Zanzibar 2020 Tundu Lissu: Hatuna maslahi na Urais Zanzibar, tutatangaza rasmi kumuunga mkono Maalim Seif

Zanzibar 2020 Tundu Lissu: Hatuna maslahi na Urais Zanzibar, tutatangaza rasmi kumuunga mkono Maalim Seif

Tundu Lissu kaleta na kuonyesha vitu tofauti. Atleast kawafundisha watu kusoma word to word sheria na kanuni zetu ili kuepuka maonevu

1. Kathibitisha kwamba hakunaga kitu kinachoitwa ni “kosa kikanuni kufanya mikutano na kuhutubia” wakati wa kukusanya sahihi za wadhamini wa form za urais

2. Huwezi kumuita mtu kizembe tu kwa kutangaza kwenye media. Lazima umkabidhi barua mkononi na mpange nae ratiba ya kukutana na sio kumuharibia ratiba zake

3. Umuhimu wa kutumia reference kwenye mambo muhimu. “If Mgombea huyu alifanya hivi na kuachwa, then na sisi tutafanya hivyo na kuachwa pia”😊

Dr. Mahera inabidi ujipange aisee. Tumia PhD yako vizuri. Wasomi wote hutafiti kabla ya kuact. Usitegemee kupokea ushauri wa maana kutoka kwa Polepole et al. Utapata taabu saana after Nov 2020
 
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
Wafikiri kwa kutumia kamasy nini? Anatangaza na hamna Cha kumfanya. Jino kwa jino mpk 28/10
 
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
Wewe ni mjumbe wa kamati za CHADEMA na ACT mpaka useme kuwa haya maamuzi sio ya chama? Wewe jamaa bure kabisa.
 
Na Lissu pia SIYO MGOMBEA bali ni WAKALA WA MABEBERU wakiwakilishwa na AMSTERDAM ambaye anaendelea kumuongoza na kum - MONITOR Lissu kupitia hiyo gadget waliyomfungia mwilini mwake wakati wa matibabu fake huko Ubelgiji.
Utabaki na hayo hayo kichwani sioni wa kukusaidia kukuambia ukweli.
 
Na Lissu pia SIYO MGOMBEA bali ni WAKALA WA MABEBERU wakiwakilishwa na AMSTERDAM ambaye anaendelea kumuongoza na kum - MONITOR Lissu kupitia hiyo gadget waliyomfungia mwilini mwake wakati wa matibabu fake huko Ubelgiji.
Hayo magadget waliyomuwekea ni hatari kwa usalama wa taifa akiwa popote iwe ikulu au kituo cha jeshi au ofisi ya usalama wa taifa yanapiga picha na kubeba taarifa za ofisi alipo na kuzipeleka nje kupitia computer ya Amsterdam jasusi LA kimataifa

MTU ana mi gadget ya kijasusi ya mabeberu mwili mzima hafai u amiri jeshi mkuu
 
Huyu Lissu atawatoa jasho la meno, pamoja na collabo ya ccm, NEC, polisi na msajili bado jamaa anawaacha gap la millenium.
“Sisi CHADEMA tumetangaza rasmi kumuunga Mkono Maalim Seif kama ilivyo kwa Cheyo na Mrema kumuunga mkono Magufuli na hili tutatangaza rasmi muda si mrefu"- Tundu Lissu.

"Kama ilivyosahihi kwa Mrema na cheyo kumuunga mkono Magufuli, ni sahihi kwa Maalim Seif na ACT kuniunga mkono na ni sahihi kwa Tundu Lissu na CHADEMA kumuunga mkono Maalim Seif na ACT." Mhe. @TunduALissu.

“Nikichaguliwa kuwa Rais nitaunda Serikali ya Chadema kwasababu ya Katiba inavyosema. Kama kutakuwa na uhitaji itabidi tubadilishe Katiba kwanza, na moja ya maazimio ya Chadema ikishinda Uchaguzi Mkuu ndani ya siku 100 tutaanzisha mchakato wa Katiba mpya.”Tundu Lissu

“Bob Amsterdam ni Mawakili wangu, wanashughulika na maswala yangu yote yakisheria ya ndani na nje ya Nchi. Kama Tume imeandikiwa barua basi Mawakili wangu wamekuwa wakitimiza wajibu wao, Kama nilivyosema uchaguzi mkuu hatutaki mchezo" Tundu Lissu

===
LISSU: HATUNA MASLAHI NA URAIS ZANZIBAR, NDIO MAANA TUNAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF

Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema CHADEMA kumuunga mkono Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo sio ushirikiano

Amesema wao hawatatangaza ‘coalition’ ya vyama vyao bali wataungana mkono kwenye maeneo ambayo hawana maslahi nayo. Amesema hawana maslahi na Zanzibar ndio maana wamemuunga mkono Maalim Seif Shariff Hamad

Amesema wamefanya hivyo kama ambavyo Lyatonga Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP walivyomuunga mkono mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli

Amesema hiyo haikatazwi na sheria. Amesema ni muungano wa vyama ndio unatakiwa kisheria kupeleka barua kwa msajili na wao hawana muungano
 
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
... ndivyo kanuni za NEC zinavyotaka?
 
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
Vile vile kama Mtanzania na mpiga kura ana haki ya kumuunga mkono mgombea yeyote. Na amesema Chama nacho kitatangaza msimamo wake....!!
 
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
ndo hivo ameshaamua mtateseka sana
 
Vile vile kama Mtanzania na mpiga kura ana haki ya kumuunga mkono mgombea yeyote. Na amesema Chama nacho kitatangaza msimamo wake....!!
Misimamo inatangazwa mara ngapi? Mara ya kwanza wametangaza mgombea wao wa Uraisi wa Chadema Zanzibar sasa wanakuja na mwingine tena kuwa wanamtaka Seif sharrf Hammad huu utoto
 
Upinzani ulishakufa tangu 2015,kilicho baki ni futuhi.
 
Back
Top Bottom