dr slaa hakwenda ikulu lakini Tundu Lissu aliingia bungeni kwa kishindo.

Huyu mtu hanyamazishwi na wanadamu, atanyamaza pale tu Mungu atakapomtwaa kwa hiyari yake lakini si kwa hila za wanadamu wenye mwili na nyama.
Usemayo ni kweli, mimi namfahamu kabla hajaingia kwenye siasa, Lisu hanaga woga wala unafiki. Tatizo kazaliwa kwenye nchi ya baba wa unafiki
 
Walibembelezwa wakati wa awamu ya iliyopita, huu ni wakati mwingine, ni lazima nidhamu iwepo katika nchi.
Nidhamu gani.Mafisadi wote wako CCM.Kuanzia escrow mpaka maafa ya bukoba mpaka kivuko cha bagamoyo.
Ifike mahali watu washindane kwa nguvu za hoja na si nguvu za dola.Katiba yetu ina mapungufu sana kama alivyosema Mwl.Nyerere.
 
Nidhamu gani.Mafisadi wote wako CCM.Kuanzia escrow mpaka maafa ya bukoba mpaka kivuko cha bagamoyo.
Ifike mahali watu washindane kwa nguvu za hoja na si nguvu za dola.Katiba yetu ina mapungufu sana kama alivyosema Mwl.Nyerere.
Bila polisi , ccm ni wepesi kuliko pamba .
 
Niliweka angalizo hili mapema sana , si kila binadamu anaweza kufanya atakacho , na ieleweke kwamba Tangu enzi na enzi shetani hakuwahi kumshinda Mungu .
 
huwezi kuniambia kuwa lissu ni mwanasiasa makini nikakukubalia hata kidogo huyu c mwana siasa bali ni mwanaharakati na mpiga kelele tu mwanasiasa makini cku zote. ujenga hoja zenye mashiko si kuongea kauli zenye kuvunja amani au kufanya ushawishi wowote wenye kuatalisha amani vitendo afanyavyo lissu ni vitendo vya kiharakati si kisiasa Na ni mtu ambae anataka kucheza na akili za watu kwa propaganda dhaifu na kupata attention ya vyombo vya habari lakini linapo kuja swala. la hoja zenye mashiko lissu ni mweupe huwezi hata kumlinganish@ na mnyika, zitto,
Mkuu kijijini kwenu ndo wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom