Ndugu zangu,
Kipekee, napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa uhai siku ya leo.
Mh. Tundu Lissu namfuatilia kwa umakini sana, tangia aanze kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini, ni kama vile anafanya kampeni tayari. Japo mimi siyo mwanasheria, ila kwa kumsikia tu, ndugu huyu anafanya kampeni tayari. Na kwa kadri siku zinavyooendelea ndiyo anazidi kujinadi kabisa.
Kwa mfano, alipokuwa Morogoro leo, ameahidi akiingia madarakani ataanzisha : ninamnukuu “a taxper’s bil of right, maana yake nini? Haki ya mlipa kodi”
Kwa mwenendo huu, na tetesi tunazozisikia za ndugu huyu kukatwa kwa sababu ya kuanza kufanya kampeni kabla ya wakati, NEC itakuwa imekosea? Sambamba na hili, nimejiuliza maswali yafuatayo:
Asanteni,
Nawasilisha
Kejuu

().

- Kwanini wagombea wengine wanatafuta wadhamini kimya kimya?
- Je, yawezekana kuna kipengele kinawafanya wagombea hawa watafute wadhamini kimya kimya, ila TL hakijui?
- Au TL amejifanya much know, akawa na tafisri yake? Yaani mwanasheria nguli katoa boko?
- Kwanini TL kwa kadri siku zinavyozidi kusongea ndiyo anafanya kampeni kabisa?
- Au tayari ameshajua kuwa jina lake litakatwa, ndiyo maana ameamua kuanza kufanya kampeni kabisa, yaani, liwalo na liwe?
- Je, akikatwa Chadema watasusia uchaguzi?
- Kama wakisusia uchaguzi, vyama vingine navyo vitasusia
- Kama navyo vitasusia, mwendo utakuwa kama ule wa uchaguzi wa serikali za mtaa?
Asanteni,
Nawasilisha
Kejuu