Tundu Lissu hakubaliki kwao? Singida haijawahi kuwa na Mbunge wa CHADEMA kwenye Majimbo yote 8 ya Singida kasoro analotoka yeye!

Tundu Lissu hakubaliki kwao? Singida haijawahi kuwa na Mbunge wa CHADEMA kwenye Majimbo yote 8 ya Singida kasoro analotoka yeye!

Kwani aliwahi kugombea majimbo yote nane???
Kigoma wanamkubali sana Zitto ila lini uliona Kigoma ina wabunge hata watatu wa Chadema au Act
 
Kigoma majimbo ya Upinzani ni zaid ya Manne toka 1995
Ni mwaka gani chadema imewahi kuwa na jimbo zaidi ya Moja huko Kigoma? Kwamba alimsurpass Lissu kwa majimbo huyo zitto?

Nitajie tu mwaka gani
 

Tukisema kiongozi anapimwa kea perfomance na sio blabla muwe mnatuelewa.

Toka uchaguzi wa vyama vingi 1995, na Tundu Lissu kujiunga CHADEMA kama mwanachama Muandamizi, takribani miaka 30 sasa.

Singida haijawahi kuwa na mbunge yeyote wa Upinzani ukiacha yeye mwenyewe Tundu Lissu jimboni kwake Singida Mashariki.

Nadhani ndie mbunge pekee ambae Kanda yake haina mbunge hata mmoja wa Upinzani ukiacha Morogoro.

Pamoja na ushawishi wake kwanini wananchi wa maeneo anayotoka hawamuelewi?

Sio Dodoma sio Singida Mambo manne;

1. Hapendi kusaidia wengine
2. Anawadharau wengine
3. Hakubaliki kwao ukiacha jimboni kwake pekee.
4. Hafanyi kazi za chama ipasavyo.

Majimbo nane yeye ana score ya 1/8 alafu analeta hoja za kujenga chama? Unajenga vip chama wakati huna historia hiyo?

Tofaut na Mpinzani wake mkuu, Freeman Mbowe... Ameijenga ipasavyo Kaskazini na zaidi mkoa anaotoka kuna kipindi alikuwa na wabunge 8/9.

Anaongea sana lakini anazidiwa Mbali sana na Heche, Sugu, Mnyika, Bony Yai, Wenje, na viongoz wengine wasio na majigambo lakini kazi zao zinaonekana.

Lissu sio mchapa kazi kama anavyojitapa? Kama hilo dogo anashindwa ataweza vipi kujenga Chadema nchi nzima?

Sasa kama Mke wake kakimbilia USA,Watoto ni RAIA wa USA 🇺🇸 unafikiri wanyaturu wala Punda ni Wajinga ?.
 
Dr Slaa alikuwa na Karatu pamoja na Simanjiro na Babati mjini.
Sio kweli simanjiro limekuja baada ya slaa kuondoka. In fact kuna majimbo kama Hanang chadema tulishindwa kabisa kuyaflip. Babati na Karatu tu ndio majimbo tuliyopata Dr Slaa akiwa peak ila alikua hakubaliki?
 
Mkuu huyo nabii mnaenuhitaji ni aidha hakubaliki kwao au hafanyi kazi za chama mkoani kwake ipasavyo
Hapana kanda ya kati ni CCM fanatics. Sio issue ya Lissu au chadema ila uelewa wa raia wake ni mdogo sana
 
Hapana kanda ya kati ni CCM fanatics. Sio issue ya Lissu au chadema ila uelewa wa raia wake ni mdogo sana
Hapana kaka,

Conversion sio hoja ya wapi ni strong na wapi sio strong...

Kwa mtu wa Caliber ya Tundu angetakiwa awe na majimbo angalao matatu.
 
Hivi mpaka sasa kuna mkoa umesema utampigia kura Mbowe kwenye uchaguzi wa 21?
 
Mkuu kuna vitu vya hisia na kuna uhalisia..
Aida Kenan ni mbunge wa wapi?

Si wameanza kidogo kidogo

Kumbuka mara zote walikuwa wanachagua CCM kipindi hiki wameanza kichagua opposition na pengine wakaongeza zaidi.

Umewahi msikia Aida anapiga kelele?
Sio kweli, katavi na Rukwa ni mikoa inakubali sana upinzani shida ni mifumo yetu tu.

Mfano hapo Nkasi, hiyo kata ya kabwe (kata kubwa zaidi) imeongozwa na chadema tokea 1995!! Yaani CCM ndio upinzani hapo Kabwe kwahiyo Aida alishakuta chadema ina kura zake yeye akazirithi tu.

Nkasi: Wananchi wa Kabwe wadaiwa kuandamana kupinga kuongozwa na upinzani
Angalia video hio ya miaka 27 ya chadema hapo Nkasi
 
Hapana kaka,

Conversion sio hoja ya wapi ni strong na wapi sio strong...

Kwa mtu wa Caliber ya Tundu angetakiwa awe na majimbo angalao matatu.
Nyalandu vipi? Si strongman wa Singida ila alipohamia chadema eti akapoteza jimbo. Tukipata tume huru trust me tutaona real influence ya opposition
 
Jamaa anajijenga mwenyewe hata mkuu wa mkoa wakati huo nafkri alikuwa Paseko Kon alihojiwa na BBC kwamba Singida Mashariki mbona hamna maendeleo,ikaonekana anaongea sana kuliko utendaji.
 
Back
Top Bottom