“Sisi CHADEMA tumetangaza rasmi kumuunga Mkono Maalim Seif kama ilivyo kwa Cheyo na Mrema kumuunga mkono Magufuli na hili tutatangaza rasmi muda si mrefu"- Tundu Lissu.
"Kama ilivyosahihi kwa Mrema na cheyo kumuunga mkono Magufuli, ni sahihi kwa Maalim Seif na ACT kuniunga mkono na ni sahihi kwa Tundu Lissu na CHADEMA kumuunga mkono Maalim Seif na ACT." Mhe. @TunduALissu.
“Nikichaguliwa kuwa Rais nitaunda Serikali ya Chadema kwasababu ya Katiba inavyosema. Kama kutakuwa na uhitaji itabidi tubadilishe Katiba kwanza, na moja ya maazimio ya Chadema ikishinda Uchaguzi Mkuu ndani ya siku 100 tutaanzisha mchakato wa Katiba mpya.”Tundu Lissu
“Bob Amsterdam ni Mawakili wangu, wanashughulika na maswala yangu yote yakisheria ya ndani na nje ya Nchi. Kama Tume imeandikiwa barua basi Mawakili wangu wamekuwa wakitimiza wajibu wao, Kama nilivyosema uchaguzi mkuu hatutaki mchezo" Tundu Lissu
===
LISSU: HATUNA MASLAHI NA URAIS ZANZIBAR, NDIO MAANA TUNAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema CHADEMA kumuunga mkono Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo sio ushirikiano
Amesema wao hawatatangaza ‘coalition’ ya vyama vyao bali wataungana mkono kwenye maeneo ambayo hawana maslahi nayo. Amesema hawana maslahi na Zanzibar ndio maana wamemuunga mkono Maalim Seif Shariff Hamad
Amesema wamefanya hivyo kama ambavyo Lyatonga Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP walivyomuunga mkono mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli
Amesema hiyo haikatazwi na sheria. Amesema ni muungano wa vyama ndio unatakiwa kisheria kupeleka barua kwa msajili na wao hawana muungano