Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, huku ni kutafuta wadhamini au ni kampeni?

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, huku ni kutafuta wadhamini au ni kampeni?

Waliyataka wenyewe,agenda zote wamempa wenyewe.Mteke watu,mfunge wengine jela kwa kuwasingizia/kuwaonea,mnashambulia kwa risasi na mapanga halafu mkiambiwa mnadai kaanza kampeni? Mbona CCM imefanyiwa Tamasha,Imezindua nyimbo za kampeni,kongamano la wenye Dini zao ambazo zimeruhusiwa kuchanganyikana na siasa za CCM Mpya hamwezi kuona kuna tatizo ila kwa Mh.Lissu mnachonga midomo.Mnatishia kumkata,kateni muone kitakachofuatia.
Subiri utaijua NEC ni nani
 
Ndugu zangu,

Kipekee, napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa uhai siku ya leo.

Mh. Tundulisu namfuatilia kwa umakini sana, tangia aanze kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini, ni kama vile anafanya kampeni tayari. Japo mimi siyo mwanasheria, ila kwa kumsikia tu, ndugu huyu anafanya kampeni tayari. Na kwa kadri siku zinavyooendelea ndiyo anazidi kujinadi kabisa...
Kuna mtu moja alisikia kiahidi kama ataongezewa mitano atageuza Tanzania kama ulaya kisha akagawa minoti bila woga ahadi hewa zisizotekelezeka swali langu menyekiti alikua natafuta wadhamini au likua anapiga kampeni?
 
Kejuu,

Huyu ndo Lissu kama Lissu!!! Umesikia hoja hizo zilivyo zamoto? Mtamwezea wapi?

Lazima mvue nguo mwaka huu. Eti Lissu hana hoja, akitema madini mnakimbilia kaanza kampeni. Na bado CCM mtaongea lugha zote mwaka huu! [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Moravia nguo nyie aisee. Huku wasanii huku viongozi wa dini zote mtaponea wapi?
 
Kuna mtu moja alisikia kiahidi kama ataongezewa mitano atageuza Tanzania kama ulaya kisha akagawa minoti bila woga ahadi hewa zisizotekezeka swali langu menyekiti alikua natafuta wadhamini au likua anapiga kampeni?
We unaonaje?
 
Nyie si mmefanya tamasha la wavuta bange pale uwanja wa mkapa, tena na leo wale watoza sadaka waliitisha kongamano la kumpongeza mgombea wenu au?

Mbona mnawashwawashwa sana na Lissu?
Acha tu hawa jamaa wao na lissu chochote atakachofanya lazima wajambe cheche,tushawaambia wawe na hedex,panadol,pedzinc nyumbani muda wote maana wataumwa vichwa na matumbo ya kuhara sana kipindi hiki.
 
Moravia nguo nyie aisee. Huku wasanii huku viongozi wa dini zote mtaponea wapi?
Hivi mnawaonaje watanzania? Mtanzania gani atashawishiwa na hao wasanii wenu uchwara?

Mtanzania gani atashawishiwa na hao wajasiliamali wenu uchwara?

Kwanza Polee sana! Naskia salamu za Morogoro na Iringa leo zimefanya Lumumba mtafutane
 
Huu sasa wivu.magufuli na wapambe wake Wakina musiba wamepiga kampeni tangu mwaka 2016 mpaka leo.lissu kaja juzi tuu mmeanza kupiga kelele.
 
Kwa Maoni yangu Mpaka sasa hakuna Mgombea aliyeidhinishwa na Tume, Kwa hiyo Hakuna Kampeni. Kinachofanyika sasa ni kuomba Watu wakudhamini ugombee.

Unapoomba udhamini ni lazima ujieleze kwa ufupi kuonyesha Mtazamo wako kiujumla. Haya unaweza kuyafanya kwa wazi au kwa kificho.itategemea njia uliyoichagua.

