Tundu Lissu: Hakuna Rais kwenye nchi hii amewahi kutufanyia kitu mbaya kama Rais Samia

Tundu Lissu: Hakuna Rais kwenye nchi hii amewahi kutufanyia kitu mbaya kama Rais Samia

Mungu Ibariki CHADEMA

Sent using Jamii Forums mobile app
Screenshot_2023-07-28-18-05-25-1.jpg
Screenshot_2023-07-28-18-04-35-1.jpg
 
Sina cha Nyongeza make sasa ni operation ya kumg'oa Sa100 na kundi lake, hapa Tundulissu umetunasa wengi tu, we kamwamshe tu Magu huko Chato, sisi tuko nyuma yako.
Lissu akiingia tu kwenye kile kibanda na kutoka basi anageuka lulu. Kuna mtu alisema pia mule ndani kuna nguvu ya ajabu. Nilimfuata pm aniambie akasema hawezi hata kuielezea.
 
Maisha yanaenda kasi sana kwenumye siasa, yule mama aliyeonekana malaika, kila mmoja akaweka matumaini kwake, akasifiwa amekuja kuliunganisha taifa, leo amegeuka sawa na mbwa anayekula watoto wake wa kuwazaa..

Na yule jamaa aliyelazwa Chato, huku akiitwa majina mabaya ya kila aina, leo anaenda kutafutwa alipolazwa ili aambiwe ubaya tunaofanyiwa, tena bila hata yeye kujitetea kwa chochote dhidi ya zile tuhuma zilizokuwa juu yake, amegeuka tumaini!.

Kweli maisha ni kuishi, a ili uishi na watu vizuri lazima uwatendee wema kila dakika bila kujali jana ulikuwa nao vipi, ukijisahau kidogo tu, hayupo anayejielewa atakayekuwa na hamu nawe.
 
Sina cha Nyongeza make sasa ni operation ya kumg'oa Sa100 na kundi lake, hapa Tundulissu umetunasa wengi tu, we kamwamshe tu Magu huko Chato, sisi tuko nyuma yako.
Magu aliwahi kukiri VYAMA vinatuchelewesha.

UOVU wa kuuza bandari zetu, imetuunganisha Watanzania wote.

Tupambane na kundi dogo lisiloitakia mema Nchi yetu,

Amen
 
Maisha yanaenda kasi sana kwenumye siasa, yule mama aliyeonekana malaika, kila mmoja akaweka matumaini kwake, akasifiwa amekuja kuliunganisha taifa, leo amegeuka sawa na mbwa anayekula watoto wake wa kuwazaa..

Na yule jamaa aliyelazwa Chato, huku akiitwa majina mabaya ya kila aina, leo anaenda kutafutwa alipolazwa ili aambiwe ubaya tunaofanyiwa, tena bila hata yeye kujitetea kwa chochote dhidi ya zile tuhuma zilizokuwa juu yake, amegeuka tumaini!.

Kweli maisha ni kuishi, a ili uishi na watu vizuri lazima uwatendee wema kila dakika bila kujali jana ulikuwa nao vipi, ukijisahau kidogo tu, hayupo anayejielewa atakayekuwa na hamu nawe.
Masikini unaamini kabisa anayosema Lisu.
Kweli wajinga ndio waliwao
 
Sina cha Nyongeza make sasa ni operation ya kumg'oa Sa100 na kundi lake, hapa Tundulissu umetunasa wengi tu, we kamwamshe tu Magu huko Chato, sisi tuko nyuma yako.
Hatuwezi kushirikiana na msaliti wa nchi sisi pia usitufananishe na nyumbu wa CDM. Tena koma kabisa mbaya zaidi TL ni mtetea ushoga mwambie aende kwa mabwana zake Ubelgiji.
 
28 Julai 2023
Bukoba, Tanzania

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA - Nitakwenda Chato Nimuombee Magufuli na Nimwambie Ona Madudu Ya Samia

Makamu mwenyekiti CHADEMA taifa Mh. Tundu Lissu akihutubia leo mjini Bukoba , asema haijapata kutokea mradi wa mwekezaji ukapigiwa upatu nchi nzima na CCM kama mkataba huu wa DP World.

Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli hawakuwahi wakiwa marais na kofia ya uwenyekiti wa chama cha CCM hawakuwatuma wanaCCM kuzunguka nchi nzima kutetea miradi ya madini, gesi, DOWANS n.k Mh. Tundu Lissu anawakumbusha wananchi waliojazana uwanjani kusikiliza mkutano wa CHADEMA

Anaendelea Tundu Lissu kusema pamoja na ukatili wote wa Magufuli hakuwahi kuwatuma watendaji wakuu wa CCM kuzunguka nchi nzima kumtetea, hivyo ana mpango wa kufika Chato akamweleze John Magufuli mambo ya ajabu wanayofanya CCM ...
 
Back
Top Bottom