Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, huku ni kutafuta wadhamini au ni kampeni?

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, huku ni kutafuta wadhamini au ni kampeni?

Halafu hotuba ya leo Waziri Mkuu kaitoa kwa mikwara sana wakati akiongea na wale wapiga dili kwa kutumia jina la Yesu, ukimuona mwambie asitufokee..!!

17 Agosti 2020
WAZIRI MKUU KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WA DINI, KUUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameshiriki katika Mkutano wa Viongozi wa Dini kuelekea Uchaguzi Mkuu Kuunga mkono Juhudi za Rais Dkt John Magufuli.

Source: Global TV online
 
Kwani ule mkutano wa leo unaofanana na liletanasha la mitama pale uhuru ni mkutano au kampeni!
 
Kejuu,

Kuna mwaka alikuja Dr Slaa kutafuta wadhamini, nakumbuka alikuja na chopa, alihutubia maelfu ya wananchi na kutoa ahadi kibao endapo atadhaminiwa na hatimae kuchaguliwa kuwa rais, hivyo sidhani kama ni tatizo vinginevyo kama kuna mabadiliko ya sheria.
 
17 Agosti 2020
WAZIRI MKUU KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WA DINI, KUUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameshiriki katika Mkutano wa Viongozi wa Dini kuelekea Uchaguzi Mkuu Kuunga mkono Juhudi za Rais Dkt John Magufuli.

Source: Global TV online
Ukisikiliza hotuba ya waziri mkuu kwa umakini utagundua kua amepanic, kaanza kutoa lugha za vitisho.
Tundu Lissu kawashika vibaya CCM na hoja zake hazijibiwi kwa propaganda za tumetekeleza.
 
Iki
Ndugu zangu,

Kipekee, napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa uhai siku ya leo.

Mh. Tundulisu namfuatilia kwa umakini sana, tangia aanze kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini, ni kama vile anafanya kampeni tayari. Japo mimi siyo mwanasheria, ila kwa kumsikia tu, ndugu huyu anafanya kampeni tayari. Na kwa kadri siku zinavyooendelea ndiyo anazidi kujinadi kabisa.

Kwa mfano, alipokuwa Morogoro leo, ameahidi akiingia madarakani ataanzisha : ninamnukuu “a taxper’s bil of right, maana yake nini? Haki ya mlipa kodi”

().​

Kwa mwenendo huu, na tetesi tunazozisikia za ndugu huyu kukatwa kwa sababu ya kuanza kufanya kampeni kabla ya wakati, NEC itakuwa imekosea? Sambamba na hili, nimejiuliza maswali yafuatayo:
  • Kwanini wagombea wengine wanatafuta wadhamini kimya kimya?
  • Je, yawezekana kuna kipengele kinawafanya wagombea hawa watafute wadhamini kimya kimya, ila TL hakijui?
  • Au TL amejifanya much know, akawa na tafisri yake? Yaani mwanasheria nguli katoa boko?
  • Kwanini TL kwa kadri siku zinavyozidi kusongea ndiyo anafanya kampeni kabisa?
  • Au tayari ameshajua kuwa jina lake litakatwa, ndiyo maana ameamua kuanza kufanya kampeni kabisa, yaani, liwalo na liwe?
  • Je, akikatwa Chadema watasusia uchaguzi?
  • Kama wakisusia uchaguzi, vyama vingine navyo vitasusia
  • Kama navyo vitasusia, mwendo utakuwa kama ule wa uchaguzi wa serikali za mtaa?
Kwa tafisri yangu isiyokuwa rasimi, namalizia kwa kusema, kuna asilimia 95% Mh. TL atakatwa kwa sababu anatafuta wadhamini huku akifanya kampeni.

Asanteni,

Nawasilisha
Kejuu

Ikifika muda wenyewe wa kampeni atakuwa kashakata pumzi, shauri yake!
 
God appointed him!..
 
Mkateni kinuke. Mbona Jiwe miaka 5 kafanya kampeni peke yake? Mpaka na matamasha kabisa ya kumnadi. Afterall bado Lissu hajapitishwa kuwa mgombea wa Urais hivyo hiyo sio kampeni usihofu.
Hakiwezi kunuka hata akikatwa. Ubavu huo hamna! Mmevurumishwa Hai na vitoto vidogo mbona hakikunuka? Msijaribu kutisha, maana hakuna anae tishika. Na pia kuhusu sheria, Lissu hajui kuzitafsiri kwa undani - ndiyo maana hajashinda kesi hata moja miaka hii.
Mahakamani hakuna kuhonga awamu hii!
 
17 Agosti 2020
Mikumi, Morogoro
Tanzania

MHE TUNDU LISSU AINGIA JIMBO LA MIKUMI NA KUPOKELEWA NA UMATI MKUBWA WA WANANCHI

Tundu Lissu akumbusha juu ya nasaha za kauli mbiu ya Mwalimu Nyerere iliyosisitiza utu ni UHURU katika kila kitu yaani Uhuru na Kazi pia Uhuru na Maendeleo na Uhuru na Umoja

Tundu Lissu anauliza kwanini Nyerere hakutanguliza Ma-barabara na Maendeleo au Miundo-mbinu na Maendeleo alijua kwanza utu wa mtu kupitia Uhuru kwanza ndiyo kitu muhimu ili kupata Maendeleo ya Kweli.

Tundu Lissu anasema binadamu siyo mifugo ukaamua kuondoa utu wao wa kuwa HURU kwa kisingizio kuwa kwa kuwanyima uhuru wa utu wao, kuwanyanyasa , kuwabeza ndiyo unataka kuwaletea Maendeleo.
source: CHADEMA MEDIA TV
 
Nadhani akianza kampeni mtaumwa vichomi na sonona.

Kwa ufupi tu hiyo inaitwa SAFISHA NJIA.
 
Back
Top Bottom