Sijamsikia Tundu Lisu akisema Naomba Kura zenu ; wakati bado hajawa mgombea wala hakuna kampeni .Kinachofanyika sasa ni ni hatua za Mchakato wa kisiasa unaotambulika na Tume.
 
Inawezekana hujausoma vizuri uzi wangu mkuu

Unapataje Wadhamini bila kuwashawishi kwa kuwaeleza ni Nini utakwenda kufanya?

Mbona mawaziri wako kila Pembe ya nchi wakielezea alichokifanya rais kana kwamba alifanya hayo PEKE YAKE?

TUSEME MAWAZIRI WANAMFANYIA KAMPENI RAIS KABLA YA WAKATI?

UZINDUZI WA MELI,
MARA, RAIS ALITOA FEDHA ILI WAKULIMA WA KOROSHO WAKIOKOPWA WALIPWE,

DUMILA waliomba 50,000,000/= za kujengea vibanda, rais akasena, atawapa 100,000,000/= ni kutoka bajeti ipi?

Anapotoa FEDHA Kama njugu, je, Bunge lilipitisha mgawo wa hivyo?

2480339_IMG_20200808_090022.jpeg
 
Hawa CCM Mpya wameziba media zote kuhoji wapinzani au kuwapa nafasi kupitia TV/Radio/ Mikutano ya wazi /Ndani kuzungumza na Taifa wapate kuwafahamu kwa miaka 5 sasa.

Hivyo njia moja ya kushawishi waTanzania wakubali kuwaamini ili kuwadhamini ni kwa kukutana nao kama hivi kwa kujitambulisha wao ni nani na kutoa historia na elimu ya uraia kuwashawishi wananchi haki yao ili wawadhamini.
 
Subiri utaijua NEC ni nani
Kazi za NEC ndiyo hizo za kukata wagombea?Kwa nini NEC inaonekana kushinikizwa kumkata Mh.Lissu?Ajabu ni kuwa wao pia wanajiandaa kutekeleza matakwa ya wateuzi wao.
 
Siyo kampeni hiyo bali anafanya siasa.

Na haki ya kufanya siasa ipo kwa mujibu wa katiba.

Haki hiyo ya kufanya siasa na freedom of speech and right to assembly haiondoki kwa ratiba za NEC

Katiba ya nchi imempa mtu haki ya KUCHAGUA na KUCHAGULIWA, na vigezo vya mtu kuchagua au kuchaguliwa vimeelezwa vizuri kwenye katiba.

NEC haina power za kumnyima mwananchi haki ya kisheria ya kuchagua au kuchaguliwa kwa kutumia vikanuni uchwara ambavyo havina uzito wowote juu zaidi ya kikatiba na sheria!

Point kubwa sana mkuu. Makatazo yasiyokuwa ya kisheria yanabaki ni ubinyaji haki, uhalifu!! Na hawawezi kumshitaki kwa anayofanya kwa sababu katiba imeruhusu.

Mtazamo wa mkuu au polisi hauzidi haki inayotolewa na katiba. Tumezoea sana “kawaida” kuifanya sheria ndio maana tunapeana taabu.

Mtu anaamka na kusema “hakuna tena siasa mpk wakati wa uchaguzi”. Keshoye anasema “mtu akafanye siasa kwenye eneo alilochaguliwa”.

Je akiwa kiongozi wa kitaifa asifanye siasa kitaifa?? Je asihamasishe wanachama kitaifa? Halafu baada ya hapo yeye anapita kila sehemu ya nchi akiwananga wananchi “mlikosea kuchagua”!!!
 
Kejuu,

..mbona Jpm na CCM wamekuwa wakifanya kampeni muda wote wakati vyama mbadala vilipokuwa vimefungiwa?

..kile alichofanya waziri mkuu na viongozi wa dini hakikuwa mkutano wa kampeni?

..kwanini mnaogopa na kuchukia ushindani kiasi hiki?

..hebu BADILIKENI.
 
Back
Top Bottom